Alinisaliti, shida tunaishi sehemu moja

Alinisaliti, shida tunaishi sehemu moja

Pole sana mkuu, tafuta kitu cha kufanya, maana unaonekana huna kazi unabaki kushinda kwa washikaji, kodi ya nyumba na kula unawezaje? Ndio maana mwenzako alikuona wa nini kuwa na mwanaume suruali.
 
Habari za saizi wana jf,nashukuru mungu anaendelea kunisimamia katika maisha yangu.
Naombeni ushauri, nilikua na msichana niliempenda sana lakini ilifika kipindi akanicheat offcoz niliumia sana tuligombana kufikia kuachana ila mbaya zaid bado tunaishi nyumba moja ya kupanga ila kila mtu na chumba chake.
Inaniumiza ninaposikia sauti yake ninapomuona kila wakati moyo wangu unasononeka sana. Sijui hata nifanyaje na jinsi maisha yalivyo magumu nimetafuta sehem nyingine ya kuishi ila nimekosa. Kwa sasa nimeamua kushinda kwa washkaji cku nzima narudi ucku geto ilimradi tu nipunguze ile hali ya kumsikia na kumuona kila wakati
Kwanini usihame kuepusha shari?
 
ni mpenz wang wa kwanza na wa pili tu ndo nliwapenda saana kihivyo..kwasasa mapenz ya hvyo yalishaisha hamna atakaeniwazisha hvyo mpk nibadli ratiba za maisha yangu aisee...pole mkuu jitahidi kutafuta chumba uhame mahali hapo
 
Kumbe dawa tayari unaijua, sasa kazi hapo hapo kaa kwa washkaj au panga sehemu nyingine , usilegeze mkuu kazaaaaaa
 
sasa ndugu unashinda kwa washkaji kazi hufanyi? unakula nini unaishi vp
 
Hama nyumba dogo,watu stamina hamna harafu unajifanya unakaza!..tafuta hela hao wadudu utawatafuna mpaka uwakinai.
Sio vizuri kuuwaita binadamu wenzio
Wadudu, kumbuka huyu ni mwanamke.
Na mwanamke ni vyema umu heshimu, umjali, umlinde, na si kumtusi na kukejeli kwa maneno ya ajabu.

Kosa la mwanamke mmoja usiwajumlishe na wanawake wengine waliobaki.
Binadamu wako tofauti hatufanani....???


 
Mkuu afadhali yako, kuna wengine walinunua nyumba pamoja, sasa mapenzi yamekwisha, kuuza nyumba ni ngumu, kuhama ukatafute sehemu nyingine ni ngumu. Unaishia kuwa na mpenzi huku unamwambia siwezi kukupeleka nyumbani, akiuliza zaidi unajibu "it is complicated". Dunia hii ni majanga.
 
Aisee we jamaa umenikumbusha mbalii kipindi icho nikiwa kijana bado nilikua na mausiano na manzi tuliyepanga nae nyumba moja situgombana kama wewe kwa akili zangu za kipindi icho nikawa kila wakati naimport manzi mpya sasa iyo miliyo yao ndo ilikua balaa na tulikua tumepakana vyumba mbona aliomba msamaa mwenyewe!
 
Kama hujaafikiana Na moyo wako utamsahau vipi?

Umebeba maumivu ambayo ulipaswa umsamehe Na uyasahau ugange yajayo

Bado una kamzigo ka maumivu moyoni mwako

Fanya hivi

Hebu kubali kabisa moyoni mwako sema nao it's over and u don't want her back

Jikite Na ubusy wa kusaka riziki mtoe mawazoni

Jichanganye Na washkaj kama hivo

Uzur n kwamba hakuna linalodumu Kila jambo linatokea Na kupita maisha lazima yasonge

"Huwezi kuendelea kusoma ukurasa mmoja wa kitabu Kila siku lazima ujue hatma ya story ilikuaje"

Kila la heri
Nashkuru sana aseee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom