Tofautisha Askofu mkuu na askofu wa kawaida.Huyo Niwemugizi ni mtu mdogo sana kuna maaskofu kibao ila maskofu wakuu ni viongozi wakuu wa nchi wa dini zao.
Pengo ni kama raisi wa wakatoliki Tanzania na Malasusa ni kama raisi wa walutheri wa tanzania.Hawa wanajua kuwa katika waumini wao wamo CCM na UKAWA na watu wa kutoka vyama vyote na wasio na vyama,wanasiasa na wasio wanasiasa.Hivyo hawa wakuu huwa makini sana kutoa matamko yanayoegemea makundi.Huwa hawajishughulishi sana na mambo ya siasa na makundi ya kisiasa tofauti na hao maskofu wa maeneo kama akina Niwemugizi au wale wa makanisa ya mifukoni mwao ambao document zote za kanisa ziko mifukoni mwao kama akina kakobe n.k
Stability ya makanisa kwao ni muhimu kuliko siasa hizi za mpito za mara leo UKAWA,kesho maandamano n.k
. Huyo Kadinal Pengo hana Impact yoyote ndani ya kanisa na Anaingia kwenye vikao vya Baraza la Maaskofu kama mjumbe wa kawaida wala haongozi vikao vyovyote ndani ya Baraza isipokuwa anaongozwa na hao kina Ngalalekumtwa na Naibu wake Niwemugizi Huyo Pengo ni Mteule tu wa Papa
tunaomba sana tuwekee msimamo wake hapa manake tumefatilia na tunajua yupo wkenye bunge la katiba tunataka msimamo wake ili tuanze kuchukua hatua
Tofautisha Askofu mkuu na askofu wa kawaida.Huyo Niwemugizi ni mtu mdogo sana kuna maaskofu kibao ila maskofu wakuu ni viongozi wakuu wa nchi wa dini zao.
Pengo ni kama raisi wa wakatoliki Tanzania na Malasusa ni kama raisi wa walutheri wa tanzania.Hawa wanajua kuwa katika waumini wao wamo CCM na UKAWA na watu wa kutoka vyama vyote na wasio na vyama,wanasiasa na wasio wanasiasa.Hivyo hawa wakuu huwa makini sana kutoa matamko yanayoegemea makundi.Huwa hawajishughulishi sana na mambo ya siasa na makundi ya kisiasa tofauti na hao maskofu wa maeneo kama akina Niwemugizi au wale wa makanisa ya mifukoni mwao ambao document zote za kanisa ziko mifukoni mwao kama akina kakobe n.k
Stability ya makanisa kwao ni muhimu kuliko siasa hizi za mpito za mara leo UKAWA,kesho maandamano n.k
Sikubaliani na wewe kwani wao kama viongozi wakuu wa dini wanapaswa waseme ule ukweli uliopo nchini kwa wakati husika. Kama serikali haiwajibiki ipasavyo lazima waseme. Wakifanya vizuri lasima wasifie. Ndio biblia inavyofundisha. Ukipindisha maneno kwa vile unataka kitu fulani cha upendeleo imekula kwako ndio sasa unaona waumini wanalalamika.
hivi huyu askofu ana msimamo gani hasa juu ya siasa za nchi yetu?nani alipendekeza huyu mtu awe askofu wetu?hivi anajua misimamo yetu au anajifanyia mambo yake anavyotaka na kujipendekeza kwake ccm?ni lini hasa tutaachana na hawa wanafiki?
Muombe Mungu akusamehe. Msimamo wa Malasuasa aliutoa maranyingi na pia kautoa pia katika waraka wa jukwaa la wakristo. Pia si mjumbe wa bunge la katiba. Nafikizi unamuongelea Mdegela wa Iringa ambaye alishawahi kutamka kuwa anaunga mkono serikali mbili. Hakuna Askofu wa KKKT aliyepo kwenye bunge la katiba. KKKT na madhehebu yooote yaliyo chini ya CCT wana mwakilishi mmoja tu na ni muumini wa kawaida. Katika wote waliopelekwa na CCT ni yeye pekee aliyeteuliwa. Japo Mtetemela alishawahi kuwa kiongozi wa CCT hayupo bungeni kwa mwavuli wa CCT.
Ni kweli huyu mlutheri mwenzetu hatoi maono yake kuhusu katiba ya nchi hiii na still wanaombea Taifa unapoombea Taifa lazima ulielekeze kukaa kwenye msimamo....!
rosemarie,
Mimi mwenyewe ni mlutheri, naipenda kanisa langu, ninampenda zaidi Mungu ninayemtumikia. Huyu askofu nadhani ana elements za ccm, au misaada ya Lowassa makanisani inawalemaza vichwa baadhi ya viongozi wetu, wapo kimya kwenye mambo muhimu yanayohusu taifa letu, hawaoni kwamba wanaoumizwa ni sisi watanzania ambao kimsingi ndiyo waumini wao.
Nina mashaka maaskofu wakuu wa makanisa na viongozi wa madhehebu wanawekwa na usalama wa taifa bila waumini kujua. Angalia Cardinali Pengo alivyo kimya. Japo viongozi wengine kwakweli wanatutetea, Severine Niwemugizi yupo vizuri sana
Ask.pengo na wenzake, wanajua nguvu kubwa ya Kanisa la Kakobe
(www.fgbfchurch.org)
Hujui kazi za viongozi wa dini kwa mujibu wa vitabu vya Mungu;na Kakobe unamsikia tu
Hivi huyu Askofu ana msimamo gani hasa juu ya siasa za nchi yetu?nani alipendekeza huyu mtu awe askofu wetu?hivi anajua misimamo yetu au anajifanyia mambo yake anavyotaka na kujipendekeza kwake ccm?ni lini hasa tutaachana na hawa wanafiki?
Ki ukweli Siasa na Dini ni sawa na mafuta na maji, haviwezi kuchanganyika pamoja. Viongozi wa dini tuwaongoze watu kuijua njia ya Mungu na tuwaache wanasiasa na propaganda zao. Mtumishi alieitwa kumtumikia Mungu kiukweli hajihusishi na siasa kwa kuwa ni mchezo mbovu. Ukijiingiza kwenye siasa lazima umkosee Mungu. Huwezi kuhubiri Siasa na dini kwa kinywa hicho hicho.Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mumpe Mungu