Aliniacha kwa fedheha, lakini leo anahitaji msaada wangu

28October

JF-Expert Member
Aug 26, 2020
285
362
Jina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.

Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.

Nikaenda kujitambulisha kwa wazazi wake ndugu na jamaa zake, nikaanza kuweka mikakati ya kutaka kumuoa.

Mwaka jana binti akadai anataka kwenda kusoma (kuongeza elimu) nikakubali kwa shingo upande sana sana sana (maana ada sikuwa nalipa mimi, ni wazazi wake), nilikubali uku nikiwa naona penzi na mipango ya ndoa ndio inaingia mchanga (kwa waliopita vyuoni nadhani mnaelewa ofu iliyokuwa inanitawala),

Binti akafika chuo mwaka wa kwanza hapa hapa jijini DASILAMU mabadiliko yakaanza kwenye semieter ya kwanza katikati, kiburi kikaanza, binti hakawa tena hataki mawasiliano na mimi, nikaanza kupata wakati mgumu sana maumivu ya kichwa juu ya penzi ilo yakaanza, ikabidi niingie chimbo kuanza kuchunguza ili niwe na majibu ya uhakika.

Kumbe alishapata mtu mpya chuoni, binti nikawa simuambii kitu tena akanisikiliza, binti nikawa simpigii simu akapokea, simtumii sms ikajibiwa, siku ya tarehe 14/02/2021 aliniambi ivi "Wewe nini umesahau kwangu mbona ujiongezi, ebu sema kuna ulicho acha nikupatie ili usiwe unanitumia sms na kunitafuta kwa simu zako, naomba niseme ivi sikutaki ili uelewe kama umeshindwa kujiongeza na waambie wote wanaojua mahusiano yetu its over now na waambie ndugu zako wasinisumbue pia" nilibaki nimebungaa kama nimepigwa na shoti za umeme.

Nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.

Ilipita miezi kadhaa.

Napokea simu kutoka kwa M akidai anataka tuongee, nikamsikiliza ilikuwa ni simu ya kutaka kuniomba msamaa kwa kilicho tokea, anadai ata yeye haelewi nini kilimpata (nikaona izi ni soud tu za mabinti wa kileo) nikamuambia tu sawa nilisha kusamehe muda tu na nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako na mtu wako mpya..

Ni binti ambaye maumivu yake bado yanaishi kwenye kumbukumbu ya maisha yangu mpaka ivi sasa,

Nadahani mnaelewa dunia ya sasa bila connection mambo yanakuwa magumu sana, nashukuru mungu mimi naishi vizuri sana na watu tofauti tofauti kwenye sector nyingi nina watu ambao kama ikitokea changamoto falani naweza wafata wakanisaidia kwa uharaka zaidi, na uyo binti analielewa ilo kabisa ameshapata changamoto nyingi uko nyuma ila nilikuwa natumia connection za watu nilio nao kusolve kwa uharaka kabisa.

Sasa uyu binti kwa sasa anasumbuliwa na changamoto flani flani amabyo anadai kama isipokuwa solved kuendelea kwakwe kwa shule kutakuwa na changamoto kubwa sana, iyo changamoto yake kwangu haitachukua ata siku mbili kuisolve kama nikichukua jukumu ilo la kumsaidia,

Baada ya kupata changamoto iyo kwa sasa ndio amekuwa akinitafuta na kuniomba niwe msaada wake.... sijawai kujibu sms zake ambazo kila akituma lazima aniombe nimsaidie kwenye ilo tatizo, sijawai pokea simu zake maana najua ataanza tu kunielezea ilo tatizo na mimi sikutaka kushughulika na mambo yake kwa sasa maana yupo kwenye mahusiano mengine.

Je wangwana wana Jamiiforum wenzangu, watu wangu wa nguvu ambao tumeshawai kupitia changamoto za kuumizwa na walio tuumiza kesho wanataka msaada wetu mnashaurije kwenye ili maana bado nina kidonda moyoni

Note: nilikaa nae kwenye mahusiano miaka 4.

Karibuni kwa mawazo yenu wana JF.
 
Kwahiyo anakukumbuka katika shida tu? Zikisha tatulika mambo yakiwa sawa anarudia matapishi. Hawa viumbe bana, sasa kama alileta dharau kabla akijua wazi wewe una msaada mkubwa kwanini alifanya vile?

Lakini kama umewiwa kumsaidia kibinadamu tu fanya ila siyo urudishe habari za kusameheana msaidie kumfanikishia Jambo lake kisha songa mbele.
 
Kwahiyo anakukumbuka katika shida tu? Zikisha tatulika mambo yakiwa sawa anarudia matapishi. Hawa viumbe bana, sasa kama alileta dharau kabla akijua wazi wewe una msaada mkubwa kwanini alifanya vile? Lakini kama umewiwa kumsaidia kibinadamu tu fanya ila siyo urudishe habari za kusameheana msaidie kumfanikishia Jambo lake kisha songa mbele..
Noted.
 
Mwambie amwambie huyo aliyenaye amsaidie.
Pia mwambie na wewe umeshapata mwenzako hivyo akuache uwe huru.
Mwisho endapo bado anakusumbua,tafadhali nipe namba yake nimsaidie atakacho.!
 
Back
Top Bottom