Nadhani hili linachangiaSikuwahi kukaa naye zaidi ya mwezi mmoja lakini hii sikuona kama ni tatizo maana wapo hata tuliodumu miaka 3 lakini bado hatukuoana.
Nipo hapa mume mwema twende PM tukayejengeNikiwaza vile kila siku naomba Mungu anipe mume mwema, lakini kwa ninayokutana nayo humu kila iitwapo leo akili inazidi tu kunichemka..!!
Habari wakuu...
Kisa changu ni huyo dada mmoja ambaye katika pitapita zangu za kusaka ni nani atakuwa mama wa watoto wangu, nikaona ndiye anafaa. Ni msichana mrembo kwa sura, rangi ya mtume na umbo namba nane. Tabia zake nilijiaminisha kuwa ni njema kupitia watu wa karibu wanaomzunguka ukijumlisha na uhudhuriaji wake wa ibada kila Jumapili.
Baharia kwa kuona hayo na ukizingatia umri wangu ulikuwa tayari unaruhusu kuvuta jiko, ikabidi nitume ombi la ndoa. Kwa bahati nzuri, mtoto wa watu akatiki kuwatelekeza wazazi wake ili aishi na mimi. Kabla ya yote hayo alisema yeye ni mcha Mungu na hapendi kabisa mwanaume anayetumia pombe au vilevi vingine. Mjuba kwakuwa nilikuwa nimekufa nimeoza, haikuwa shida kuachana na vitu hivyo viovu maana havikuwa na faida kwangu.
Miezi mitatu nikiwa naye, dada wa watu akaanza kubadilika. Kwanza, hawapendi ndugu zangu hasa wadogo zangu, analala hadi saa 4 bila kujali kuwa anayo majukumu kama mama wa familia. Kilichoniua zaidi ni zile text mbili nilizozikuta kwenye simu yake baada ya kuipekua yeye akiwa amelala fofofo. Amekuwa mkali kwangu hata kwa jambo dogo, kuna wakati najawa na hasira natamani nimchape ngumi za kila rangi ila nahofia maana naweza kumjeruhi vibaya.
Solution yangu imebidi nirudi kwenye starehe yangu ya kula mitungi na nimekuwa mlevi wa kupindukia kuliko hata mwanzo. Huyu Grace atakuja kunisababishia matatizo makubwa. Natamani kuwaeleza wazazi wake ila ninawaheshimu sana kwa jinsi wanavyoniheshimu pia.
Nipo njia panda, ngoja niende baa muda huu maana amekataa kupika eti anasema anaumwa japo tangu asubuhi alikuwa mzima na muda sio mrefu amerudi kutoka saloon kusukwa.