Ali Mbarouk Mshimba mgombea wa CHADEMA Jimbo la Uzini Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ali Mbarouk Mshimba mgombea wa CHADEMA Jimbo la Uzini Zanzibar

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MAFILILI, Jan 22, 2012.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  SIKU chache baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC- CCM) kumteua mfanyabiashara, Mohammed Raza kuwania nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Jimbo la Uzini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejibu mapigo.

  Katika kuhakikisha kuwa kinalinyakua Jimbo hilo, Chadema imemteua Ali Mbarouk Mshimba kuwa mgombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho kwa Jimbo hilo la Uzini.

  Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Mwandamizi wa Habari na Uenezi, Ofisi ya Makao Makuu ya Chadema, Zanzibar, Dadi Kombo Maalim ilisema uteuzi huo umefanywa na Kamati Kuu ya Chadema Taifa.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo ulifanywa katika mkutano wa kawaida uliofanyika Dar es Salaam jana chini ya Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara), Said Amour Arfi na Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa.

  Uamuzi huo ulipitishwa kwa kauli moja na Kamati Kuu ya chama Taifa baada ya kupokea
  taarifa ya mchakato wa uteuzi wa awali uliofanywa na ngazi husika za Chadema Jimbo la Uzini iliyowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Hamad Musa Yusuph.

  Katika taarifa hiyo Kamati Kuu ya Chama Taifa ilielezwa kwamba uchukuaji fomu za uteuzi wa ndani ya chama ulianza Disemba 15, mwaka jana na kuhitimishwa Januari 15 mwaka huu ambapo jumla ya wanachama watatu walichukua fomu za kugombea.

  Kura za maoni za uteuzi wa mgombea zilifanywa Januari 17, mwaka huu ambapo Ali Mbarouk Mshimba alikubaliwa kwa kura zote 126 za wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo, kati ya wajumbe 130 waliopaswa kuhudhuria kutoka katika shehia zote 13 za Jimbo la Uzini.

  Mapendekezo hayo ya Jimbo la Uzini ya kumteua Ali Mbarouk Mshimba yaliridhiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Kati kilichofanyika Januari 18, mwaka huu.\

  Source:gazeti la habari leo januari 22, 2012

  HONGERA CDM KWA KUDUMISHA MUUNGANO
   
 2. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu atakua mpinzani ama msindikizaji.? Watu wana ngoma yao bwanaaa, sio kila mtu anayejiskia kucheza aingie uwanjani tu!
   
 3. M

  Mkono JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ukirejea hali ilivyokuwa jimbo la Igunga kabla na baada ya uchaguzi mambo madogo kama haya hautasumbuka kuyachanganua.
   
 4. k

  kiche JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Naomba kauli hii pia uitoe na Arumeru mashariki!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  mungu wafumbue macho waznz
   
 6. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Mkuu FF,

  Una sababu za kuwa na ujasiri huu hasa kwa zanzibar kwamba itakuwa rahisi kwa CCM kushinda.Lakinu uwe na angalizo kwamba kwa sasa hakuna chama cha upinzani Zanzibar.Na itakuwa ni CDM kujipima nguvu visiwani.Siasa ni mchezo.Anything can happen ,let us wait
   
 7. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  So what?
   
 8. D

  DOMA JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Jamani tuwe makini asije kuwa shibuda mwingine
   
 9. L

  Liame Senior Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamaa wa Chadema si walisema humu JF hawana shida na Zanzibar leo tena wanameza maneno yao!
   
 11. j

  jigoku JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145

  Kwani Igunga mlishinda au CCM ilitangazwa?na ukitaka kujua kama CCM ilitangazwa huyo mbunge wenu ameshindwa kufanya kile mlichokizoea kukifanya wana magamba,matokeo yake alikimbilia Singida,Dodoma na Pugu(Dar)kuwashukuru wananchi kwa kumchagua,na hivi juzi juzi tu kama unafuatilia utakuwa unajua kilichompata huyo Mbunge wa NEC-bwana Kafumu,watu wanaendelea kumzomea,watu waligoma kuendelea kujadili ujio wa katiba mpya kama angeendelea kuwapo mahali pale,mwisho wa siku alisababisha mdahalo kuvunjika.sasa huwezi kutupatia reference ya uchaguzi wa Igunga kwa uchaguzi wa jimbo la Uzini,acha tusubiri mpambano.
   
 12. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  muandilie mumeo kitafunuo mwanamke unaangaka asubuhi mitandaoni
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Chadema wakishinda huko Zanzibar tatembea bila nguo kutoka Posta mpaka Kimara na kurudi.
   
 14. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  UTEUZI WA MGOMBEA JIMBO LA UZINI


  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua Ali Mbarouk Mshimba kuwa mgombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Uzini.

  Uteuzi huo umefanywa na Kamati Kuu ya chama taifa katika mkutano wake wa kawaida uliofanyika Dar es salaam tarehe 20 Januari 2012 chini ya uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) Said Amour Arfi (Mb) na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa.

  Maamuzi hayo yalipitishwa kwa kauli moja na kamati kuu ya chama taifa baada ya kupokea taarifa ya mchakato wa uteuzi wa awali uliofanywa na ngazi husika za CHADEMA Jimbo la Uzini iliyowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Hamad Musa Yusuph.

  Katika taarifa hiyo Kamati Kuu ya Chama Taifa ilielezwa kwamba uchukuaji fomu za uteuzi wa ndani ya chama ulianza tarehe 15 Disemba 2011 na kuhitimishwa tarehe 15 Januari 2012. Jumla ya wanachama watatu walichukua fomu za kugombea.

  Kura za maoni za uteuzi wa mgombea zilifanywa tarehe 17 Januari 2012, ambapo Ali Mbarouk Mshimba alikubaliwa kwa kura zote 126 za wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo, kati ya wajumbe 130 waliopaswa kuhudhuria kutoka katika shehia zote 13 za Jimbo la Uzini.

  Mapendekezo hayo ya jimbo la Uzini ya kumteua Ali Mbarouk Mshimba yaliridhiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Kati kilichofanyika tarehe 18 Januari 2012.

  Ali Mbarouk Mshimba alizaliwa tarehe 10 Aprili 1966 katika Kijiji cha Tunduni, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Zanzibar. Ali Mbarouk Mshimba ni Katibu wa CHADEMA wa Jimbo la Uzini na ni Mwalimu wa Skuli Msingi Mchangani Chamba.

  Ali Mbarouk Mshimba amesoma Shule ya Msingi Uzini mwaka 1977 mpaka 1984 na Shule ya Sekondari ya Fidel Castro mwaka 1984 mpaka 1987 na baadaye kusoma mafunzo ya ualimu ya miaka miwili katika ngazi na nyakati mbalimbali mwaka 2006 mpaka 2008 (Special Certificate in Teacher Education through Teachers Advancement Program) yaliyoratibiwa na Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Imetolewa tarehe 21 Januari 2011 na:

  Dadi Kombo Maalim
  Afisa Mwandamizi wa Habari na Uenezi
  Ofisi ya Makao Makuu Zanzibar
   
 15. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Hawana shida nayo kivipi? Wapi kamanda. Waweza kuonesha ili tuamini hayo maneno! Ili usije ukaonekana unaandika umbea
   
 16. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Watu watasubiri kwa hamu wakuone ulivyo mkuu au siyo. Waambie tu jamaa zenu waweke leveled playing ground, actually CHADEMA itaingia Zanzibar safari hii kwa nguvu sana, kwenda kuamusha siasa za upinzani ambazo zimeanza kufifia kama si kufa kabisa, katika kudai uwajibikaji wa serikali na watawala kwa wananchi.
   
 17. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Mkuu, eneo analotoka mtu, kabila au dini, has never been an issue, it is not issue, it won't be issue ndani ya CHADEMA anapotafutwa mtu mwajibikaji kwa ajili ya kutumikia watu, kwa maendeleo ya watu. Ni uwezo na wito, maana CHADEMA suala si vyeo, ni kupangiana majukumu, commitment, na dedication to the struggle huku spirit ya volunteerism ikipewa kipaumbele ndiyo msingi ulioifikisha CHADEMA hapo ilipo leo, si suala la vyeo, ukanda, wala anakotoka mtu, kama ambavyo unataka kuonesha hapa wewe MS.

  Unataka kuendelea kuwaaminisha watu wenye fikra kama zako dhidi ya CHADEMA kuwa wagombea waliowania nafasi mbalimbali katika chaguzi zilizopita na zinazoendelea nchini, walitoka Moshi na kugawanywa kwenye majimbo au kata, wilaya au mikoa? After all Mtanzania yeyote anaruhusiwa kuchagua na kuchaguliwa mahali popote na kwa nafasi yoyote, almuradi awe anakidhi vigezo vya kisheria, kanuni, taratibu na hasa katiba ya nchi, juu ya hicho anachotaka kugombea, kutimiza haki yake (na wajibu)
   
 18. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Where do u stand mkuu. What is ure true colour? Mbona unazungumza points zinazopingana katika suala moja. Utaonekana huna hoja, lakini unabisha tu for the sake ya kubisha kamanda. Jipange vyema au ndo blah blah za watu wa magamba.
   
 19. s

  saguge Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera chadema kwa kumpitisha mwl ally mbarouk mshimba bila fedha na wala kuchakachua kama magamba.chadema ndicho chama cha kada zote na kimbilio la masikini.jimbo la uzini ndio chimbuko la mapinduzi ya zanzibar na waliopinduliwa ni waarabu na mgombea wa ccm raza ni mwaarabu.ndani ya ccm ili uteuliwe ama uwe mfanyabiashara au uhonge sana au uwe mgeni au mtoto wa mafisadi.haya kazi kwenu kati ya mzawa na mwaarabu.
   
 20. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuwaachie wazanzibar wataamua maana niwakumbushe kuwa hata wagombea ni wazanzibar hivo tusiwasemee wazanzibar kwani wao wanamfaham mshimba na Raza kuliko sisi.
   
Loading...