Kwanza uache kujiita Sheikh!Sasa akamuombe mkewe kijana anakuja kuombaje mzee?
hahahahahahahahahhahahahahahhahahahah, we jamaa ni kwere hahahahahahhahaaDuh,kashapiga konde mkuu,kuoa mtu wa miaka 55 we unaona kazi ndogo
msamehe tuu huyo ni ndugu yako,usipomsamehe utakuwa huna tofauti naye,kumsamehe nayo ni adhabu,em imagine baada ya kumsaidia atakuangaliaje,atapata aibu iliyoje halafu wewe ndo unazuga huna hata moja.hapo lazima heshima irudi na umbea ataacha,lakini usisahau kuwa huyo ni ndugu yako no matter what,kukuletea zengwe hakumfanyi kuwa sio ndugu yako.Wadau nawasalimu,
Kuna mdogo wangu ambae wakati naoa aliendesha kampeni ya kunitangaza vibaya kuwa naoa mwanamke mzee, alizunguzuka kwa ndugu na jamaa akisema maneno hayo, ni kweli mke wangu amenizidi umri nina 34 yeye ana 55 hata hivyo tulipendana hivyo hivyo tukaamua kuoana, ndugu zangu wengi walipinga ndoa hiyo, upande wa mke wangu ndio ilikua balaa hasa watoto wa mke wangu walidai nimemuoa mama yao kwa sababu ya pesa lakini sikujali, tukafunga ndoa na tunaendelea kuishi kwa amani
Sasa, huyo mdogo wangu amejikuta yupo kwenye matatizo, nyumba anayoishi na familia yake inatakiwa kurudishswa kwa mmiliki wa awali baada ya mmiliki huyo kushinda kesi mahakamani dhidi ya mdogo wangu, ama alipe fidia kiasi cha million kumi na tano au aachie nyumba (kiwanja) ndani ya miezi sita awe amelipa pesa hizo, zimebaki wiki mbili ama Tatu ikamilike miezi sita na hajafanikiwa kupata pesa hizo, ni wazi kiwanja kinarudishwa kwa mshindi wa kesi
Hivyo amekuja kwangu kuniomba msaada wa hizo 15 million ili akomboe kiwanja chake, maana kwenye kesi wanamgombania kiwanja Ingawa yeye ndie amewahi kujenga hapo, hivyo panatakiwa kubomolewa kama atakosa pesa hizo, baada ya kunieleza tatizo hilo pia akamueleza mke wangu, mm kwa sasa hela zangu ziko kwenye mizunguko ila mke wangu yeye anazo na yupo tayari kumsaidia kama mm nikikubali na kutoa go ahead, ila nimekataa kwa udhalilishaji alionionesha wakati naoa
Huyu bwana mdogo alinidhalilisha sana wakati naoa huyu mwanamke, nimeshangaa sana leo anakuja kuomba msaada kwa huyu huyu mwanamke aliedai ni mzee kwamba nabemendwa na kadhalika,
Sasa yeye ameoa binti mdogo wanaelingana rika sasa ampe hizo pesa, mm nilikua nna maana yangu kuoa huyu mama, nimeshahangaika na masista duu sana nawajua ukiyumba kidogo tu anakimbia, sasa ngoja tuone huyu wa kwake kama kama atastahimili hii tufani
Wadau mlikua mnasemaje au tumsaidie tu?
Sijui kama nimeeleweka vizuri, naomba niweke hiviMkuu najua dogo wako alikuudhi sana..ila kiuhalisia hatakama ni mimi ningepinga wewe kumwoa huyo mama mwenye miaka 55.. Sio tamaduni zetu kumwoa mwanamke anaelingana na mama zetu...kwa hiyo mm nafikiri dogo alikua na nia nzuri tu ila ilipingana na mtazamo wako..
Mimi nafikiri msaidie tu..undugu hauishi..bado ni ndugu yako tu..wewe msaidie tu..
Kumbuka....usimtukane mamba kabla ya kuvuka mto.
Ingekua vice versa bado ungeshangaa?Ohh my... Pole. Nimeishia hapo nliposoma miaka.
Yeye ndie alietukana mamba kabla hajavuka mtoto, hivyo huo msemo wa kioo unamfaa yy zaidiKumbe dogo alisema ukweli ambao huutaki kusikia sasa unajenga bifu, acha ujinga hakuna aijuae kesho so msaidie usijione maisha umeyapatia na usivunje kioo kwa kukuonesha tongotongo usoni mwako
Kumbe ulimuowa uyu mama sababu ulikuwa juu ya mawe[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] kumbe kweli umefata Pesa sio mapenzi asante kwa kuwa mkweliYeye ndie alietukana mamba kabla hajavuka mtoto, hivyo huo msemo wa kioo unamfaa yy zaidi
Maisha hayana formula, hapa mjini kila mtu akikwambia jinsi alivyo Pata pesa au jinsi alivyofanikiwa kimaisha unaweza kuzirai, wapo majambazi, madawa ya kulevya, wengine walidhalilika ili kufanikiwa, hivyo mm nina akili zangu timamu kuamua kuoa mama mtu mzima wa 55 lengo ni kuweka maisha sawa Ndo maana hata yy dogo hakwenda kuomba pesa kwa ndugu wengine kaja kwangu, nisingemuoa huyu mwanamke na maisha yangu yakawa kama zamani angekwenda kuomba wapi hiyo 15 million, maana zamani wote familia nzima tulikua juu ya mawe sasa angemuomba nani kama nisingeoa huyu mwanamke?
Wakubwa zako wanapofanya vitu flan wanafanya kiutu uzima na wanajua wanachokifanya usiwabeze,
Yeye na wote walionibeza wakati naoa huyu mwanamke ndio hao sasa hawakauki kwangu kuomba misaada, sasa huo tuiteje kama sio unafiki?
Mbona yeye dogo amemshika ugoni mkewe mara mbili na hajamwacha lakini mbona mm kaka yake nipo kimya sijawahi hata siku moja kumwambia amwache mkewe, you know why? Ni maamuzi yake it's non of my business
Sasa Kuna jambo kubwa kwenye maisha kama mkeo kulala na mtu. Mwingine? Lakini mm kwa kifua changu cha kiutu uzima nilikaa kimya na kumwachia amalize mwenyewe
Acha ajifunze maisha through the hard way
Swali la kizushi mfano ww ndo ungekuwa tajiri unaela alafu uyo mama Hana ela je ungekuwa????Sijui kama nimeeleweka vizuri, naomba niweke hivi
Mm sikwenda kumuomba ushauri wakati nataka kuoa, sababu kuoa ni uamuzi wangu binafsi, hata yeye hakuja kuniomba ushauri wakati anaoa
Hivyo alichokifanya yeye ni majungu, alitembea kila kaya katika ukoo akipika majungu na kunisema vibaya, tena kwa matangazo makubwa, ni ukosefu mkubwa wa adabu kwa kaka yako
Sasa leo kinachomleta leo kuomba msaada kwa huyu huyu mwanamke mzee ni kipi? Je morally inakubalika? Mtu uliedai mzee hafai leo akusaidie inakuja?
Mbona hoja hii mnaikwepa kila nikiisema hamjibu?
Ni sawa na kumuita ndugu yako jambazi na unamtangaza kote kuwa mali zake amepata kwa ujambazi, halaf kesho unapata tatizo unaenda kwa huyo jambazi kuomba msaada, Je upewe huo msaada kweli?
Nijibuni
Ulitaka niwatangazie watu kwamba nimefuata pesa?Kumbe ulimuowa uyu mama sababu ulikuwa juu ya mawe[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] kumbe kweli umefata Pesa sio mapenzi asante kwa kuwa mkweli