Albert Mangwea (Special Thread)

Mwachen Ngwea apumzike...

Who told you kuwa ukifa dhambini unakwenda kupumzika?!!Mshara wa dhambi ni mauti tena ya milele motoni,
msijidanganye na lugha yenu ya kipuuzi ya R.I.P,hakuna mtu anakwenda kupumzika kama anafia dhambini,
mnataka kwenda sehemu nzuri baada ya kufa Mungu anasema muache dhambi mumpokee Yesu ili muende
hiyo sehemu nzuri hakuna namna nyingine ya kupumzika hata mngezikwa na dunia nzima
 
Labda kwanza lets find out what made him do/engage na hivyo vitu. Ila naamini mazuri yapo hata kama wewe hujayaona mkuu, kila mtu ana mapungufu yake jamani..na kazi ya kuhukumu sio yetu. simply speaking!!!!!

Hakuna suala la mtu kuhukumiwa hapa mtu amefia dhambini isemwe wazi mnaficha nini ,hii haiwasaidii waliobaki
na kuendelea kula madawa ya kulevya' Vitabu vya dini vimeweka wazi na hata ndani ya nafsi ya mtu anajua ulevi ni
dhambi ya kumpeleka mtu motoni baada ya kufa'
 
Vijana tumepoteza mwelekeo,na hatujui wapi tunaelekea.
Tunaambukizana maovu na hatukumbushani mema na mtu mwema hawezi kufundisha Mikasi na Mitungi na hafi kifo cha kishitani.
Mungu katupa akili we should not fall for enything
 
Nilikuwa wa kwanza kuhoji hili na nikaenda mbali zaidi nikahoji nguvu hii ingetumika kabla yawezekana angekuwa sehemu nyingine.
Kwa wanaobisha naomba kuuliza kifo chake kimesababishwa na nn?
 
Hakuna suala la mtu kuhukumiwa hapa mtu amefia dhambini isemwe wazi mnaficha nini ,hii haiwasaidii waliobaki
na kuendelea kula madawa ya kulevya' Vitabu vya dini vimeweka wazi na hata ndani ya nafsi ya mtu anajua ulevi ni
dhambi ya kumpeleka mtu motoni baada ya kufa'
Nakubaliana na wewe kabisa ila kumbuka wakati anakata roho pengine alitubu na kusamehewa who knows? hata dakika yako ya mwisho inaweza kukuokoa..cha msingi tukemee matumizi ya madawa ya kulevya but kusema mtu kafia dhambi siungi mkono. ni mawazo yangu lakini!
 
Yaani hata mateja yanasifiwa. Nyie bongo flavor acheni hizo. Kwani lazima ukiwa masnii uwe teja?
 
kuna watu umu wanajifanya Sir God,wanajua kuhukumu marehemu,ambaye ajafanya dhambi yoyote awe wa kwanza kuhukumu.tusimuingilie kazi mungu,kwanza siku ya mwisho wale mnaowategemea kwenda mbingun sababu ni maaskofu au wwachungaj amtowakuta,mtakuta watu msiowategemea ,mshindwe,mwachen marehemu apumzike kwa amani.RIP Albert Mangwea tutafata mazuri uliyoacha
 
Tatizo waafrika na hasa wabongo ni wanafki sana na hawabadiliki hata arudi MASIHA, ki ukweli wewe unayesema maiti ya mwenzio ichapwe bakora una ukamilifu gani? Nikweli wewe umejichunguza na ukaridhika kwamba uko kamili mbele za M ungu na jamii kwa ujumla? Si kweli hauko kamili. Sisi wakristo tunaamini dhambi zote ni sawa mbele za Mungu! Kutembea na mwanamke ambaye si mke wako na kula unga wote wenu ni moto tu! Kuiba kazini na kula unga zote ni dhambi! Uchoyo na kula unga ni the same! Acheni unafki waafika, Ndio ninyi mnaosemaga ooh' NGURUWE ni haramu mimi siri na huku uko baa na mke wa mtu! Acheni ushamba duniani tunapita tu na kila mtu anapambana kivyake na hizi changamoto zilizomo humu, huna sababu au uwezo aw kuwakosoa wengine kwa kufikiri dhambi zako ni nafuu kuliko za wengine, Badilikeni wantu weusi hamjachoka tu kuitwa nyani kwa mambo yenu ya kinafkinafki!!
 
Nakubaliana na wewe kabisa ila kumbuka wakati anakata roho pengine alitubu na kusamehewa who knows? hata dakika yako ya mwisho inaweza kukuokoa..cha msingi tukemee matumizi ya madawa ya kulevya but kusema mtu kafia dhambi siungi mkono. ni mawazo yangu lakini!

Ni kweli yawezekana kabisa kutubu dakika ya mwisho kabla ya kufa,lakini sio suala la kujifariji nalo kwani
ni ngumu mtu anayefia katika ulevi kukumbuka suala la toba
 
Inapendeza watanzania na hasa watangazaji na wanahabari wote kuwa wawazi ili kuelimisha na kunusuru wananchi pale inapotokea vifo vinavyotokana na kuendekeza mambo yanayoharibu jamaa bada ya kutoa sifa za uongo. Ili tuwe na jamii salama yatupasa tuache unafiki na badala yake kukemea na kubainisha madhara kwa mfano wa mtu huyo ambaye anajulikana na jamii moja kwa moja.

Imezoeleka jamii na vyombo husika vinapolimisha juu ya madhara ya madawa ya kulevya. Utumia mifano iliyombali na waelimishwaji. Inapendeza kuweka wazi kwa mtu kama huyu ambaye 80% ya jamii yetu inamfahamu na hatima yake imeshuhudiwa na jamii hiyo kuliko kuendekeza unafiki.
 
Watanzania sisi ni wanafiki alivyokuwa mzma watu kimya tu wanamwangalia kwan walikuwa hawajui kuwa anabugia lakn kifo chake sasa watu eeeh radio ndo usiseme hata nymbo zke ameuza baada ya kifo.tujifunze mzik bla dawa inawezekana
 
Ni kweli yawezekana kabisa kutubu dakika ya mwisho kabla ya kufa,lakini sio suala la kujifariji nalo kwani
ni ngumu mtu anayefia katika ulevi kukumbuka suala la toba
nimekusoma mkuu
 
Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti....., ndugu zangu wapendwa msidanyanywe....mtenda dhambi ni mtumwa wa dhambi...., Mi sielewi fun wa Ngweah wanasema sio Unga wala sio sumu, inakuwaje wote na m2 the p kuungua pamoja? what a coincidence! hebu tujue ukweli
 
kwani chanzo cha kifo chake ni nini?

chanzo cha kifo chake ni moyo kuacha kufanya kazi.
kwani chanzo cha kifo cha huyo baba wenu wa taifa ni kipi?si kilikuwa Mkanda wa Jeshi=Ngoma?(UKIMWI).
 
Hakuna aliye sema Ngwea ana dhambi tunasema alifia ktk matendo ya dhambi, kama alitubu hiyo ni yake yeye na Muumba, nawewekusema si-wa Afrika ni nyani ni zaidi ya dhambi (kufuru) kwani tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. je Mungu ni nyani? Ngonepi
 
Last edited by a moderator:
hujakosea,natumia madawa kweli,ila sio mliberali kama wewe.

Mi naamini ktk Biblia na ndiyo sababu si muongo, mnafiki, waongo, wachawi, wazinzi, wafiraji hawata ulithi uzima wa milele, ukajitenge nao wafanyao uovu.
 
Nimesikitishwa sana na huu uzi pamoja na baadhi ya comments za wadau. Kuna watu humu wanajifanya wao ni watakatifu kiasi cha kunyooshea vidole wengine na pia kumlaumu marehemu. Ngwair ni mmoja wa mamilioni ya watz wahanga wa hayo madawa. Kwanini tulaumu wanywaji wa vilevi huku tukisifia viwanda vinavyotengeneza hivyo vilevi?

Mtu akikupiga ngwala akakuangusha kwa lengo la kukuchelewesha mashindanoni, hilo ni kosa lake, lakini wewe uliyeangushwa kuendelea kukaa hapo chini ni UPUMBAVU wako.

Hakuna aliyesema kwamba yeye ni mtakatifu, lakini kuna mambo yapo wazi na si ya kuyaunga mkono. Ngwea hakutumia madawa sababu ya kukosa kwake elimu juu ya madawa bali alitumia madawa kwa fahari ya maisha yake. Watu kuleta madawa ya kulevya si kisingizio cha wewe kuyatumia na kujiita muhanga.

Ashakhum si matusi 'wengine wameleta condom, haya kanunue basi ujamiiane na ndugu zako kwa kuwa si kosa lako ni kosa la walioleta condom sokoni'

Vijana tutumie vyema akili zetu. Yule mpumbavu aliyekufa, ana wapumbavu wengine wengi nyuma yake. Ili wapumbavu mliobaki muelewe dhahama ya upumbavu, ilipaswa sababu ya kifo chake ielezwe pale kwenye kusanyiko na sio kujilizaliza eti Mungu amuweke mahali pema peponi.

Hakuna mtakatifu, lkn jitahidi kusafisha njia zako kadiri uwezavyo. Unafiki ndio unatuponza. Usipende kuelezwa maneno matamu, penda kuelezwa ukweli. Wakati anatumia hayo madawa na kuweka ------ nje wote tuliona ni sawa, ila leo kafa ukweli huo huo haukubaliki.

UNAFIKI NDUGU ZANGU, unafiki mbaya. Issue si ulikufaje, issue ni uliishije. Maisha ya kipumbavu ndio huelezea kifo cha mtu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom