Ali Mbarouk Mshimba mgombea wa CHADEMA Jimbo la Uzini Zanzibar

Ali Mbarouk Mshimba mgombea wa CHADEMA Jimbo la Uzini Zanzibar

Chadema wakichukuwa hilo jimbo naihama rasmi CCM. Hii challenge niliitowa hata Igunga.

sasa unamweleza nan hapa? Si utibu kwanza machusi yako hayo na sura yako kama wasira! BRAVO CHADEMA.
 
ni vizuri CDM kuweka mgombea huyu znz,kwani ni sehemu pia ya kujitangaza visiwani ambapo tutatumia u-ccm b wao kuwaambia wananchi umuhimu wa mgombea wetu!!!
 
Mikakati ya ushindi imekaaje?
Tume ya uchakachuzi (ccm D) mnawajua vema, lakini vipi wagombea wa ccm B (CUF) na ccm C (NCCR) ni akina nani?

Best wishes CDM maana kuishinda timu ya refa si kazi ndogo.
 
mushimba? ni wazi rufaa hapa nyeupe



Wewe Ms kumbe hata majina ya Wapemba wenzio hauyajui. Jina lake ni Mshimba na Siyo MUSHIMBA! Nakumbuka kufundishwa Maths pale mlimani na Professor fulani Mlimani aliyekuwa akiitwa Mshimba alikuwa faculty ya Science. Hata hivyo bado naamini jina lake siyo tatizo hata likiwa linafanana na majina ya bara maana watanzania wengi ni wabantu.
 
nafikiri ni fursa kwa cdm kujipambanua na kuonyesha uhai wa upinzani wa kweli visiwani kwa kupitia hilo jimbo,na cha msingi ni kujipanga vya kutosha tu
 
Kazi rahisi sana kwa Ali Mbarouk Mshimba. Tumia kauli mbiu, "CCM imewafikisheni hapo mlipo katika lindi la ufukara; na CUF ndio hao hao CCM 'B'. Chagueni chama mbadala!!!!!!"
 
Acha ubaguzi kwa majina yenye asili ya bara.mbona hawa hawakukatiwa rufaa?Juma "N'hunga"-Dole,Ibrahim "Sanya"-Mji Mkongwe,Masolwa Cosmas "Masolwa"-Bububu,Fatuma "Maghimbi"-chakechake na Mzee "Ngwali"-Mkwajuni


mushimba? ni wazi rufaa hapa nyeupe
 
Nilijuwa atakuja mtu ataongea kama wewe na ndio maana nikakumbusha Igunga niliyasema hayahaya. Si kwa kuwa magwanda hawawezi, la hasha, kwa hao "candidates" wanaowachaguwa. Hawana vigezo. Tanzania majimboni hakichaguliwi chama anachaguliwa mtu, na hilo tumeliona kwa Shibuda, Mrema na Kafulila.

Mkuu FF,
Nakubaliana na point yako kiasi,Lakini kwa sehemu kama Zanzibar,Vyama vya siasa bado vina sauti kubwa,Kuna sehemu kule pemba CUF inaweza kusimamisha jiwe na likashinda.Ishu ya kuwa na candidate mwenye mvuto ni ya muhimu sana especially kwa CDM ambayo inahitaji kuingia Zanzibar (Ku penetrate),hivyo suala la vigezo ni very key.
 
Mkuu FF,

Una sababu za kuwa na ujasiri huu hasa kwa zanzibar kwamba itakuwa rahisi kwa CCM kushinda.Lakinu uwe na angalizo kwamba kwa sasa hakuna chama cha upinzani Zanzibar.Na itakuwa ni CDM kujipima nguvu visiwani.Siasa ni mchezo.Anything can happen ,let us wait
Ikiwa ni hivyo basi hata hapo ulipodhani palikuwa na Chama cha upinzani Zanzibar jimbo hili lilibaki kwa CCM, sasa sioni tofauti yake!
 
Nilijuwa atakuja mtu ataongea kama wewe na ndio maana nikakumbusha Igunga niliyasema hayahaya. Si kwa kuwa magwanda hawawezi, la hasha, kwa hao "candidates" wanaowachaguwa. Hawana vigezo. Tanzania majimboni hakichaguliwi chama anachaguliwa mtu, na hilo tumeliona kwa Shibuda, Mrema na Kafulila.

Faiza uko sahihi Kabisa! Hili jina limekuwa likiring akilini mwangu tangu nilipolisikia kumbe huyu Bwana namuelewa sana sana kwani ni mchezo mmoja, shule moja (Wana CHADEMA humu huita Madrasa) na nahisi pengine nae anataka kujitowa kimaisha tu. Sioni kama ni mwanasiasa hasa na nikimuangalia na yule wa Magamba nahisi labda watu wa uzini wawe na kisasi na CCM ndio CDM washinde. Hata hivyo kama CUF walikuwa wakishindwa kila siku jimboni humo sifikiri kuwa watu wake wana kisasi hivyo na CCM kiasi cha CDM kushinda!
 
Chadema wakichukuwa hilo jimbo naihama rasmi CCM. Hii challenge niliitowa hata Igunga.[/QUO

Dada Foxy nafahamu jeuri unayojivunia ya uchakachaji matokeo kama inavyojionyesha katika makabrasha ya tume ya uchaguzi vinginevyo ningelikuomba usiwe mvivu wa kupambanua mambo ya siasa kwa kina na ukajionea jinsi gani mliowadanganya jana leo hawadanganyiki tena.....how proud r u my sis kuwaona watanzania wenzio wakitaabika sababu ya magamba? tazama insecurity ilivyoongezeka miaongoni mwa watanzani, or coz wewe ni wa upande uuuuuuuuuuuuuuuuule that u don't bother kabisa Tanganyika yetu......thnk big na toa fikra mgando my sisi..

Naona kama umesahau kuwa unazungumzia uchaguzi wa jimbo la Zanzibar ambalo CDM haina wala haijawa na Sera nayo. Jiangalie hata unavyochangia Ki uchadema, KiuTanganyika !
 
Watu watasubiri kwa hamu wakuone ulivyo mkuu au siyo. Waambie tu jamaa zenu waweke leveled playing ground, actually CHADEMA itaingia Zanzibar safari hii kwa nguvu sana, kwenda kuamusha siasa za upinzani ambazo zimeanza kufifia kama si kufa kabisa, katika kudai uwajibikaji wa serikali na watawala kwa wananchi.

Si unaona?! Sisi tuwanyonge yakhe, tena huwo ubabe mtakaotuletea kwetu tutauwezaje yakhe? Si mwajuwa sisi ni midebwedo? Leo mwataka debwedeko nasi na hiyo miguvu yenu? Hatuwawezi yakhe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu, eneo analotoka mtu, kabila au dini, has never been an issue, it is not issue, it won't be issue ndani ya CHADEMA anapotafutwa mtu mwajibikaji kwa ajili ya kutumikia watu, kwa maendeleo ya watu. Ni uwezo na wito, maana CHADEMA suala si vyeo, ni kupangiana majukumu, commitment, na dedication to the struggle huku spirit ya volunteerism ikipewa kipaumbele ndiyo msingi ulioifikisha CHADEMA hapo ilipo leo, si suala la vyeo, ukanda, wala anakotoka mtu, kama ambavyo unataka kuonesha hapa wewe MS.

Unataka kuendelea kuwaaminisha watu wenye fikra kama zako dhidi ya CHADEMA kuwa wagombea waliowania nafasi mbalimbali katika chaguzi zilizopita na zinazoendelea nchini, walitoka Moshi na kugawanywa kwenye majimbo au kata, wilaya au mikoa? After all Mtanzania yeyote anaruhusiwa kuchagua na kuchaguliwa mahali popote na kwa nafasi yoyote, almuradi awe anakidhi vigezo vya kisheria, kanuni, taratibu na hasa katiba ya nchi, juu ya hicho anachotaka kugombea, kutimiza haki yake (na wajibu)

Eti mbona vitambulisho vyote huandikwa mwahala ali[pozaliwa mtu. Si Tanzania tu bali pote ulimwenguni!
 
Kazi rahisi sana kwa Ali Mbarouk Mshimba. Tumia kauli mbiu, "CCM imewafikisheni hapo mlipo katika lindi la ufukara; na CUF ndio hao hao CCM 'B'. Chagueni chama mbadala!!!!!!"

Ule ni upande wa pili na kwa bahati mbaya hujuwi chochote juu ya upande huo. Ni ushauri tu ....Angalia mchezo tu angalau hiyo ruzuku wanayopata CHADEMA nayo itumike huu upande, basi si jengine lolote!
 
Back
Top Bottom