Nani kakuambia hapa tunatafuta Mshindi?
Ujue kuna tatizo moja dogo sana, watu hawajawahi fika Rwanda, nchi ambayo hata Rais wake kuna wakati huwa anajiendesha mwenyewe kwa gari lake.
Hii ina maana kwamba Rwanda bado haijawa nchi ya amani kihivyo, kwa hiyo karibu kila mgeni anayeweza kuvuta idadi ya watu hulindwa hivyo.
Hebu watembee kwanza waone sio kuja kujitia aibu tu hapa. Karibu kila msanii akienda kule hulindwa na Jeshi kwa kuhofu anaweza kupata madhara kutokana na ujio wake kuwa na idadi kubwa ya watu ama kujulikana na wengi.
Kuhusu hiyo show ya Uyu N'umwaka iliyofanyika Amahoro, sijui kuna tatizo la uelewa au watu wamepotoshwa au mimi sijaelewa, ila nachojua lilikuwa ni tamasha.
Kwa bahati naijua maana ya tamasha (concert), ni kama ilivyo kwa Fiesta au usiku wa Matumaini, mi nadhani haiwi ya msanii mmoja, ila huwa na msanii mkuu.
Kila mwisho wa mwishoni mwa mwaka Amahoro hufanyika tamasha kubwa kama lile na kuhusisha wasanii wa ndani kadhaa na wa nje wachache.
2012 mwishoni nilikuwa Rwanda kikazi, wasanii wageni walikuwa P Square na hata Rais Kagame alikuwa mmoja wa waliohudhuria. Kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambayo haijawahi tokea mpaka sasa.
Nadhani tutafundishana polepole hapa hadi tutaweza ongea lugha moja. Hili ni jukwaa kubwa sana.
Ova