Alikuwa binadamu kweli?

Alikuwa binadamu kweli?

Hili kwangu rahisi sana, ila nilisema mpaka utupe wewe ushahidi na ukiri ya kuwa wewe ni Muongo.

Kisha nakuja kukuthibitishia ya kuwa Majini wapo.

Haya for the sake of Argument maana naona tunazunguka palepale.

Mimi ni lirongo na sina Ushahidi wa majini.
Haya wewe weka ushahidi wa majinni
 
Historia inaanza hivi...

Kipindi nkiwa bado shule secondari miaka kumi sasa imepita, nilinunuliwa simu na bro wangu. Siku moja ghafla mida ya mchana iliingia SMS kutoka kwa namba ngeni ikisomeka "ukitoka hostel nijulishe uniazime kitabu chako" sikumbuki sawa sawa but nimeotea tu kwa kumbukumbu.

Nikaanza kuchat nae kitabu gani na wewe nani. Ndipo mbele akagundua amekosea number na kuomba radhi kwamba alikuwa anamtumia mdada mmoja classmate wake namba zinafanana baadae tukaanza kufahamiana kwa kuendelea kuchat.

Alijitambulisha anaitwa Jimmson Henry, anasoma chuo kikuu mlimani (UDSM). Yuko mwaka wa pili bachelor degree ya information technology (IT). Anaishi hostel za mabibo lakini kwao Tabata.

His paternity origin is Ngazdja from Comoros islands, and Lindi mtwara kwa upande wa mama. He was so talkative,cheerful,funny na utani mwingi!

Tuliendelea na mazoea ya kuwasiliana, alinieleza mengi kuhusu maisha yake nami yangu pia.

Mwisho sababu ya ujana akaanza kuniomba nafasi nami nikampaa bila hata kumuona.

Mazoea yaliendelea ikafika muda nipo likizo akaomba tufahamiane kwetu tunapoishi, alianza yeye nikamleta kwetu hadI bi mkubwa alimuona.

Ikafika zamu yangu nikaunga "tuisheni" kwao maeneo ya Tabata liwiti.

Nilivyofika kwao aliweza kunitambulisha kwa mdogo wake wa kiume hawapishani sana kiumri anaitwa James. Tuliongea mengi na kuna mzee jirani pia alikuwa ni seremala naye akamuuliza huyu nani akanitambulisha rafiki yake.

Baada ya kuondoka tukaanza kuwasiliana ananiambia we ni mzuri sana hadi huyu mzee hapa jirani ananitania yule mrembo umemtoa wapi, kakangu pia!

Few months later akamaliza mwaka wa pili na kuwa likizo na mimi nkiwa natarajia kuingia mitihani yangu ya final.

Akanijuza kapata mwaliko America kutoka kwa rafiki zake wawili na taratibu zote za visa, tickect kafanya kwa gharama za wenyeji wake akafanikiwa kwenda. Alikaa kwa miezi mwili tunawasiliana kwa njia ya email nkiwa na mdogo wake.

Akirudi na tukaanza kuwasiliana as usually.

Kufupisha kuna kipindi alikua anapitia majukumu magumu ya kifamilia kama mtoto wa kwanza kwao, akawa anakosa hata muda nami. Nami nikawa frustrated na mambo yangu tukakorofishana na kupotezeana.

Baada ya mwaka mmoja nikiwa chuo sikuweza kuhimili alikuwa amenikaa sana kichwani hadI napata msongo wa mawazo.

Nikajiambia kwao napakumbuka nijaribu kwenda. Nilipanga weekend asubuhi nikaifikia nyumba nikiwa nimekaa mbali kidogo nione kama atatokea mtu.

Masaa yalipita nikahisi hawapo japo mlango upo wazi. Akatokea mdada mrefu mweupe nikajua atakuwa member mojawapo wa familia.

Nilisogea na kumsalimia akanijibu nikaanza kumuulizia jamaa wakaanza kushangaa hawamjui. Nilitaka details zote hadI wadogo zake na Dada zake hawamjui.

kuulizia ile nyumba wale wadada wanadai wao wameishi pale tangu udogoni na mtaa mzima wanawajua. Haijawahi kuishi familia nyingine hata kupangisha.

nikawauliza kama kuliwahi kuwa na mzee seremala upande wa nyumba anaranda mbao wanajibu hakujawahi kuwa na fundi seremala hapo.

Na nikiangalia like eneo naona tupu hakuna dalili yoyote hata mzee kuacha mabenchi ya mbao.

Kuna maduka around nikawa nawauliza wanadai hawajahi kuishi na mtu wa aina hiyo, hawamjui
Lakini nyumba ni ile ile hadI ndani kuko vile vile. Mpaka sasa sipati jibu.

Maana alishare nami vitu vingi mno mpaka harusi ya mdogo wake ilifanyika kwenye nyumba hiyohiyo.

Safari zake zote mamake ahata akiwa anaumwa na2julishwa nimpe pole mkwe. Plans zake zote.

Mfano alivorudi kutoka America alipewa zawadi ya gari akaghairi sababu hana uwezo wa kuhudumia, akaomba badala yake atumiwe vifaa vya office tufungue stationary kubwa Kijitonyama.

Alikua so bright kiasi anapata nafasi za kazi kwenye biashara na makampuni za maprofessor wake. Kila kitu ndani ya ofisi anashare nami.

Mpaka sasa ananiwinda kichwani kama mzimu na hapo kwao ndo hivi kama nilivyopakuta sijapata majibu hadI sasa.

Alikuwa nani?
Ngoja, ni pale junction ya Liwiti baada ya uwanja kushoto? Then unaenda hadi kwenye junction yenye maduka Mengi?
 
Haya for the sake of Argument maana naona tunazunguka palepale.

Mimi ni lirongo na sina Ushahidi wa majini.
Haya wewe weka ushahidi wa majinni
Hujakiri bado unaleta uhuni. Sababu nipo hapa kwa ajili ya kuonyesha ujinga wenu ulipo.

Naanzia hapa.

Ushahidi wa kwanza ni katika qur'aan soma surat "al Jinn".
 
Hujakiri bado unaleta uhuni. Sababu nipo hapa kwa ajili ya kuonyesha ujinga wenu ulipo.

Naanzia hapa.

Ushahidi wa kwanza ni katika qur'aan soma surat "al Jinn".
Sasa hapo itabidi kwanza niiamini hiyo Quran.Jambo ambalo mtu mwenye akili hawezi fanya.

Ni sawa niseme kuna Jogoo mkubwa mwenye uwezo wa kubeba mtu..ukaniomba ushahidi mimi nakuambia kasome kitabu cha darasa la tatu cha Pazi na jogoo wa ajabu
images%20(1).jpg
haya leta mwingine...huo umefeli
 
Sasa wewe unasema Nyerere wa leo, kijana mbona hata kutoa mifano hujui ? Hata mimi Nyerere nimemuona.

Weia mfano wa mtu wako unaye muamini wa miaka na mikaka iliyopita kisha mimi nikuwekee marejeo ya kihistoria juu ya mtume Muhammad, tena kwa chain mpaka kufika kwake, jambo ambalo elimu hii hakuna walio pewa ila sisi, nasema tena hakuna walio pewa ila sisi.

Usinifosi kuweka mfano unaotaka.
Nyerere leo hii hayupo hata kama kafa jana bado ni mtu ambaye leo hayupo kwahyo uwepo wake ni swala linalodai ushahidi...

Haya weka sasa hayo marejeo kwa Chain mpaka Muhammad na ushahidi wake sitaki maneno matupu. Anza na Source ya kwanza kabisa ambayo unaamini iliandikwa kipindi Chake
 
Ngoja, ni pale junction ya Liwiti baada ya uwanja kushoto? Then unaenda hadi kwenye junction yenye maduka Mengi?
Upande wa shule..unafata ile barabara ya vumbi inakatiza mbele ya jumla moja kubwa zuri kina fence. kama unashuka bondeni hivi.
 
What jamani am trying to help you, wewe si umesema umekiss tu dont worry hajakuchukua kiroho kwa kiss tu, halafu mimi nakusaidia kiroho ni mchungaji mimi, nipe namba PM, mimi sitakupoteza mtaa kama yeye bali nitakuonyesha kila kitu, nina maono i will help you upate ukweli
Nlitaka kuandika kisa.keyboard ikabadili
 
Sasa wewe unasema Nyerere wa leo, kijana mbona hata kutoa mifano hujui ? Hata mimi Nyerere nimemuona.

Weia mfano wa mtu wako unaye muamini wa miaka na mikaka iliyopita kisha mimi nikuwekee marejeo ya kihistoria juu ya mtume Muhammad, tena kwa chain mpaka kufika kwake, jambo ambalo elimu hii hakuna walio pewa ila sisi, nasema tena hakuna walio pewa ila sisi.
Samahani hivi wewe ni jini?
 
Hakua Binadamu, na Una bahati, na uache kumfikilia..,.... Ili hiyo Bahati kidogo uliyonayo isije kupotea, ukajuta kuzaliwa....... Mm ni Muhanga, kila ulichosema was the same Kwangu, but Mm nilijua baada ya kuwa nimeumia tayari.
Nakuomba dada angu kama usipojali share nasi kisa chako kwa kweli ni mambo ya kufikirisha sana
 
Usinifosi kuweka mfano unaotaka.
Nyerere leo hii hayupo hata kama kafa jana bado ni mtu ambaye leo hayupo kwahyo uwepo wake ni swala linalodai ushahidi...

Haya weka sasa hayo marejeo kwa Chain mpaka Muhammad na ushahidi wake sitaki maneno matupu. Anza na Source ya kwanza kabisa ambayo unaamini iliandikwa kipindi Chake
Kwanza rekebisha nilipokukosoa. Weka mfano muafaka, na ule ulio rejea. Nasubiri uwekke mfano stahiki.

Nakufosi uweke mfano stahiki.
 
Sasa hapo itabidi kwanza niiamini hiyo Quran.Jambo ambalo mtu mwenye akili hawezi fanya.

Ni sawa niseme kuna Jogoo mkubwa mwenye uwezo wa kubeba mtu..ukaniomba ushahidi mimi nakuambia kasome kitabu cha darasa la tatu cha Pazi na jogoo wa ajabuView attachment 1675043haya leta mwingine...huo umefeli
Kutokuiamini si hoja, hoja ni wewe kupinga kilichomo humo kwa hoja na ubainifu,huwa hatusemi tu ilimradi tunasema, bali ithibati ndiyo huuweka wazi ukweli.

Tukisema kila mtu aseme, watasema tu kama wewe unavyoamua kusema ila kizaazaa huja kama kile kilichokukuta ukashindwa kutupa ushahidi hata ule ulio ushuhudia ya kuwa uliona majini yakifugwa.

Kwahiyo bado hujavunja ithibati yangu, sababu umesema kwamba huamini ila hujakosoa kilichoandikwa mule na hili huwezi mpaka unazikwa.
 
Back
Top Bottom