Aliniunganishia nikaoa mke, ila nina mashaka

Buzi Maarufu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2019
Posts
422
Reaction score
330
Ni Kaka yangu tumezaliwa mama mmoja baba tofauti,miaka 10 iliyopita alinipigia simu akaniuliza kama nina mpango wa kuoa,nikamjibu naaaamu nina mpango huo ila bahati mbaya kila nikiangaza hukuhuku na kule nakutana na vicheche tu,sijampata mwanamke ambaye anafaa kuwa mke

Bro akaniambia "kuna binti jirani yangu hapa yuko vizuri sana kimaadili nakushauri uje umuone kama utampenda ongea naye naamini atakufaa,nikapanga safari kuelekea huko anakoishi brother nikamuona binti nikavutiwa naye baada ya siku kadhaa nikarusha ndoana hatimaye nikafanikiwa kuopoa samaki, mpaka sasa tuna watoto wawili.

Kilichonifanya nije hapa kwenu Wana jukwaa ni huyu mtoto wetu wa pili,anafanana sana na marehemu baba yake Kaka yangu,hili jambo limenipa wasiwasi mkubwa sana sina raha kabisa nahisi broo alishafanya ufuska na mke wangu,binadamu huwa tunafanana Ila kinachonitia wasiwasi zaidi mke wangu anapenda sana kumtajataja brother.

Mara shemeji kafanya hiki mara kile mara shemeji anaishi vizuri na mkewe nk, nisaidieni ndugu zanguni nifanye nini ili nipate kujua ukweli kama mtoto ni wangu au brother?
 
Ngumu kumeza,btw me sijaona,tuwasubiri wakuu wenye ndoa na changamoto zenu.
 
Hapo Kwako Hakuna Tatizo Lolote
Ishi Naye Vema Huyo Mkeo
Mengine Hayo Hayana Mashiko
 
Siutumie njia za Kiintelijensia, hawa walipewa uwezo mkubwa wa akili lkn sisi tukapewa uwezo mkubwa wa kuwashinda.

Kwa mfano....

Eehhh Kaka, jana hukunielewa simu ilikua inasumbua sana, naomba unieleweshe kuhusiana na Gharama na hatua za kufuata ili nipime DNA na wanangu kuna mambo yananichanganya sana Ndugu yangu.

Eehhh sawaaa, ndio ndio, Basi Kesho nitakuja hapo Mimi na Mke wangu na Watoto .

Unakata simu.( Hakikisha hapo alikua anasikia maongezi)

Unaendelea na ubize, kama ni mjuaji mjuaji , Atakuuliza ,iyo DNA vipi, inamana huniamin? Unapiga kimya tu unamwambia Dunia ina Mengi (Mama yangu kanishauri )... kwaivo jiandae Kesho tutaenda wote na watoto .( Chunguza Mabadiliko na muitikio wake kupitia Uso)...

Then Hapo unakua umemshampanga Mtu wako hata wa kituo cha afya tu, mkifika mambo yawe ivi..
(Baada ya blaah blaaah ) ... mtachukuliwa Sampo na kutumwa kisha Majibu yenu ni baada ya Wiki Mbili.

Mnarudi zenu, sasa izo wiki mbili mbili zakusubiri huku ukijifanya "Mama K sisi watu wazima ni busara sana kuniambia ukweli tupate muafaka wa jambo hili kuliko kusubiri mpaka majibu " ..izi wiki mbili hizi lolote linaweza tokea.

SEMA NIN, KWAN UNATAFUTA NINI???... aya ndio kakuambia ukweli nawewe umejua ukweli , utafanya nn??? Usikute unampendaa??kumuacha huwezi na ukweli umeujua?? Huoni kama unamoyo mwepesi utakufa mapema??? Kitanda hakizai Haramu alisikika Mzee mmoja alogongewa Mke

Aya ndo umejiaminisha ni wako, utamwomba msamaha??? Utamwambie asimwambie Kaka yako.??? Sio kwamba ndo utakua umefanya mazingira ya kuliwa sasa?

Kama una moyo mgumu fanya ivo ,utaleta mrejesho mapema.

Ila nadhani ungefunika kombe nakuamin wewe ni Baba wa wanao, nahuyo ndio mkeo, nakwamba Kaka yako hawez fanya hayo.
 
Na ukiujua ukweli ukawa mchungu basi uwezekano wa kupoteza furaha ni mkubwa sana.

Pole sana mkuu..hili jambo ni zito halihitaji majibu mepes.

Dhambi kubwa unayoipitia kwa sasa ni “kuhisi”

Bwana akutie nguvu.
 
Siutumie njia za Kiintelijensia, hawa walipewa uwezo mkubwa wa akili lkn sisi tukapewa uwezo mkubwa wa kuwashinda.

Kwa mfano....

Eehhh Kaka, jana hukunielewa simu ilikua inasumbua sana, naomba unieleweshe kuhusiana na Gharama na hatua za kufuata ili nipime DNA na wanangu kuna mambo yananichanganya sana Ndugu yangu.

Eehhh sawaaa, ndio ndio, Basi Kesho nitakuja hapo Mimi na Mke wangu na Watoto .

Unakata simu.( Hakikisha hapo alikua anasikia maongezi)

Unaendelea na ubize, kama ni mjuaji mjuaji , Atakuuliza ,iyo DNA vipi, inamana huniamin? Unapiga kimya tu unamwambia Dunia ina Mengi (Mama yangu kanishauri )... kwaivo jiandae Kesho tutaenda wote na watoto .( Chunguza Mabadiliko na muitikio wake kupitia Uso)...

Then Hapo unakua umemshampanga Mtu wako hata wa kituo cha afya tu, mkifika mambo yawe ivi..
(Baada ya blaah blaaah ) ... mtachukuliwa Sampo na kutumwa kisha Majibu yenu ni baada ya Wiki Mbili.

Mnarudi zenu, sasa izo wiki mbili mbili zakusubiri huku ukijifanya "Mama K sisi watu wazima ni busara sana kuniambia ukweli tupate muafaka wa jambo hili kuliko kusubiri mpaka majibu " ..izi wiki mbili hizi lolote linaweza tokea.

SEMA NIN, KWAN UNATAFUTA NINI???... aya ndio kakuambia ukweli nawewe umejua ukweli , utafanya nn??? Usikute unampendaa??kumuacha huwezi na ukweli umeujua?? Huoni kama unamoyo mwepesi utakufa mapema??? Kitanda hakizai Haramu alisikika Mzee mmoja alogongewa Mke

Aya ndo umejiaminisha ni wako, utamwomba msamaha??? Utamwambie asimwambie Kaka yako.??? Sio kwamba ndo utakua umefanya mazingira ya kuliwa sasa?

Kama una moyo mgumu fanya ivo ,utaleta mrejesho mapema.

Ila nadhani ungefunika kombe nakuamin wewe ni Baba wa wanao, nahuyo ndio mkeo, nakwamba Kaka yako hawez fanya hayo.
CHUKUA USHAURI WA HUYU JAMAA,KAONGEA VITU KONKII SANA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom