Alen Kijazi, Dkt Agness Kijazi na sasa Eng. John Kijazi, Dah!!

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,767
29,721
Wadau,

Leo hii Rais amemteua Bwana John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Mimi baada ya kusikia hili jina lake la mwisho la KIJAZI nikawakumbuka Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bwana Alen KIJAZI pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Bi. Agness KIJAZI.

Nimewaza kwamba hawa watatu ni ndugu au majina tu yanafanana? Na kama ni ndugu, inakuaje ndugu wote watatu wanakuwa na nafasi serikalini tena nafasi nyeti tu? Ni Juhudi zao binafsi mpaka wamefika hapo, au kubebana au coincidence tu?

Kuna yeyote anewajua hawa watatu kiundani?

Karibuni
 
Kwa hiyo hata kama ni ndugu, kama walipiga umande kisawasawa, wakafanya kwa uaminifu, wasichaguliwe kwenye nafasi ambazo wala hazishabihiani?? Katibu Mkuu Kiongozi, na TANAPA na Hali ya hewa wapi na wapi??

Halaf huyu aliyechaguliwa leo, je angelikuwa yeye ndio kaanza kuteuliwa ndipo hao wengine wakajateuliwa hapa pangelitosha??

Let's not discuss people, let's discuss matters. Huyo Maropeee atawajibika kutokana na hili liskandaliii???
 
Kama wapo vizur upstairs na ni waadilifu basi wacha wapige kazi, na naamini hakuna upendeleo hapo kwani wazee wao walikuwa na mahusiano ya karibu na watawala wetu wa awamu zote?
 
Back
Top Bottom