BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,217
.......hapo ndio umuhimu wa condom unapoonekana
umefanya vema kwamtoro.nafikiri pendo anahitaji shughuli ya kumkeep busy kwa sasa ili angalau asahau haya mapito. wakati anaendelea kutafta kazi anaweza hata jifunza course fupi fupi kama kozi za computer hivi. vipi wazazi wake au anko hana uwezo wa kumuendeleza kielimu au hajawaambia kama ana mpango wa kuendelea kubukua?
No! Leo nipo pande za African then jioni nitakuwa Calabash Mwenge. Tukutane mdau
Kwani wewe mtu akija pekupeku huwezi kukataa? au tatizo huwa hamna kauli? Lakini mbona mkiwa mnaongea mnajiona wajanja iweje mkifika kitandani mzubae? Na siyo kila mwanaume atakuuliza hali yako ya mzunguko wa hedhi wengi wao elimu ya uzazi hawafuatiliii hivyo ni jukumu lenu kuwa makini!
umefanya vema kwamtoro.nafikiri pendo anahitaji shughuli ya kumkeep busy kwa sasa ili angalau asahau haya mapito. wakati anaendelea kutafta kazi anaweza hata jifunza course fupi fupi kama kozi za computer hivi. vipi wazazi wake au anko hana uwezo wa kumuendeleza kielimu au hajawaambia kama ana mpango wa kuendelea kubukua?
hiyo mimba iliingia yenyewe!!!!!!!!!!!
huwa sipendi kama jambo lishatokea badala ya mtu kushauri nini kifanyike unaanza kulaumu. hebu tu fikiria pendo angekuwa ni mdogo wako ungejisikiaje kwa haya uliyoyaandika? kama huna cha kushauri pole tu inatosha na kumlaumu pendo haisaidii maana maji yashamwagika. lakini wanaume mtambue jukumu la kuzuia mimba zisizotarajiwa ni la kwenu wote. muhimu kujadili na mpenzi wako mapema. hata kama mwisho wa siku mwanamke ndio muathirika zaidi ila unajiskiaje kuharibu maisha yake? unajiskiaje mwanamke mwanamke akilia na kujutia nafsi yake kwa ajili yako? mwisho wa siku muone mungu hawapi mnayostahili sababu mmemkosea.
mabinti wana mitihani sana nafikiri wengi bado hawaijui vizuri elimu za uzazi..kwa unavyomuona ni binti anaejielewa au ndio vile tena kashajikatia tamaa na maisha?Kweli Husninyo
Nimeyafanyia utafiti wa kina maelezo yake. Inaelekea wazazi wake wanao uwezo mdogo, na inawezekana kabisa pasipo shaka Clemence alifungua njia. Ni msichana before akuwa kwenye mahusiano. Mjomba wake anayemtegemea nimegundua akuzaa kwa uzazi wa mpango. Ana watato wengi ambao wengi wao wapo secondary na wachace wapo primary. Kwa hiyo mjomba wake wakwake wenyewe wanamtoa jasho.
Nakubaliana na wewe kuwa jukumu la kuzuia mimba ni la watu 2, lakini kama wewe husemi nani atakusemea? Nimekuwa nikifanya utafiti wa kuwauliza wasichana kuazia 2006, wengi wao haswa waliosoma kuanzia sekondari walikuwa wakijua jinsi ya kujizuia kutokupata mimba, lakini wasichana wengi waliosoma kuanzia 2008 hadi leo hawajui hata siku mbaya katika mzungungo wao wa hedhi, nilichokuja kugundua ni kwamba hamsomi somo la biolojia mkalielewa, kwani hata wadogo zangu 2 wanajua 1 hajui na sas yupo form 5, unadhani wanaume wa sasa digitali waache kufuatilia mziki waanze kufuatilia kumuepusha mwanamke asipate mimba ni abadan.
mabinti wana mitihani sana nafikiri wengi bado hawaijui vizuri elimu za uzazi..kwa unavyomuona ni binti anaejielewa au ndio vile tena kashajikatia tamaa na maisha?
Pendo amekosa tu kujitambua na kujiamini. Ukiwa kama mshauri wake msaidie ajitambue kuwa Clement hamfai, hastahili kuwa naye na sie wa hadhi yake kimaadili na hata kimapenzi. Kitendo cha Clement kumshauri tu kuitoa ile mimba ilikuwa ni dalili tosha kuwa Clement hakuwa amedhamiria kuishi naye kama mpenzi wake. Mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na nia angemwambia imeshatokea, twende kwa wazazi tukaji'shtaki', tuombe msamaha tupewe Baraka ya kuwa mwili mmoja tulee mwanetu. Lakini kwa kuwa Clement hakuwa amempenda kwa dhati ndio maana alimwambia akaitoe. Pili mwambie Pendo kuwa yeye ana bahati kuwa MUNGU amemwonyesha mapema kuwa Clement siye, ingekuwa vipi kama angeolewa naye kasha Clement akamletea mwanamke mwingine ndani na kuanza kuishi naye? Au angemtesa kimapenzi? Mwisho mwambie Pendo aamke Clement siyo wake, wake yupo na anavyozidi kumfuata Clement ndivyo Clement anavyozidi kumdharau na anaweza hata kumtake for his advantage ili tu ajifurahishe. Na pia kwa kumfuata fuata Clement na kulilia asipopendwa hajitendei haki yeye na nafsi yake. Mdedicatie wimbo wa Serebuka wa Mwasiti
Maskini aje kwangu nitampoza roho