[h=1]Aliko Dangote[/h] Rukia:
urambazaji,
tafuta
[TABLE="class: metadata plainlinks ambox ambox-style"]
[TR]
[TD="class: mbox-image"]

[/TD]
[TD="class: mbox-text"]This article
is an orphan, as few or no other articles link to it. Please
introduce links to this page from
related articles;
suggestions may be available.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: infobox, width: 20"]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"]Aliko Dangote[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Amezaliwa[/TH]
[TD]
10 Aprili 1957 (umri 56)
Kano, Nigeria[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Kazi yake[/TH]
[TD]
Chairman &
CEO,
Dangote Group[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Wazazi[/TH]
[TD]Alhaji Dangote[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH]Tovuti[/TH]
[TD]
dangote-group.com[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Aliko Dangote (aliyezaliwa
10 Aprili 1957) ni
mfanyabiashara nchini
Nigeria. Yeye ni mmiliki wa
Dangote Group, ambayo ina shughuli katika Nigeria na nchi nyingine kadhaa za
Afrika Magharibi. Msaidizi tajiri wa Rais wa kitambo,
Olusegun Obasanjo na chama tawala cha
People's Democratic Party (PDP), Dangote huendesha biashara ya bidhaa ya Nigeria kupitia kampuni yake na kujuana na wanasiasa. Akiwa na wastani wa thamani wa karibu dola bilioni 2.5, alihesabiwa na
Forbes kama mmoja wa watu wenye asili ya kiafrica tajiri kabisa, nyuma ya
Mohammed Al Amoudi (bilioni $ 9,0 ) na Oprah Winfrey (bilioni $ 2,7).[SUP]
[1][/SUP]

Dangote Group
[h=2]Wasifu wa Biashara[/h] Kundi la Dangote, awali biashara ndogo iliyoanzishwa mwaka 1977, sasa ni muungano wa makampuni mengi iliyo na thamani ya
naira trilioni mingi na iliyo na oparesheni nchini
Benin,
Ghana,
Nigeria na
Togo. Biashara za Dangote ni pamoja na usindikaji wa chakula, utengenezaji saruji na kusafirisha mizigo. Kundi la Dangote linatawala soko la sukari nchini Nigeria, kwani yeye ndiye msambazaji mkubwa zaidi wa sukari nchini katika makampuni ya
vinywaji laini, watengenezaji pombe na
watengenezaji peremende. Kundi la Dangote limekua kutoka kwa biashara kampuni ya biashara hadi kuwa kundi kubwa zaidi la Viwanda nchini Nigeria, pamoja na kiwanda cha kusafishia sukari cha Dangote (kampuni iliyo na pesa zaidi katika
Soko la Hisa la Nigeria, yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 3 na usawa wa Aliko Dangote umefika bilioni $ 2), kiwanda kikubwa zaidi barani Afrika cha kutengeneza simiti: Obajana Cement, Kiwanda cha Unga cha Dangote miongoni mwa mengine.
Dangote alijihusisha pakubwa katika kufadhili kampeni ya Obasanjo ya kuchaguliwa upya katika uchaguzi wa mwaka 2003, ambapo yeye alichangia zaidi ya milioni N200 (milioni $ 2). Alilichangia milioni N50 (milioni $ 0.5) Msikiti wa Taifa akitumia kukindi cha "Friends of Obasanjo na Atiku", na akachangia milioni N200 (milioni $ 2) kwa hifadhi la vitabu la Rais. Zawadi hizi zenye utata kwa wanachama wa chama tawala cha
People's Democratic Party zimechangia wasiwasi juu ya ufisadi licha kampeni za kupambana na rushwa zilizoongozwa na Obasanjo katika kipindi chake cha pili cha uongozi.[SUP][
onesha uthibitisho][/SUP]
[h=2]Marejeo[/h]