Alinizuia pombe ndiyo nimuoe ila leo kawa chanzo changu cha ulevi wa kupindukia

Sikuwahi kukaa naye zaidi ya mwezi mmoja lakini hii sikuona kama ni tatizo maana wapo hata tuliodumu miaka 3 lakini bado hatukuoana.
Nadhani hili linachangia
Nimeshuhudia baadhi ya rafiki zangu wameoa wake dizain yako yaan bila kujuana vzr
Tikitaka za humu ndani mpk mtu anasema anajuta
 
Nadhani hili linachangia
Nimeshuhudia baadhi ya rafiki zangu wameoa wake dizain yako yaan bila kujuana vzr
Tikitaka za humu ndani mpk mtu anasema anajuta

Hakika, uchumba una umuhimu sana
 
Ulifanya jambo la hatari sana kuacha Tiba . Afadhali sasa umerudi kwenye Tiba utapata ahueni . Usirudie tena kuacha Tiba .
😜😜😜 nitakutafuta mkuu nikuoverdose . Piga mambo mkuu life haina kelele wala
 
Ulifanya jambo la hatari sana kuacha Tiba . Afadhali sasa umerudi kwenye Tiba utapata ahueni . Usirudie tena kuacha Tiba .
😜😜😜 nitakutafuta mkuu nikuoverdose . Piga mambo mkuu life haina kelele wala

Itakuwa vizuri sana mkuu
 
Habari wakuu...

Kisa changu ni huyo dada mmoja ambaye katika pitapita zangu za kusaka ni nani atakuwa mama wa watoto wangu, nikaona ndiye anafaa. Ni msichana mrembo kwa sura, rangi ya mtume na umbo namba nane. Tabia zake nilijiaminisha kuwa ni njema kupitia watu wa karibu wanaomzunguka ukijumlisha na uhudhuriaji wake wa ibada kila Jumapili.

Baharia kwa kuona hayo na ukizingatia umri wangu ulikuwa tayari unaruhusu kuvuta jiko, ikabidi nitume ombi la ndoa. Kwa bahati nzuri, mtoto wa watu akatiki kuwatelekeza wazazi wake ili aishi na mimi. Kabla ya yote hayo alisema yeye ni mcha Mungu na hapendi kabisa mwanaume anayetumia pombe au vilevi vingine. Mjuba kwakuwa nilikuwa nimekufa nimeoza, haikuwa shida kuachana na vitu hivyo viovu maana havikuwa na faida kwangu.

Miezi mitatu nikiwa naye, dada wa watu akaanza kubadilika. Kwanza, hawapendi ndugu zangu hasa wadogo zangu, analala hadi saa 4 bila kujali kuwa anayo majukumu kama mama wa familia. Kilichoniua zaidi ni zile text mbili nilizozikuta kwenye simu yake baada ya kuipekua yeye akiwa amelala fofofo. Amekuwa mkali kwangu hata kwa jambo dogo, kuna wakati najawa na hasira natamani nimchape ngumi za kila rangi ila nahofia maana naweza kumjeruhi vibaya.

Solution yangu imebidi nirudi kwenye starehe yangu ya kula mitungi na nimekuwa mlevi wa kupindukia kuliko hata mwanzo. Huyu Grace atakuja kunisababishia matatizo makubwa. Natamani kuwaeleza wazazi wake ila ninawaheshimu sana kwa jinsi wanavyoniheshimu pia.

Nipo njia panda, ngoja niende baa muda huu maana amekataa kupika eti anasema anaumwa japo tangu asubuhi alikuwa mzima na muda sio mrefu amerudi kutoka saloon kusukwa.

Pole sana! Lakini lazima ujue umeletwa duniani kwa makusudi na unalo jibu kama umeshatimiza makusudi hayo au lah! Kuutesa mwili wako kwa sababu ya matatizo ya ndoa yanayotokana na mtu uliyemchagua mwenyewe ni ujinga na ni dhambi!


Ulifanya kosa kubwa kuacha tabia ya ulevi kwa sababu ya mwanamke nafikiri ulitakiwa kucha kwa faida yako na familia yako inayokutegemea lakini si sababu ya huyu anaye kutesa!

Ukweli ni kwamba kwenye maisha ukiona umefanya jambo kwaajili ya mtu fulani jiandae kwa mawili either kulia au kufurahi ....lakini uwe na uhakika zaidi wa kulia na kuwa dissapointed.


Lazima ujue kuwa wewe kama mwaume lazima utatue hayo matatizo yanayo kusibu na si kuyakimbia kwa kujitesa na pombe za kupindukua ....

Nikuhakikishie unalolifanya ni kama kujaribu kujiua kabisa maana unautesa mwili wako bure na pengine utakwisha tuu lakini hutokufa kamwe mpaka utakapo jua unatakiwa kusimama na kuwa kiongozi wa familia yako na kuhakikisha una tatua matatizo yako hayo lakini si kujitesa kwa kunywa pombe kijinga!


Inaonekana kwenu wankutegemea ndio maana unaumizwa na kutopendwa nduguzo...sasa amka achana na ulevi jipange kutatua hayo matatizo...,.uwezi kuendeleza ulevi halafu utegemee ndugu zako watabaki salama!
 
Back
Top Bottom