Aliyejeruhiwa TEGETA kwa kupigwa risasi afariki dunia

Kuna ubaya gani mtu akiuliza swali ajibiwe?kwani Jf mmeambiwa ni ya kutoa taarifa tu na sio kuuliza pia?

OOOOOO kama nikweli Mungu ampumzishe mahali pema kwenye Amani ya milele ..kwani vitu vyenye Ncha kali Vitatumaliza hapa kwa Dunia
 
Wajameni habari zenu.
Nimesikia habari za kufariki kwa yule ndugu aliyepigwa risasi na polisi kule Tegeta wakati wa operesheni ya Polisi kuondoa magari yanayoegeshwa pembezoni mwa barabara, je kuna ukweli wowote?
Hata kama hajafa, tunataka Said Mwema ajiuzulu.
 
Mimi ninaifahamu vyema familia ambayo polisi walimvizia mtoto wao wa mwisho aliyekuwa mfanya biashara. Wakamkamata asubuhi akienda kununua bidhaa. Wakachukua pesa yote na simu ya mkono kisha wakampiga risasi halafu wakatangaza wameua jambazi. Polisi damu ya kijana huyu, kilio cha baba, mama, ndugu, na marafiki hakitawaacha salama. Huu ni wakati wa kulitafakari upya jeshi hili. Mpaka hapa tulipofikia inatosha yaani jeshi zima linanuka damu na rushwa tupu.
 
Rapherl

Hakika naunga hoja yako mkono na ukijaribu kufuatilia kwa karibu mauaji yote kwa raia waliotangulizwa mbele ya haki na mapolisisiem hakika ni wale wote tajwa hapa chini.

Marehemu MUNGU amlaze mahala pema peponi!


Hili ndo tatizo la kuajiri Askari wengi bila kuwa na mpango mzuri wa mafunzo haiwezekani Kuruta akae miezi mitatu chuoni alafu aje uraiani uniambie kashahitimu!,hakuna mtu anaye jifunza silaha miezi mitatu.lazima utakuwa muuaji tu,Angalia asilimia kubwa ya Askari wanaoua ni hawa ambao wametoka depo miaka ya karibuni
 
Last edited by a moderator:
bado na mwandishi kavamiwa wa tanzania daima kavamiwa nyumban kwake na polis kapigwa risasi,polis wanajichanganya wanasema walikuwa kwenye harakat za kusaka majambaz,wananchi tumelala tu
 
mkuu nawe huna taarifa duh umetukatya steam make tulitaka kujua kumbe nawe unauliza swali lilelile. sawa mkuu

hapana ndugu, mimi nimepata kusikia sikia tu na ndio maana kwenye bandiko mama nimeweka kama tetesi ili wenye taarifa zaidi watuhabarishe....kumbuka pia kuna uwezekanano wa kuongezea comments za wadau wengine kwenye bandiko mama
 
Ni kweli amefariki - kwenye Radio One asubuhi ya leo wametangaza - AISEE ............ yaani.............. Halafu kijana only 15 years - so prime of his age ............this is not fair .... jamani...........

MASKINI MAMA YAKE, MASKINI BABA YAKE ........ MASKINI NDUGU ZAKE ....... MASKINI RAFIKI ZAKE...........

KWA KWELI INAUMA SANA ................ HUU UMWAGAJI DAMU NI KAFARA YA CHICHIEM ... NITAKOSEA???? MBONA BASI SERIKALI HAICHUKUI HATUA YOYOTE JAMANI???????

kwa mara ya kwanza NATAMANI KWENDA MBINGUNI ......... DUNIA IMENICHOSHA..........:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
 
Hili jambo linasikitisha sana ndugu zangu.

Where are the lawyers??? We should sue these ****** who are finishing us off in our own streets, houses and backyards!! We need to make too expensive for them to continue killing us with impunity. We could even form a class act a lawsuit mounted against the police by a big group of people and if we fail in these courts, we go all the way to the hague. This is what we need. Mwangosi, mwandishi wa jana yule, huyu kijana wa tegeta, wale wafuasi wa chadema lukuki, dr ulimboka, and so on and so on. The list is endless na wameshajenga mazoea kuwa hatuwafanyi lolote.
 
Hakuna mwenye ubavu wa kuingia mtaani hapa wala hakuna mtu ambaye ngozi yake imeungua vya kutosha kusema liwalo na liwe kila mtu anacho cha kupoteza akiingia mtaani na hivyo hayo ni maneno ya uchochezi. Kuingia mtaani ni kimbunga au mafurika yanayokuja kwa wakati muafaka ambapo watu hawana cha kupoteza. Hali hiyo haijafikia na bado iko mbali sana tupigie kelele mabadiliko ya kiutendaji lakini sio mambo ya kuingia mtaani: tena ungekuwa serious ungeanza wewe sio kuongopea wenzio
 
Jeshi la polisi limegeuzwa kuwa jeshi la wezi, majambazi na wauaji. No one is safe these days. Watu kibao wanauawawa na polisi bila sababu ya kueleweka. Raia tuchukue hatua na kujilinda wenyewe. Hivi vitu vizito vyenye ncha kali vitatumaliza kama tutaendelea kuwachekea hawa polisi ilhali wakitumaliza kidogo kidogo na hawachukuliwi hatua hata kidogo. Silaha zinanunuliwa kwa kodi zetu kisha zinatumiwa kuangamiza watanzania wenzetu wasio na hatia. Ngoja yakukute wewe, ndugu yako au mtu wako wa karibu ndio utajua namaanisha nini exactly.
 
Hakuna haja ya kungoja kama kweli uko serious anza wewe chukua petroli jimwagie kisha jipige kiberiti mbona wenzio wamefanya hayo?
 
Back
Top Bottom