Usiku kucha umelala ukiwaza uamke na uwongo gani ili na wewe uonekane umeanzisha thread
Hahaha! Nakupongeza kweli hii thread imekaa kizushi zaidi .
Usiku kucha umelala ukiwaza uamke na uwongo gani ili na wewe uonekane umeanzisha thread
Source: TBC
Kiwanda cha cementi kitajengwa eneo la MUSALE mkoani Mtwara. Kichocheo ni uwepo wa gesi ASILIA.
MANUFAA: kitaajiri watu 5,000, kitachochea maendeleo ya kusini n.k.
MWEKEZAJI: ni ALIKO DANGOTE yule tajiri wa NIGERIA na mmoja wa matajiri wakubwa AFRICA.
WAKANDARASI: Kiwanda kitajengwa na WAASIA!
SIFA: Kitakuwa kiwanda kikubwa kabisa AFRICA.
TETESI SERIKALINI/MTAANI/NDANI YA CHAMA: Kuna tetesi serikalini, Lumumba na mtaani kuwa kiwanda hiki kitakuwa na mkono wa CCM!..
SISIEMU itaambulia 10% (bila kuchangia fedha yoyote) - kwa kuwa mwekezaji mwenza kwa kutumia mikataba waliyoingia na DANGOTE kipindi cha uongozi wa MUKAMA ndani ya CCM..
Hali hii inachagizwa na ziara ya bwana DANGOTE hapa nchini kubebwa na CHAMA CHA MAPINDUZI.
Taarifa zaidi zinaonyesha. .Harakati zote hizi za kuanzisha makampuni ya biashara, kusaka nafasi za tenda na uwekezaji, ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao, ambao chama cha mapinduzi kinajiandaa kifedha kukabiliana na upinzani mkali utakaowalazimu kuingia gharama kubwa sana kuliko uchaguzi wowote uliowahi kufanyika TANZANIA.
My take: Natarajia kuona CCM ikicheza michezo michafu mingi kwa siri au wazi wazi ili ijihakikishie usalama 2015.
Natarajia kuona fedha nyingi zikiendelea kukusanywa na kutumika kuhujumu demokrasia kama hali inavyoendelea sasa.
Maneno haya uliyasema 17 April 2013 bado yako hai na sasa ukweli umeanza kudhihirika.Endapo hii nchi itakuja kuchukuliwa na upinzani kuna mambo mengi ya ajabu yatafichuliwa!! Tutaona vitu vingi sana!! Na hili wakilifikilia viongozi wa CCM wanatafuta kila njia kuhakikisha upinzani hautii mguu magogoni!!
Pole sana ndugu yangu Ben popote uliko Mola akupe wepesi wa madhila yanayokupata.Dangote ndiyo zake.Hata kule Nigeria anashirikiana na chama tawala cha PDP kufanya ufisadi
Aliwachangia mamilioni ya hela uchaguzi uliopita
Aliwahi kukumbwa na kashfa ya kuchakachua hisa alipokua mwenyekiti wa soko la Hisa Nigeria