Algerian airline loses contact with plane carrying 110 passengers

Algerian airline loses contact with plane carrying 110 passengers

KUN

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2011
Posts
383
Reaction score
80

Ndege ya Algeria yapoteza mawasiliano




​
140724102424_air_algerie_512x288_arsiv.jpg


​

24 Julai, 2014 - Saa 11:40 GMT

Shirika la ndege la Taifa la Algeria, limesema limepoteza mawasiliano na moja kati ya ndege zake iliyokua ikitoka Burkinafaso kwenda Algiers kupita sahara.

Mawasiliano yalipotea dakika 50 baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji wa Ouagadougou, shirika hilo limeeleza.

Ndege namba AH 5017 ilikua na abiria 110 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo.

Chanzo cha habari kimeliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa Ndege hiyo haikua mbali na mpaka wa Algeria wafanyakazi wa ndege hiyo walipoambiwa wabadili uelekeo kwa kuwa mawasiliano yalikua hafifu na kuepuka hatari ya kugongana na ndege nyingine katika njia ya Algiers-Bamako.
Mawasiliano yalipotea baada ya kubadilishwa kwa njia.

Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.




CHANZO: BBC Swahili


UPDATE


Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali.

Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.

Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.

„Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"


Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo.
"Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"


Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo.

"Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"


Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko
"Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana."
Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema.



140724105202_bangla_algeria_304x171_bbc_nocredit.jpg

​


CHANZO:
BBC Swahili
25 Julai, 2014 - Saa 02:42 GMT
 
Jamani. .

Tunaomba ipatikane,yasiwe Yale ya Malaysia.
 
Taarifa kutoka CNN ni kwamba ndege ya Algeria, Air Algeria yenye abiria 116 inayotokea Barkina Faso kuelekea Algiers, mji mkuu wa Algeria imepoteza mawasiliano na radar.

Tuombe Mungu iwe salama.
 
daah, inatisha. Tumuombe mungu ifike na kutua salama huko inakoelekea
 
Hali inazidi kuwa mbaya.
Hivi ni kitu gani sasa hiki?
 
Duuuuuh balaa!!! Kwenye kitabu cha Ufunuo pameandikwa nyakati za mwisho nzige wa chuma watawaangamiza wanadamu kuliko awali. Nzige wa chuma ni vyombo vya moto!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
OMG. Hope kule hakuna Russian supported rebels and missiles.
 
Ndege iliyokuwa imebeba jumla ya abiria 116 (110 wasafiri na 6 wafanyakazi) imepotea katika rada huko Afrika Magharibi wakati ikitoka Ouagadougou (Bukinafaso) kwenda Alger (Algeria) .Imepotea katika mazingira ya kutatanisha dakika 50 baada ya kuondoka.
Ndege hiyo yenye namba za usajili AH5017 inayomilikiwa na kampuni binafsi la Kihispania chini ya mamlaka ya Air Alger .Iliondoka Bukina faso saa 1:17 na ilitakiwa kutua Alger mnamo 5:10 a.m , lakini cha kushangaza mpaka muda wa kuwasili kutimia ndege hiyo ilikuwa haijawasili na haijulikani mahala ilipo mpaka sasa, imefatiliwa pia katika njia yake ila haijapatikana , ingawa kuna wasi wasi kama iliweza dunguliwa Mali ingawa bado hawana uhakika.
Ila mpaka sasa bado ni utata juu ya mahala ilipo.
Mkasa wake umenikumbusha ile ndege ya Malaysia. Stay tuned.

Source: SKYNEWS -breaking news.
 

Attachments

  • map-1-522x293.jpg
    map-1-522x293.jpg
    30.9 KB · Views: 242
BREAKING NEWS: Algerian airline 'loses contact' with plane carrying 110 passengers after it disappears off radar while flying from Burkina Faso to Algiers.
=============================================

Algeria's national airline says it has lost contact with a plane carrying 110 passengers and six crew after it disappeared off the radar on a flight from Burkina Faso to Algiers.

Air Algerie said air navigation services lost track of the flight around 50 minutes after take-off.


The plane, which is owned by Spanish private company Swiftair, was last picked up on radar at 1.55am GMT, the official Algerian news agency said.

The flight should have landed in the Algerian capital at 5am GMT.

article-2704018-1FEEEF7600000578-795_634x423.jpg


Vanished: Algeria's national airline says it has lost contact with a plane (believed to be an Airbus A320 like the one above) carrying 110 passengers and six crew members after it disappeared off the radar



Conflicting reports said the aircraft was an airbus A320 or a McDonnell Douglas MD-83.
The flight path of AH5017 from Ouagadougou, the capital of the west African nation of Burkina Faso, to Algiers was not immediately clear.


A source from Air Algerie told the AFP news agency said contact was lost while it was still in Malian air space approaching the border with Algeria.



The source said: 'The plane was not far from the Algerian frontier when the crew was asked to make a detour because of poor visibility and to prevent the risk of collision with another aircraft on the Algiers-Bamako route.


'Contact was lost after the change of course.'


The airline announced that the plane had gone missing in a brief statement carried by national news agency APS.


It added that the company initiated an 'emergency plan' in the search for flight AH5017, which flies the four-hour passenger route four times a week.
Ougadougou is in a nearly straight line south of Algiers, passing over Mali where unrest continues in the north.

article-2704018-1FEF1F6300000578-285_634x474.jpg


Fateful path: Contact was lost with flight AH 5017 while it was still in Malian air space approaching the border with Algeria after taking off from Ouagadougou, the capital of the west African nation of Burkina Faso




One of Algeria's worst air disasters occurred in February this year, when a C-130 military aircraft carrying 78 people crashed in the mountainous northeast, killing more than 70 people.


Tamanrasset in the deep south was the site of the country's worst ever civilian air disaster, in March 2003.


In that accident, all but one of 103 people on board were killed when an Air Algerie passenger plane crashed on takeoff after one of its engines caught fire.
The sole survivor, a young Algerian soldier, was critically injured.
The incident comes a week after Malaysia Airlines flight MH17 was shot down by a surface-to-air missile over Ukraine, killing all 298 people on board.



Concerns were first raised about the plane when it disappeared from radar screens while passing over the city of Donetsk last Thursday.


The plane was travelling at 33,000 feet on a pre-determined flight path when it suddenly vanished from trackers, immediately notifying air traffic controllers of the prospect that the plane had either crashed or made an emergency landing.
Flight radars generally monitor moving objects only, so if an aircraft disappears from the screens it either means the plane has become stationary or there has been a fault with the tracking system.


Tragically in the case of MH17 the former was true - but it wasn't until body parts and plane wreckage were spotted scattered over an eight square-mile area in eastern Ukraine that a crash could be officially confirmed.

In the case of the missing Malaysia Airlines flight MH370, the latter was the true, where it is believed the radar transponder system was deliberately turned off by someone on board


That plane is believed to have crashed in the Indian Ocean, killing all 239 people on board, but the wreckage has never been found and the cause of the disaster is unknown.

Source:dailymail
 
Ni kweli nimesikia hata mimi NDEGE ya shirika la ndege la Algeria imetoweka kutoka mitambo ya rada dakika 50 baada ya kupaa kutoka Burkina Faso ikielekea Algiers.
 
Back
Top Bottom