Kijazi: Msidanganywe, Maini na Mafuta ya Tembo sio dawa ya Kansa ya ini wala Kansa ya Uzazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Salaam Wakuu,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Allan Kijazi amawaeleza Wahariri na Waandishi wa habari Wandamizi zaidi ya 50 waliokutana Dodoma leo tarehe 10 Dec 2020 kwamba, kuna ujangiri mpya wa tembo umeibuka upya.

Kijazi amesema kwamba Majangili Wamebuni mbinu mpya ya kuhakikisha Tembo wanauliwa. Wanawadanganya Wananchi kuwa Mafuta ya Tembo na maini ya Tembo ni dawa ya kansa ya ini, kansa ya kizazi na Vidonda vya tumbo. Matokeo yake Wananchi wanaweka sumu kwenye Maboga na kuwatega Tembo kwa Misumari ili wapate maini na mafuta ya tembo.

Matokeo yake Wanaishi kuuza meno ya trmbo kwani mafuta na maini ya Tembo hayana soko lolote bali ni mbinu ya Majangili kuhakikisha wanapata meno ya Tembo. Kijazi kasema hadi sasa hakuna Utafiti wa Kisayansi unaonesha kwamba Mafuta na Maini ya Tembo ni dawa ya kansa.

Pia Kijazi kagusia tabia ya Watu kuwinda Wanyama wakidai ni Kitoweo, lakini matokeo yake Wanageuza Hifadhi kama sehemu ya biashara kwa kuuza nyama nje ya mipaka ya nchi.

Kijazi Katoa onyo kwa Majangili wote na kuwatahadharisha waache vitendo hivyo.

Vilevile ameelezea Tuzo tatu za Kimataifa ambazo TANAPA imepata ambazo ni tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Uwanja wa ndege wa Msembe na tuzo ya Viwango bora vya uhifadhi.

GEE_0498.JPG
GEE_0504.JPG



======

HOTUBA YA DKT ALLAN KIJAZI, KAMISHNA WA UHIFADHI WA TANAPA NA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA TANAPA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, DODOMA TAREHE 10/12/2020

NDUGU MENEJIMENTI YA TANAPA,

WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI,

WANAHABARI WAANDAMIZI WA HABARI ZA UHIFADHI NA UTALII NCHINI,

WANAHABARI DODOMA,

WAGENI WAALIKWA,


Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kuwepo salama Dodoma leo.

Ndugu Wahariri na Wanahabari Waandamizi,

Shirika la Hifadhi za Taifa tumekuwa na utamaduni wa kukutana na Wanahabari wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini kila mwaka kwa nia ya kuhabarishana na kuhamasishana kuhusu umuhimu na mchango wa vyombo vya Habari kwenye kufanikisha malengo ya Shirika

Napenda kukiri kwamba mikutano yetu nanyi imetusaidia kwa kiwango kikubwa kulitambulisha Shirika pamoja na majukumu yake kwa jamii. Ninaamini kwamba vyombo vya Habari vimetoa mchango mkubwa kwenye kufanikisha uwanja wa ndege wa Ruaha kuchaguliwa kuwa wa kwanza Afrika na wa pili duniani kuwa uwanja wenye mandhari nzuri kuliko viwanja vingine vyote Afrika na Duniani. Hifadhi ya Serengeti kuchaguliwa kuwa Hifadhi bora kuliko zote Afrika, na TANAPA kupata tuzo ya dhahabu ya ubora wa utoaji huduma kati ya mashirika 51 yaliyochaguliwa kutoka nchi 39 duniani na taasisi inayoitwa European Society for Quality Research (Taasisi ya Ulaya ya Utafiti wa ubora wa viwango).

Napenda kukiri kwamba, Kalamu zenu magazetini, vipindi vyenu katika redio na televisheni mara zote zimeongeza chachu ya utendaji kwetu katika kazi hasa pale mlipotupongeza na kutukosoa kwa nia chanya kabisa.

Napenda kukiri kwa kiwango kikubwa mmekuwa sehemu ya mafanikio ya TANAPA kutokana na weledi mkubwa katika kazi zenu.

Ndugu Wahariri na Wanahabari Waandamizi,

Leo tunakutana Dodoma ikiwa ni muendelezo wa Mikutano yetu ya kila Mwaka ya kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa Majukumu yetu Pamoja na Mipango yetu ijayo.

Kipekee kabisa, hasa baada ya zoezi la Uchaguzi Mkuu, Hotuba ya Mheshimiwa Rais, John Pombe Magufuli, ya kuzindua Bunge la 12 na Ilani ya CCM 2025 zimebainisha wazi Malengo na Matarajio yake katika Sekta ya Utalii, Sisi TANAPA tumeipitia hotuba na Ilani ya Chama Tawala 2020 – 2025 na tunaamini kwamba kupitia kikao hiki tuweke bayana Mipango na Mikakati hiyo ili Umma wa Watanzania uweze kufahamu.

Ndugu wahariri na Wanahabari waandamizi,

Katika mkutano wetu wa siku mbili mtapata fursa ya kusikia kutoka kwetu Mawasilisho yafuatayo:-

1. Mikakati ya TANAPA kuhusu Utekelezaji wa ILANI YA CHAMA TAWALA

2. Jinsi tulivyojipanga kuboresha utalii, hasa baada ya janga la homa ya mapafu – COVID - 19

3. Uhifadhi na Ushirikishwaji Jamii kwa nia ya kushiriki kwenye kuboresha hali zao za Maisha.

4. Utekelezaji wa mradi wa usimamizi wa maliasili na uendelezaji utalii kusini mwa Tanzani

5. Umuhimu wa Mfumo wa Kijeshi katika shughuli za Uhifadhi

6. Uhifadhi wa Wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka.

Ni Imani yangu kwa niaba ya TANAPA kuwa mtakuwa Mabalozi wazuri wa TANAPA katika kutoa ushauri mzuri kwenye mada tajwa na kuihabarisha jamii juu ya Mipango na Mikakati yetu ya Kiuhifadhi na Kiutalii.

Pamoja na mada hizi nilizotaja, napenda kutoa taarifa kwamba Mikakati ya Kiserikali na kishirika iliyowekwa imesaidia sana kupunguza wimbi la ujangili nchini. Hata hivyo, kuna dalili za kuibuka wimbi jipya la ujangili wa tembo ambalo linahamasishwa na watu wachache wenye nia ya kuwahamasisha wananchi na kuwajengea Imani kwamba maini na mafuta ya tembo yanasaidia kuponya Kansa y aini, Kansa ya kizazi kwa akina mama na vidonda vya tumbo.

Kutokana na kuaminishwa huko, baadhi ya wananchi wameanza kutumia mbinu za kuweka sumu kwenye maboga, na misumari kwenye maeneo wanayopita ili kuweza kupata maini na mafuta. Lakini pia wanapowaua tembo hao, wanaofanya kampeni hizo wananunua memo ya tembo hao. Nitoe rai kwa wananchi kwamba hakuna Ushahidi wowote wa kitaalam unaoonyesha kwamba maini na mafuta ya tembo yanatibu magonjwa yaliyotajwa. Hizo ni mbinu zinazotumika kuwadanganya wananchi ili wawatumie kufanikisha biashara ya meno ya tembo. Natoa onyo kwamba hatutasita kumchukulia hatua mwananchi yoyote bila kujali uwezo wake au nafasi yake katika jamii.

Mwisho niwatakie kikao chema na niwaombee tuwe wasikivu kwa mada zitakazowasilishwa na kutoa michango stahiki.

Napenda sasa kutamka rasmi kuwa mkutano wa Mwaka wa Wahariri na Wanahabari Waandamizi umefunguliwa Rasmi.

Asanteni kwa kunisikiliza.
 
Mapolice wa wanyamapori ni balaa, ukikamatwa unawinda kwenye hifadhi wanakuchuna unyao wote then wanakuambia haya potea..
 
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi amesema kuwa kuna dalili za kuibuka wimbi jipya la ujangili wa tembo nchini ambapo linahamasishwa na watu wachache.

Kijazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Tanapa, amesema kuwa watu hao wamekuwa wakiwadang’anya wananchi kuwa mafuta na maini ya tembo yanatibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa ya ini, ya kizazi kwa wakinamama na vidonda vya tumbo.

Kutona na hali hiyo ametoa onyo kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wahusika bila kujali wadhifa wala nafasi aliyonayo huku akiwaasa wananchi kutokubali kutumiwa na watu kwenye biashara hiyo haramu.
 
Usiku wa kuamkia leo kijijini Robanda Serengeti , simba wameuwa na kula muzi watano, ndama wawili, na wengine wanne kupotelea porini baada ya kukimbizwa toka kwenye banda la mzee Mabenga.
Mhifadhi pamoja na kuambiwa hajafika hata kusema pole.
Wananchi watawaacha simba salama?
TANAPA kaeni vizuri na majirani.
 
Hapa ndipo inapokuja ile dhana ya kuendeleza Wananchi kwanza.

Ukiwa na taifa la Watu duni kwa hali, mali na elimu uwe tayari kukabiliana na matatizo mengi zikiwepo imani kama hizo.

Wenzetu huko mbele huwezi kusikia bado Mamlaka zinahangaika kuwakumbusha Wananchi wanawe mikono kabla ya kula au baada ya kutoka chooni.
 
Back
Top Bottom