Alidai nimeoa bibi kizee, sasa anaomba msaada

sheikh yasin

Member
Aug 6, 2015
61
45
Wadau nawasalimu,

Kuna mdogo wangu ambae wakati naoa aliendesha kampeni ya kunitangaza vibaya kuwa naoa mwanamke mzee, alizunguzuka kwa ndugu na jamaa akisema maneno hayo, ni kweli mke wangu amenizidi umri nina 34 yeye ana 55 hata hivyo tulipendana hivyo hivyo tukaamua kuoana, ndugu zangu wengi walipinga ndoa hiyo, upande wa mke wangu ndio ilikua balaa hasa watoto wa mke wangu walidai nimemuoa mama yao kwa sababu ya pesa lakini sikujali, tukafunga ndoa na tunaendelea kuishi kwa amani

Sasa, huyo mdogo wangu amejikuta yupo kwenye matatizo, nyumba anayoishi na familia yake inatakiwa kurudishswa kwa mmiliki wa awali baada ya mmiliki huyo kushinda kesi mahakamani dhidi ya mdogo wangu, ama alipe fidia kiasi cha million kumi na tano au aachie nyumba (kiwanja) ndani ya miezi sita awe amelipa pesa hizo, zimebaki wiki mbili ama Tatu ikamilike miezi sita na hajafanikiwa kupata pesa hizo, ni wazi kiwanja kinarudishwa kwa mshindi wa kesi

Hivyo amekuja kwangu kuniomba msaada wa hizo 15 million ili akomboe kiwanja chake, maana kwenye kesi wanamgombania kiwanja Ingawa yeye ndie amewahi kujenga hapo, hivyo panatakiwa kubomolewa kama atakosa pesa hizo, baada ya kunieleza tatizo hilo pia akamueleza mke wangu, mm kwa sasa hela zangu ziko kwenye mizunguko ila mke wangu yeye anazo na yupo tayari kumsaidia kama mm nikikubali na kutoa go ahead, ila nimekataa kwa udhalilishaji alionionesha wakati naoa

Huyu bwana mdogo alinidhalilisha sana wakati naoa huyu mwanamke, nimeshangaa sana leo anakuja kuomba msaada kwa huyu huyu mwanamke aliedai ni mzee kwamba nabemendwa na kadhalika,

Sasa yeye ameoa binti mdogo wanaelingana rika sasa ampe hizo pesa, mm nilikua nna maana yangu kuoa huyu mama, nimeshahangaika na masista duu sana nawajua ukiyumba kidogo tu anakimbia, sasa ngoja tuone huyu wa kwake kama kama atastahimili hii tufani

Wadau mlikua mnasemaje au tumsaidie tu?
 
Sikiliza fikra zako, wewe ndio unamjua mdogo wako vizuri.

Japo no matter what undugu haufi ukimsaidia itakuwa afadhali kwako baadae usipomsaidia utakuwa mzigo wako baadae, sidhani kama utaweza kuvumilia kuona ndugu yako anateseka
 
Wadau nawasalimu,

Kuna mdogo wangu ambae wakati naoa aliendesha kampeni ya kunitangaza vibaya kuwa naoa mwanamke mzee, alizunguzuka kwa ndugu na jamaa akisema maneno hayo, ni kweli mke wangu amenizidi umri nina 34 yeye ana 55 hata hivyo tulipendana hivyo hivyo tukaamua kuoana, ndugu zangu wengi walipinga ndoa hiyo, upande wa mke wangu ndio ilikua balaa hasa watoto wa mke wangu walidai nimemuoa mama yao kwa sababu ya pesa lakini sikujali, tukafunga ndoa na tunaendelea kuishi kwa amani

Sasa, huyo mdogo wangu amejikuta yupo kwenye matatizo, nyumba anayoishi na familia yake inatakiwa kurudishswa kwa mmiliki wa awali baada ya mmiliki huyo kushinda kesi mahakamani dhidi ya mdogo wangu, ama alipe fidia kiasi cha million kumi na tano au aachie nyumba (kiwanja) ndani ya miezi sita awe amelipa pesa hizo, zimebaki wiki mbili ama Tatu ikamilike miezi sita na hajafanikiwa kupata pesa hizo, ni wazi kiwanja kinarudishwa kwa mshindi wa kesi

Hivyo amekuja kwangu kuniomba msaada wa hizo 15 million ili akomboe kiwanja chake, maana kwenye kesi wanamgombania kiwanja Ingawa yeye ndie amewahi kujenga hapo, hivyo panatakiwa kubomolewa kama atakosa pesa hizo, baada ya kunieleza tatizo hilo pia akamueleza mke wangu, mm kwa sasa hela zangu ziko kwenye mizunguko ila mke wangu yeye anazo na yupo tayari kumsaidia kama mm nikikubali na kutoa go ahead, ila nimekataa kwa udhalilishaji alionionesha wakati naoa

Huyu bwana mdogo alinidhalilisha sana wakati naoa huyu mwanamke, nimeshangaa sana leo anakuja kuomba msaada kwa huyu huyu mwanamke aliedai ni mzee kwamba nabemendwa na kadhalika,

Sasa yeye ameoa binti mdogo wanaelingana rika sasa ampe hizo pesa, mm nilikua nna maana yangu kuoa huyu mama, nimeshahangaika na masista duu sana nawajua ukiyumba kidogo tu anakimbia, sasa ngoja tuone huyu wa kwake kama kama atastahimili hii tufani

Wadau mlikua mnasemaje au tumsaidie tu?
piga moyo konde ndugu
 
kweli kipenda roho hula nyama mbichi, walisema wahenga, lakini 34 mpaka 55 palefu (soma paleeefu) ni kama mama na mtoto wake. mama akiwa amemzaa mtoto wake akiwa na miaka 21!!
Hivi kibaiolojia, mke wa huyu bwana katika umri huo anaweza kuzaa? just for curiosity
 
sheikh yasin mafunzo ya Mohamed hayafundishi ndugu kusameheana?
Yanafundisha kusameheana, hata hivyo dini mara nyingi ipo too lenient, ukiifuata dini all the time unaweza kukwama, wakati mwingine nature na common sense ndio vinatakiwa kutumika

Matatizo katika maisha humfanya mtu akomae, wacha apate hili tatizo ajifunze maisha through the hard way
 
Pole sana mkuu.

Samehe tu usonge mbele.

Msaidie halafu achana naye, hata wewe ukijichunguza vizuri kuna watu unawawazia mabaya sana na wao hawajui na wala sio wabaya kiviile, sema tu hujapata nafasi ya kuwafungukia kama jamaa alivyokufungukia.

Huo ndio ubinadamu wenyewe.
 
Mwenye pesa zake anataka kumsaidia..We tatizo lako nn..Kwani mkeo alikuwa hajui kama mdogo wako anafanya kampeni ili msioane..Mbona yeye kakunjua moyo na anataka kumsaidia
Ndio maana amesita kumpa msaada hadi amekuja kuniuliza mimi maana yeye mwenyewe anakumbuka vizuri kampeni iliyofanywa na bwana mdogo dhidi ya ndoa hii
 
kweli kipenda roho hula nyama mbichi, walisema wahenga, lakini 34 mpaka 55 palefu (soma paleeefu) ni kama mama na mtoto wake. mama akiwa amemzaa mtoto wake akiwa na miaka 21!!
Hivi kibaiolojia, mke wa huyu bwana katika umri huo anaweza kuzaa? just for curiosity
Kwani tatizo ni nini hasa? Mbona safi tu, napata mapenzi mazito mno kuzidi hata hao waliooa rika moja, maisha hayana formula, tusikariri
 
Daaah... Shekhe naona ulienda kuhemea tu hapo, yaani unaona mtu umri wa mama yako??

Khatare sana wewe, hata hukujisikia kama vile uko na mama mzazi?
 
Kaka shikilia msimamo hapo hapo maana baade atakuja kujua kuwa mke wako ndio kazitoa hizo hela ndio atakudhalilisha zaidi.
Mwambie mke hapa huyu hapewi kitu...anadhani masista duu ndio dili...wale wakugegeda tuu sio wakujiaminisha kwao na maisha
 
Back
Top Bottom