Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,778
Ngozi ni binti wa miaka 22 akiwa mwanafunzi wa chuo mwaka wa pili akisomea shahada ya usawi wa jamii. Ngozi amejaliwa ana weusi wa kiafrika na figure number nane, ukichanganya na kujipenda kwake, ni binti mrembo sana. Katika familia yao Ngozi ni binti wa kwanza kufika chuo kikuu kwahiyo mashangazi na mama wadogo wote wanafuraha kuelezea maendeleo ya Ngozi.
Likizo moja ya chuo ambayo ilikua takriban miezi miwili, mama mdogo wa Arusha alimualika Ngozi aende kwake akapumzike. Mama mdogo ameolewa na mfanya biashara, kama unavyojua machalii wote ni mamilionea!! Kwakifupi mama mdogo maisha super. Tena kwa kutokutaka binti yake asipate tabu, mama mdogo alituma ticket ya ndege kutoka DSM.
Wiki ya kwanza Ngozi kukaa Arusha alikuwa exited kwanza kumuona mama mdogo ambae hawajaonana muda mrefu, pili alikuwa haijui Arusha kabisa. Mama mdogo anakigrocery kwahiyo asubuhi walikuwa wanatoka wote na kurudi jioni. Baada ya wiki mbili ile ratiba ilimchosha Ngozi, ingawa alijitahidi sana kutoonyesha lakini wenyeji wake walimstukia. Mama mdogo alivunjikwa moyo, basi mume wake akamuambia hawa vijana ni wakuwatoa jioni sehemu za starehe.
Uncle alimuambia Ngozi ajiandae wanatoka, mama mdogo mitoko haiwezi kwanza mwenyewe anawatoto wadogo, kwahiyo akishafunga biashara yake anataka awe nyumbani na watoto wakilala na yeye apate kupmzika. Ngozi aliinjoy sana mtoko, na yeye ni mtu wa kinywaji, alipiga viwine vyake huko, walirudi usiku wa kama saa nane.
Alfajiri mmoja katika watoto wa mama mdogo akawa na temperature tena anatapika, mama mdogo ilibidi amwamshe mume wake wamuwahishe mtoto hospitali, wanafika kwenye gari mama mdogo anakuta kufuli la kike, mume wake alikataa kabisa kuwa hafahamu chochote kuhusu lile kufuli. Ngozi alipoulizwa amebaki kimya, ugeni wa Ngozi uliishia pale, na uhusiano na mama mdogo mpaka sasa hauna afya njema kibaya zaidi ni kuwa mama mzazi wa Ngozi anamtetea mwanae na mama mdogo amekuwa mtu mbaya sana.