Alidai nimeoa bibi kizee, sasa anaomba msaada

Mkuu msaidie tu mwezi Wa toba huu mpate thawabu Na pia ajue kuwa kaka Yake ukukosea kuoa maana amekuja kupata msada toka kwako alafu akija kukushukuru ndio umweleze ukweli lazima atakuomba msamaha
 
Tukiludi ki uhalisia ni kweli umeoa ajuza..ila inapokuja shida usifikirie kulipiza kisasi kama uwezekano wa kumsaidia upo msaidie ndungu yako
 
Kwani tatizo ni nini hasa? Mbona safi tu, napata mapenzi mazito mno kuzidi hata hao waliooa rika moja, maisha hayana formula, tusikariri
Hakuna kukariri hapo,hapo umempendea pesa huyo mzee ndomana huna sauti unasema ndugu yako akamuombe huyo mkeo,anaanzaje na wakati wewe ndugu.yake upo?
 
lazima huyo mwanamke ni mzungu au ana helani kweli umeoa mzee kwa nini tufiche
 
Kwai Sara alizaa akiwa na umri wa miaka mingapi?
 
Jamani mke anakuzidi miaka 21? You must be psychologically lacking something!
 

Kama hayo yote unapata,hata mm nakuunga mkono.Kamua vitu vzr baba achana na kelele za watu
 
mpatie huo mpunga,andikishianeni,chukua nyaraka za nyumba zote,mwekee time frame ya kurejesha hzo fedha,deadline ikifika na hujapata fedha zako nyumba yako,msaidie kwa namna hiyo ili baadae asije kukugeuka
 
Duu umeoa bibi yako?

Njaa hizi zitatuua vijana.
 
Fuata roho yako.
Fanya maamzi binafsi kama jinsi ulivyodhamilia kumuoa huyo mkeo.

Wakati mwingine yapasa tuudhihirishie umma ya kwamba malipo ni hapa hapa duniani.
 
Dah... Ni kweli ulimuoa kwa sababu anamshiko? Nauliza tu [emoji4]
 
Kwai Sara alizaa akiwa na umri wa miaka mingapi?
Mkuu ugesoma vizuri swali langu ungenielewa. nimeuliza kuwa "kibailogia huyo mwamamke anaweza kuzaa? kwa taarifa yako Sara hakuzaa kwa sababu alikuwa na sifa za kibailojia na ndiyo maana katika Biblia sara mwenyewe alishangaa kuambia atazaa
Mwanzo 18:11-13 inasema "Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?
Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee"
Lakini kama ni kwa ahadi Mungu kama ile aliyoitoa kwa Sara hapo sina swali na sifa hapo zitakuwa za kiroho zaidi kuliko za kibailojia.
 
utakuwa umeoa ....wa serkal iliopita nn. teh
 
menopause ishafika. hawez zaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…