Alinizuia pombe ndiyo nimuoe ila leo kawa chanzo changu cha ulevi wa kupindukia

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Habari wakuu...

Kisa changu ni huyo dada mmoja ambaye katika pitapita zangu za kusaka ni nani atakuwa mama wa watoto wangu, nikaona ndiye anafaa. Ni msichana mrembo kwa sura, rangi ya mtume na umbo namba nane. Tabia zake nilijiaminisha kuwa ni njema kupitia watu wa karibu wanaomzunguka ukijumlisha na uhudhuriaji wake wa ibada kila Jumapili.

Baharia kwa kuona hayo na ukizingatia umri wangu ulikuwa tayari unaruhusu kuvuta jiko, ikabidi nitume ombi la ndoa. Kwa bahati nzuri, mtoto wa watu akatiki kuwatelekeza wazazi wake ili aishi na mimi. Kabla ya yote hayo alisema yeye ni mcha Mungu na hapendi kabisa mwanaume anayetumia pombe au vilevi vingine. Mjuba kwakuwa nilikuwa nimekufa nimeoza, haikuwa shida kuachana na vitu hivyo viovu maana havikuwa na faida kwangu.

Miezi mitatu nikiwa naye, dada wa watu akaanza kubadilika. Kwanza, hawapendi ndugu zangu hasa wadogo zangu, analala hadi saa 4 bila kujali kuwa anayo majukumu kama mama wa familia. Kilichoniua zaidi ni zile text mbili nilizozikuta kwenye simu yake baada ya kuipekua yeye akiwa amelala fofofo. Amekuwa mkali kwangu hata kwa jambo dogo, kuna wakati najawa na hasira natamani nimchape ngumi za kila rangi ila nahofia maana naweza kumjeruhi vibaya.

Solution yangu imebidi nirudi kwenye starehe yangu ya kula mitungi na nimekuwa mlevi wa kupindukia kuliko hata mwanzo. Huyu Grace atakuja kunisababishia matatizo makubwa. Natamani kuwaeleza wazazi wake ila ninawaheshimu sana kwa jinsi wanavyoniheshimu pia.

Nipo njia panda, ngoja niende baa muda huu maana amekataa kupika eti anasema anaumwa japo tangu asubuhi alikuwa mzima na muda sio mrefu amerudi kutoka saloon kusukwa.
 
Daaaah ndoa zina changamoto ila naona changamoto zingine zimezidi aiseee sasa unaoa ili upate faraja kwa mtu ambaye unaamka asubuhi ukute chai tayari sasa huyo mke ambaye hapendi ndugu na hapendi kupika huyo sio mke.

Inauma sana
 
Sory mkuu!! najua upo kaunta unapata moja mbili moja moto,naomba niulize,huyo grace ulikaa naye muda kidogo katika uchumba kabla ya kujilipua kuoa? Au shape na rangi ya mtume iliharakisha zaidi!!

Sikuwahi kukaa naye zaidi ya mwezi mmoja lakini hii sikuona kama ni tatizo maana wapo hata tuliodumu miaka 3 lakini bado hatukuoana.
 
Sikuwahi kukaa naye zaidi ya mwezi mmoja lakini hii sikuona kama ni tatizo maana wapo hata tuliodumu miaka 3 lakini bado hatukuoana.
Ok!! simamia uhalisia wako(kama mlevi kunywa,mkorofi onesha ukorofi wako kama upo nao) maana mwenzio kaonesha rangi yake halisi kitabia.Muhimu simama kama baba,embu mpe kerbu mbili tatu ili ajue anaishi na mume na sio boyfriend!!
 
Ok!! simamia uhalisia wako(kama mlevi kunywa,mkorofi onesha ukorofi wako kama upo nao) maana mwenzio kaonesha rangi yake halisi kitabia.Muhimu simama kama baba,embu mpe kerbu mbili tatu ili ajue anaishi na mume na sio boyfriend!!

Ninavyojijua mbona nitaua mtoto wa watu!
 
Back
Top Bottom