LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,977
- 37,879
Wakati nasoma chuo, profesa wetu mmoja aliwahi kutuambia, " Wewe kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu, nikikuuliza unitajie jina la mji mkuu wa Tanzania, halafu ukaandika DODOMA, I will give you a BIG ZERO! Kwa nni? kwa sababu majibu yako hayawezi kuwa tofauti na majibu ya mtoto wa Darasa la mtano au mbeba mizigo wa pale bandarini, coz hata yeye ukimuuliza swali hilo atakupa jibu hilohilo sasa kutakuwa na tofauti gani kati ya mwanafunzi wa chuo kikuu na mwanafunzi wa darasa la tano au mbeba mizigo wa bandarini..WEWE KAMA MSOMI W CHUO KIKUU, NIKIKUULIZA MJI KUU WA TANZANIA NI NINI, HAUTAKIWI KUISHIA KUSEMA DODOMA! UNATAKIWA UENDELEE MBELE ZAIDI KWA KUTOA SABABU, KWA NINI DODOMA, NANI ALIYEPENDEKEZA DODOMA UWE MJI MKUU WA TANZANIA NA ALITOA SABABU GANI, UNADHANI ALIKUWA SAHIHI KUUPENDEKEZA MJI WA DODOMA? KAMA SIO SAHIHI UNADHANI NI MJI GANI ULIPASWA KUWA MJI MKUU NA KWA SABABU GANI? NA KAMA DODOMA IKIVAMIWA NA KUANGAMIZWA AMA IKIKUMBWA NA GHARIKA KAMA TETEMEKO LA ARDHI N.K KIASI CHA KUU DESTROY MJI UNADHANI NI MJI GANI MWINGINE WA TANZANIA UTAFAA KUWA MJI MKUU . NATEGEMEA KARATASI YAKO YA MAJIBU ITAKUWA NA KUANZIA ANGALAU KURASA KUMI NA ZAIDI.......Mwisho wa kunukuu..
Kwa kutumia hoja na mantiki ya profesa wangu, leo ninaomba kuwauliza wana JF wenzangu, hivi neno " ALAMA ZA NYAKATI " huwa linamaanisha kitu gani haswa? Mimi ni miongoni mwa mamilioni ya watanzania wanao litumia neno hili mara kwa mara kama mazoea tu bila kuujua undani wake..
WANA JF WENZANGU NAOMBA MNISAIDIE KUJUA! WITH MUCH RESPECT AND APRECIATION