Tanzania Sweetheart
Member
- Mar 17, 2020
- 46
- 63
MWANZO
Hebu jaribu kuwaza, upo ofisini kwako. Unapata taarifa kuwa mke wako kipenzi amepata ajali ya gari. Walioshuhudia wanakwambia watu watatu wamekufa hapo hapo na mke wako amepakiwa katika gari la hospitali akiwa mahututi huku nguo zake zimetapakaa damu.
Unaiacha ofisi na kutoka mbio ukiwa umerukwa na akili. Unapofika hospitali, mke wako ndio anakata roho kwenye wodi ya majeruhi.
Mwezi mmoja baada ya msiba wa mke wako unagutushwa usingizini saa tisa usiku na mtu aliyegonga mlango wa nyumba yako. Unapofungua mlango unamkuta mke wako aliyekufa mwezi mmoja uliopita akiwa amesimama mbele ya mlango akiwa na barua mkononi.
Ukimtazama hana tofauti na siku ile aliyokufa. Amevaa nguo zake zile zile zilizochanikachanika kutokana na ajali na mwili wake umetapakaa damu nyeusi iliyoganda!. Anakupa barua iliyokuwa mkononi mwake.
Unapoikunjua na kuisoma, imeandikwa.
“Bado wiki moja na wewe utakufa!”
Bila shaka utanishituka sana….
Sasa endelea.
Naitwa Hashim Mustafa. Kazi yangu ni ualimu. Umri wangu sasa unakaribia miaka arobaini na mitano. Nimeshafanya kazi ya ualimu katika shule mbalimbali za msingi za mkoa wa Tanga hadi kuteuliwa kuwa mwalimu mkuu.
Sikuteuliwa ualimu mkuu kwa rushwa, ukabila wala kujuana kama inavyotokea kwa baadhi ya walimu, bali niliteuliwa kutokana na uwezo wangu, elimu yangu na uzoevu wangu katika kazi za ualimu.
Baada ya kuwa mwalimu mkuu, shule nilizopewa zilikuwa zikifanya vizuri mwaka hadi mwaka na kunisababishia kupata sifa nyingi.
Binafsi nilipenda sana kufundisha shule za vijijini kwa sababu walimu wengi walikuwa hawazipendi kutokana na mazigira ya vijiji vyetu kutoridhisha kwa walimu.
Lakini mimi nilikuwa na sababu zangu za kupenda shule hizo. Kwanza ni kuwapa haki watoto wa vijijini na wao kupata elimu bora na si bora elimu. Pili mimi mwenyewe nilipenda sana kilimo na ufugaji. Nilikuwa mkulima mzuri na pia mfugaji. Nilipenda kufuga ng’ombe, mbuzi na kuku wa kienyeji.
Shughuli hizo za kilimo na ufugaji zilinipatia faida kubwa kutokana na kuuza mazao ninayopata kwenye kilimo na mifugo yangu.
Kabla ya kuwa mwalimu mkuu, tayari nilikuwa nimeshaoa mke ambaye nilizaa naye watoto watatu, wakike watupu. Wa kwanza nilimuita Wema, wa pili aliitwa Pili na wa tatu nilimuita Tatu.
Watoto hao walipokuwa wakubwa walikuwa wakinisaidia sana kazi za shambani kwangu baada ya muda wao wa masomo.
Wilaya nilizofanyia kazi ni Muheza, Korogwe na Handeni. Wakati nikiwa Handeni katika shule ya Msingi ya Chanika, binti yangu wa kwanza alipata mchumba. Alikuwa amemaliza kidato cha nne na kushindwa kufaulu kwenda kidato cha tano. Lakini mimi nilikataa kumuozesha mume. Nilitaka aendelee na masomo.
“Mwanangu soma kwanza halafu utakujaolewa” nilimwambia Wema ambaye alikuwa amekata tamaa baada ya kutofaulu kuendelea kidato cha tano.
Tulikubaliana na mwangu kuwa nitafute pesa ili nimpeleke chuo cha VETA kilichopo Tanga ili akasome masomo yoyote atakayopenda mwenyewe.
Miezi sita baadaye ndipo lilipotokea tukio ambalo sitalisahau hadi siku ya kufa kwangu. Mke wangu alikuwa anakwenda Korogwe kuwasalimia wazazi wake. Tulikubaliana kuwa angelala siku moja na siku ya pili yake angerudi.
Aliondoka saa moja asubuhi kwenda stendi, muda ambao na mimi niliondoka kwenda shule.
Nilifika shule dakika chache kabla ya saa moja na nusu. Kengele ya mstarini ikapigwa. Wanafunzi wakajipanga mistari chini ya mwembe. Tulifanya sala na paredi kidogo kisha niliwapa hutuba fupi wanafunzi kabla ya kuwaruhusu waingie madarasani.
Wakati nimeketi ofisini mwangu nikipanga kazi zangu nikapokea simu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu ambaye aliniambia basi alilopanda mke wangu lilikuwa limepata ajali.
Ilikuwa taarifa iliyonishitusha lakini sikuwa na sababu yoyote ya kuitilia shaka kwani licha ya kutokumfahamu mtu aliyenipigia simu hiyo, mimi mwenyewe nilikuwa maarufu. Nilikuwa nikifahamika na watu ambao mimi mwenyewe nilikuwa siwajui kutokana na kazi yangu ya ualimu.
“Ni basi gani lililopata ajali?” nikamuuliza mtu aliyenipigia.
“Ni basi la Mamujeez, lililokuwa linaenda Korogwe’
N kweli kuwa mke wangu aliniambia kuwa angepanda basi hilo linaloondoka saa moja na nusu asubuhi kwenda Korogwe.
“Limepata ajali sehemu gani?’
“Ni mwendo wa kilometa tatu tu kutoka hapa Handeni. Watu watatu wamekufa hapo hapo na wengine wengi wamejeruhiwa”
Nikashituka na kumuuliza “Waliokufa ni akina nani?’
“Sikuwatambua lakini nimemuona mke wako amejeruhiwa vibaya na amepakiwa kwenye gari la hospitali pamoja na majeruhi wengine”
Hapo hapo mkono wangu ulioshika simu ulianza kutetemeka kwa taharuki.
“Unasema amepelekwa hospitali?” nikamuuliza mtu wa upande wa pili kwa sauti iliyoonesha wazi kufadhaika.
“Basi acha niende nikamuone. Asante sana kwa kunijulisha”
Nikaitia simu mfukoni na kunyanyuka kwenye kiti. Nilimuita msaidizi wangu na kumjulisha kuwa nilikuwa ninatoka kwenda hospitali ya wilaya.
“Kuna nini mwalimu?”
“Kuna mtu amenipigia simu ameniambia kuwa basi la Mamujeez limepata ajali na mke wangu alikuwa amepanda hilo basi kwenda Korogwe”
“Kuna abiria waliojeruhiwa?”
“Nilivyoelezwa ni kwamba mke wangu ni miongoni mwa abiria waliojeruhiwa na kupelekwa hospitali. Nataka kwenda kumuona”
Baada ya kuondoka pale shule niliona kwenda mwendo wa kawaida ningechelewa kufika huko hospitali, ikanibidi nipige mbio. Watu walioniona walishangaa.
Nilikimbia hadi hospitali ya wilaya. Ulikuwa mwendo wa karibu kilometa mbili. Nilipofika nilikuwa ninahema na shati lote lilikuwa limeloa jasho.
Niliwauliza wauguzi kama kulikuwa na majeruhi wa basi la Mamujeez lililokuwa limepata ajali.
Muuguzi mmoja niliyekuwa ninamfahamu aliniuliza majeruhi niliyekuwa namuhitaji.
“Ni mke wangu. Nimeambiwa amejeruhiwa vibaya” nikamwambia.
“Anaitwa nani?’
“Mariam Mohamed”
“Nasikitika kukwambia kuwa Mariam amefariki dunia sasa hivi”
Nikashituka na kumkazia macho muuguzi huyo.
“Mke wangu amefariki dunia?”
Muuguzi huyo aliponiona nimetaharuki aliniambia. “Hebu twende ukathibitishe wewe mwenyewe, nisije nikakutajia mtu ambaye siye”
“Hebu twende”
Nikaenda na yule muuguzi hadi Mochwari. Tulipofika alinitolea mwili wa mwanamke aliyekuwa na mavazi yaliyoloa damu.
Nilipomtazama tu niligundua kuwa alikuwa mke wangu. Ingawa nilishaona maiti nyingi katika umri wangu lakini mshituko nilioupata kwa kuiona maiti ya mke wangu ulifanya nionekane sikuwa na uzoevu wa kuona maiti.
“Loh masikini mke wangu…umeiaga dunia…kumbe ile asubuhi ndio ulikuwa unaniaga….!” Maneno yalianza kunitoka kama niliyepagawa.
“Umemuona ndiye yeye?” muuguzi akaniuliza.
“Ndiye yeye jamani!. Hivi mmehakikisha kama amekufa kweli? Isijekuwa amezirai tu!” nikamwambia muuguzi.
“Hapana. Amekufa na amethibitishwa na daktari. Kama angekuwa amezirai tusingemuweka humu”
“Alhamdulilahi!” nikabaki kushukuru.
Tulitoka na yule muuguzi katika kile chumba. Nilikuwa nimetoa kitambaa cha mkononi nikajifuta jasho na machozi usoni mwangu.
“Mke wangu ndio umekufa kweli?” nikawa najisemea peke yangu.
“Mbele yake, nyuma yetu. Sote sisi ni njia hiyo hiyo” Muuguzi akaniambia lakini uso wake haukuonesha hata chembe ya huruma.
“Ni kweli lakini ametangulia ghafla bila kutazamia. Asubuhi tulikuwa pamoja….” Nilishindwa kuendelea kumueleza. Nikajifuta tena machozi yaliyokuwa yakinitiririka.
Zile kumbukumbu za kuagana na mke wangu asubuhi zilikuwa zikijirudia akilini mwangu kama sinema inayorudia tukio lililopita.
“Sasa uende ukawaarifu ndugu na jamaa, muje muuchukue mwili wa marehemu. Cheti cha kifo chake kitakuwa kimeshatayarishwa na daktari” muuguzi akaniambia.
Nikaondoka hapo hospitali na kurudi nyumbani. Niliwaarifu wanangu ambao walipopata taarifa ya kifo cha mama yao waliangua kilio. Nikawapigia simu ndugu, jamaaa, marafiki na watu mbalimbali wakiwemo walimu wenzangu.
ITAENDELEA
Sent using Jamii Forums mobile app