Aliemaliza degree 2018 yupo kitaa, mwenzake alierudia form 4 akiwa "25 years" kahitimu diploma mwaka jana 2024 ila tayari kapata ajira taasisi nzito

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Hawa ni wanafunzi naowajua vizuri walimaliza form 4 mwaka 2012

Moja alifaulu kwa division 1 ya point 16 (ya enzi hizo), akaenda A Level shule nzuri ya private akafaulu division 2 nzuri, chuo akamaliza 2019, hakuwa mvivu wa kusubiria kazi ijilete, ni mpambanaji, kajitolea sana na kuhudhuria interviews, ajira aliwahi kupata kampuni flani ya waarabu ila mazingira ya kazi yalimshinda akaacha, mwaka juzi alipata ajira nzuri shirika la NGO ila ilikuwa ya mkataba wa mwaka 1, maisha yalikuwa mazuri kwa kiasi chake, ajira ilipoisha akafungua duka lakini biashara ilimshinda akafunga, kwa sasa yupo kitaa lakini anajikusanya upya arudi

Mwenzake waliemaliza form 4 pamoja alifeli kabisa, division 4, mwaka 2021 alipiga pepa ya kurudia mtihani wa form 4 kama mtahiniwa binafsi, kwa muda huo alikuwa na miaka 25 au 26, Matokeo yakatoka hayakuwa mabaya akaenda Diploma aliyomaliza mwaka jana

Kuna ajira za Taasisi flani nzito zilitangazwa mwaka huu, siwezi kuiweka itamfichua kirahisi huko aliko,

Alienda kupiga interview, akaingia oral, akapita.

FUNDISHO

kuwahi kumaliza sio kuwahi kufika
kuwa na kikubwa zaidi haimaanishi mwenye kidogo hawezi pata.
ambae yupo kitaa sio mwisho wake, anaweza kufanikiwa siku yoyote, game bado haijaisha
 
Ukweli ni kwambs maishs ni bahati unaweza uka perform vzr darasani lakn mtaani ukawa na poor performance

Kwa hiyo respect ni kitu cha muhimu sana kweny maisha
 
Back
Top Bottom