Alikiba sio star?

Alikiba sio star?

nyakandula

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
1,251
Reaction score
1,735
Leo nilikua uwanja wa tabata shule kuangalia mechi za ligi ya mchangani..ALIKIBA nae alikicheza namba 9 kiukwel mpira anajua kucheza ila nilichoshangaa watu wala hawamshangai kama tulivozoea kwa mastaa wakionekana katika sehem za kawaida yan watu hata kuomba nae picha hakuna dah ikanishangaza sana nikajiuliza angekuja diamond pale uwanjan sijui kama pangechezeka.sas nikajiuliza hivi huyu jamaa sio super star?sikupata majibu
20180314_164302.jpeg
 
Nina rafiki yangu anakaa Tabata aliniambia alimuona kiba akicheza shule ya msingi Tabata,sikumuamini ila wewe umethibitisha kwani hapo nyuma nakiona kituo cha polisi Tabata.Hapa ndio jamaa anapofeli kibiashara na kutokupata deal kubwa na makampuni makubwa huwezi ww mwenyewe kujichukulia poa alafu wakupe brand uibebe ww kama balozi na hapo nasikia ana bidhaa ataziingiza sokoni naona watu nao watazichukulia poa.Ila muacheni ndio maisha yake aliyoyachagua.
 
Mpaka unashangaa maana yake unakiri ni star. Ipo hivi, watu wanaokuona kila siku hawawezi kukushangaa.

Kusema kweli natamani siku ali kiba nimuone live ili nimshangae. Huenda ana jina ambalo halitendei haki
 
Jamaaa amepiga assist safi saaana.

Jamaaa alikusanya kijijini...!

Big up kiba. Maisha ndo hayahaya
 
Mbona Mjomba Mpoto anatembea pekupeku, we kucheza mpira na viatu ndio unaona hatari?
 
Au Dudu Baya mbona anakunywa gongo lakini bado ni star ? Kuwa star sio lazima unywe bia tu na kusahau whisky ya asili
 
Leo nilikua uwanja wa tabata shule kuangalia mechi za ligi ya mchangani..ALIKIBA nae alikicheza namba 9 kiukwel mpira anajua kucheza ila nilichoshangaa watu wala hawamshangai kama tulivozoea kwa mastaa wakionekana katika sehem za kawaida yan watu hata kuomba nae picha hakuna dah ikanishangaza sana nikajiuliza angekuja diamond pale uwanjan sijui kama pangechezeka.sas nikajiuliza hivi huyu jamaa sio super star?sikupata majibuView attachment 722540
Hii simu yako uliopigia hii picha lazima itakuwa tecno lile toleo la mabaamedi.
 
kiba keshazowea sana uswahilini ..mirungi anagonga tu sana apo vijiweni .. jama ni kama chidibenz wameshamzoweya pale ilala na kaliako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom