Aliniacha kwa fedheha, lakini leo anahitaji msaada wangu

Hadi kuja JF kuomba ushauri ni ishara tosha kwamba wewe ni farasi na dhaifu mno. Ushauri wangu mtatulie hiyo shida yake na wakati anagongwa na bwana ake ukamshikie miguu.
 
Achana naye; fanya maisha yako ikiwezekana mpige block. Acha udhaifu isipokuwa kama una nia ya kumrudia

lakin ukimrudia lazima atakuumiza tena
 
Hivi wadada kwanini hatuelewi...ukishazingua kwa mwanaume usirudi ng'oo

Komaa na misala yako
 
Mkuu Msaidie huyo Mdudu,hiyo ni fursa adhim ya kufanya Closure na yeye.Msaidie kisha mfungie ukurasa.Asikutafute mpaka kiyama.Yeye ndiye kapoteza,kwa nini umshikilie rohoni mwako mjinga mmoja tu huyo.
Mdudu?? C'mon

Ndo mnatuita hivo?
 
Jina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.

Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.

Nikaenda kujitambulisha kwa wazazi wake ndugu na jamaa zake, nikaanza kuweka mikakati ya kutaka kumuoa.

Mwaka jana binti akadai anataka kwenda kusoma (kuongeza elimu) nikakubali kwa shingo upande sana sana sana (maana ada sikuwa nalipa mimi, ni wazazi wake), nilikubali uku nikiwa naona penzi na mipango ya ndoa ndio inaingia mchanga (kwa waliopita vyuoni nadhani mnaelewa ofu iliyokuwa inanitawala),

Binti akafika chuo mwaka wa kwanza hapa hapa jijini DASILAMU mabadiliko yakaanza kwenye semieter ya kwanza katikati, kiburi kikaanza, binti hakawa tena hataki mawasiliano na mimi, nikaanza kupata wakati mgumu sana maumivu ya kichwa juu ya penzi ilo yakaanza, ikabidi niingie chimbo kuanza kuchunguza ili niwe na majibu ya uhakika.

Kumbe alishapata mtu mpya chuoni, binti nikawa simuambii kitu tena akanisikiliza, binti nikawa simpigii simu akapokea, simtumii sms ikajibiwa, siku ya tarehe 14/02/2021 aliniambi ivi "Wewe nini umesahau kwangu mbona ujiongezi, ebu sema kuna ulicho acha nikupatie ili usiwe unanitumia sms na kunitafuta kwa simu zako, naomba niseme ivi sikutaki ili uelewe kama umeshindwa kujiongeza na waambie wote wanaojua mahusiano yetu its over now na waambie ndugu zako wasinisumbue pia" nilibaki nimebungaa kama nimepigwa na shoti za umeme.

Nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.

Ilipita miezi kadhaa.

Napokea simu kutoka kwa M akidai anataka tuongee, nikamsikiliza ilikuwa ni simu ya kutaka kuniomba msamaa kwa kilicho tokea, anadai ata yeye haelewi nini kilimpata (nikaona izi ni soud tu za mabinti wa kileo) nikamuambia tu sawa nilisha kusamehe muda tu na nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako na mtu wako mpya..

Ni binti ambaye maumivu yake bado yanaishi kwenye kumbukumbu ya maisha yangu mpaka ivi sasa,

Nadahani mnaelewa dunia ya sasa bila connection mambo yanakuwa magumu sana, nashukuru mungu mimi naishi vizuri sana na watu tofauti tofauti kwenye sector nyingi nina watu ambao kama ikitokea changamoto falani naweza wafata wakanisaidia kwa uharaka zaidi, na uyo binti analielewa ilo kabisa ameshapata changamoto nyingi uko nyuma ila nilikuwa natumia connection za watu nilio nao kusolve kwa uharaka kabisa.

Sasa uyu binti kwa sasa anasumbuliwa na changamoto flani flani amabyo anadai kama isipokuwa solved kuendelea kwakwe kwa shule kutakuwa na changamoto kubwa sana, iyo changamoto yake kwangu haitachukua ata siku mbili kuisolve kama nikichukua jukumu ilo la kumsaidia,

Baada ya kupata changamoto iyo kwa sasa ndio amekuwa akinitafuta na kuniomba niwe msaada wake.... sijawai kujibu sms zake ambazo kila akituma lazima aniombe nimsaidie kwenye ilo tatizo, sijawai pokea simu zake maana najua ataanza tu kunielezea ilo tatizo na mimi sikutaka kushughulika na mambo yake kwa sasa maana yupo kwenye mahusiano mengine.

Je wangwana wana Jamiiforum wenzangu, watu wangu wa nguvu ambao tumeshawai kupitia changamoto za kuumizwa na walio tuumiza kesho wanataka msaada wetu mnashaurije kwenye ili maana bado nina kidonda moyoni

Note: nilikaa nae kwenye mahusiano miaka 4.

Karibuni kwa mawazo yenu wana JF.
alikuwa nini huyo inaonekana unampenda sana
 
Isafishe nafsi yako kwa kuachia msamaha na alama ya mtu aliyesamehe ni kuwatendea wema wale waliotukosea......

Wanadamu ni viumbe wenye kubadilika badilika ndio maana hata Mungu anatuasa kuwa tunakubaliana jambo basi kuwe na mashahidi kwa kuwa kiumbe mwanadamu ana kawaida ya kubadili maamuzi......

Kama yeye amekubadilikia ndivyo ambavyo pengine na wewe ungembadilikia.....

Kama umeamua kumsamehe na kuendelea na maisha mengine basi hupaswi kumuwekea kinyongo na kama jambo lipo ndani ya uwezo wako wewe msaidie kwani Mungu pekee ndiye anayelipa wema na sio mwanadamu........

Kukubali kumsaidia kutatoa tafsiri kuwa umesamehe na kumsahau na umeamua kuendelea na maisha yako bila ya yeye na uwepo wako mbele ya macho yako haukupi shida...

Kukataa kumsaidia kunakutafsiri kuwa bado una kinyongo na upo kwenye mateso makali baada ya kuvunjika kwa mahusiano yenu...........

Vaa uanaume, jitoe kwenye tope la visasi na chuki achia upendo na ubinadamu na hiyo ndio fimbo na funzo kwa watesi wako.......
una umri gani mzee?
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokupata.
Yaliwahi kunipata na mimi kwa mtindo huo huo.
Usije ingia mtego wa kusolve economic problems za huyo binti, maana tatizo likiisha atayeyuka tu kama barafu kwenye jua.

Narudia usijeingia mtego huo, wamekula wengine sasa wewe ndio wa kupangusa makali.
amletee ukauzu tu
 
Back
Top Bottom