Alinikimbia kwa sababu ya shule, sasa anataka turudiane

Kuna vitu huwa naona ni virahisi tu kufikiria na kufikia maamuzi na sual hili ni moja ya mambo marahisi mwanaume kuweza kuwazua na kufikia jibu sahihi.
Huyu ndugu yetu naona anataka kuoa "chuma chakavu". Ukweli ni kwamba hakuiona thamani yake mwanzo na kuamua kwenda kwa mwanaume mwingine, kifupi ni kwamba alifanywa kama plan B.
Mwanamke huyo sio kweli kwamba anampenda jamaa, kama ni mapenzi basi yaliisha zamani.

Last edited by a moderator:
kuwa makini ndugu unaweza kuta tayari mwenzio alisha nasa ugonjwa wetu wa siku hizi matokeo yake atakuja kwako ili akuasambazie nawe. huyo mwache na ujinga wake akae nao
 
kama wanawake wameisha bora umuwowe lakini kama bado wapo(wanaojitambua) ni maramia umwache aende zake,huyu shetani hafi mpaka kiama so ujiandae tena shetani akimpitia ukubaliane na matokeo.
Nimependa mawazo yako bidada
 
Binadamu ambae hajawahi kufanya makosa basi ujue hajawai kufanya chochote katika maisha yake,kukiri makosa na kuomba msamaha ndiyo jambo muhimu zaidi katika maisha...ukianza kujifanya mtabiri wa maisha yako au ukategemea utabiri wa watu kuhusu maisha yako hasa ya mapenzi aisee kila mara utakua ombaomba wa ushauri,umefanya maamuzi yako mwenyewe mara ngapi na haujajutia? kama bado anza na hili na kama pia hujawahi jutia maamuzi yako pia fanya na hili.
 
ilikuwa mwaka 2009 nikawa A-level msichana niliyekuwa nimempanda sana na kumwahidi kumwoa mara baada ya kumaliza shule yeye akiwa amehitimu kidato cha nne na kupata DVN 4 ya 26 tukiwa tumekubaliane aende chuo cha certificate akasome kwa ustawi wa maisha yetu ya baadae lkn kilichotokea ni kwamba yule binti aliingiwa na tamaa na kuamua kuolewa na mwanamme mwingine bila hata kunijulisha niliumia sana lkn nikasonga mbele baada ya miaka 3 yule dada kaachika kwa huyo bwanake na kaamua kwenda college na alizaa mtoto mmoja sasa ananishawishi nimuuoe nakusema kwamba yule hakuwa chaguo lake nakwamba ni matokeo ya shetani sasa nifanyeje wadau

Mshauri arudiane na mume wake usitegeke kirahisi namna hiyo ww,vinginevyo jiandae kuumia zaidi. Kwanza waliozaa huwa hawawezi kuachana sana sana ukisharudiana nae utajiweka kwenye stress tu maana jamaa akija kumuona mtoto wake tu ww pressure juu,ushauri wangu ni kwamba huyo hukuzaliwa nae,kama alivyokukimbia na kwenda kwa huyo jamaa mwenye mtoto nae ndivyo atakavyoweza kukukimbia tena. Anyway kichwa chako ndio serikali yako pia akili za kuambiwa changanya na zako mkuu.
 
mps habari za mbeya, au siku umeama? dah wewe nakushauri uendelee na maisha tu,achana na mjanja mjanja
 
ilikuwa mwaka 2009 nikawa A-level msichana niliyekuwa nimempanda sana na kumwahidi kumwoa mara baada ya kumaliza shule yeye akiwa amehitimu kidato cha nne na kupata DVN 4 ya 26 tukiwa tumekubaliane aende chuo cha certificate akasome kwa ustawi wa maisha yetu ya baadae lkn kilichotokea ni kwamba yule binti aliingiwa na tamaa na kuamua kuolewa na mwanamme mwingine bila hata kunijulisha niliumia sana lkn nikasonga mbele baada ya miaka 3 yule dada kaachika kwa huyo bwanake na kaamua kwenda college na alizaa mtoto mmoja sasa ananishawishi nimuuoe nakusema kwamba yule hakuwa chaguo lake nakwamba ni matokeo ya shetani sasa nifanyeje wadau

Unataka kuoa MFU!

Kiapo cha ndoa ni hadi kifo kiwatenganishe. sasa huyu katenganishwa na mmewe, hii ina maanisha either yeye au huyo mumewe au wote wamekufa. Angalia huyo ni either mfu au mjane.

Mwombe Mungu akupe MKE sio mjane au mfu. Je shetani anayemsingizia kesha kufa? muulizie may be kafa, vinginevyo bado ni rafiki yake na ndio maana alishindwa kuishi na huyo aliyekuwa mumewe kwa kumsikiliza sana shetwani wake.
 
Kwa hyo ww unamwona huyo mwanaume mwenzio aliemuacha ni mjinga wewe ndo mjanja unaetaka kumuoa? Mpk unaomba na ushauri? Inaonesha amekuaminisha kwamba jamaa ndo alikua ana matatizo maana inavyoonesha yeye ndo kamuacha jamaa kwa kusema hakuwa chaguo lake..mtu aliachika kwenye ndoa hua anamatatizo flan yataka moyo kuishi naye amin hvyo..usijikute romeo na huyo manzi ndo juliet wa kwa shakespear
 
Achana naye huyo kikaragosi... Wala hata usimsikilize. Kama alidanganywa na shetani, mwambie amfuate huyo huyo shetani ndo amuoe...
 
ilikuwa mwaka 2009 nikawa A-level msichana niliyekuwa nimempanda sana na kumwahidi kumwoa mara baada ya kumaliza shule yeye akiwa amehitimu kidato cha nne na kupata DVN 4 ya 26 tukiwa tumekubaliane aende chuo cha certificate akasome kwa ustawi wa maisha yetu ya baadae lkn kilichotokea ni kwamba yule binti aliingiwa na tamaa na kuamua kuolewa na mwanamme mwingine bila hata kunijulisha niliumia sana lkn nikasonga mbele baada ya miaka 3 yule dada kaachika kwa huyo bwanake na kaamua kwenda college na alizaa mtoto mmoja sasa ananishawishi nimuuoe nakusema kwamba yule hakuwa chaguo lake nakwamba ni matokeo ya shetani sasa nifanyeje wadau

Uamuzi mbovu utakaoufanya katika maisha yako ukimrudia..
 
Back
Top Bottom