Alama mpya za ufaulu zapingwa

Alama mpya za ufaulu zapingwa

Haya majanga yataitokea puani serikali ya ccm kwasababu wamewapa wanafunzi ruhusa ya kula, kuchati fb,kusikiliza miziki ya bongo fleva, kuzurura halafu pktoba wakutane mjengoni. Haingii akilini kufanyia majaribio maisha ya watu kwakuwaharibia mfumo wamaisha kwakuwapa mwanya mkubwa wakufaulu kwa marks za ajabu ajabu, ama kweli kipofu kaona mwezi kadhani harufu ya wali. Hongereni kwa huu upofu mnaozidi kuuendeleza,hiyo ''big results now'' inawazuzua hadi mnaleta majanga yatakayogharimu maisha ya watoto wetu. Watanzania wenzangu tutambue kwamba watoto wetu ndio watakaoathirika na mfumo huu usio na chembe ya matumizi ya akili ya kawaida ktk kufikiri,kuamua na hao wadau ambao mnasema mmewashirikisha inaleta utata na wao pia inawezekanaje washiriki upuuzi huu kama ni wadau wa elimu kweli ????????? Serikali kama kweli hili mmeliamua liwe hivi kwanini waziri anapingana na katibu mkuu wake???? Kwanza hii ni dalili yakukurupuka, pili wizara na watendaji wake wote hawajui watendalo,tatu, wizara haina bodi yawashauri wakitaaluma ndio maana kila mtu anakuja na wazo lake halafu mnaishia kuzozana kwenye vyombo vya habari......aibu yenuuuu hiyo wizara ya elimu. Na wewe rais inakuwaje unamtoa mtu kwa matrekta ,ma cartepiller unampa wizara ya elimu???????/ huoni kama unawadharau wananchi sasa hebu ona madhara yake watu wanaamka nakuja na upuuzi eti wanafanya majaribio kwamda wamiaka minne... Hebu tufikiri haya sio mahindi wala kilmo cha pamba ambacho unaweza chukua mbegu fulani kujaribu kama zinaweza kuzalisha magunia mengi, hii ni elimu na maisha ya watu hebu acheni huu upuuzi na maisha ya watu.
 
Jamaa wanataka kupotezea eti wanazungumzia mambo ya Div 5 na Div 0 badala ya kutoa maelezo kuhusu tangazo lote. Lukuvi amesema taarifa ya Mchome si taarifa ya Serikali, je, ina maana kuwa alichotangaza Prof Mchome kila kitu ni batili? Watoto wetu wanafanya mtihani tuambiwe kama wataendelea kupanuliwa magoli kama alivyotangaza Mchome au tufuate ya Lukuvi na Mulugo?

Mkuu uliona mbali, hili jambo bado lina sintofahamu nyingi naipongeza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kwa kuingilia kati watanzania tuambiwe lengo hasa la kushusha hivyo viwango ni nini?
 
Utaratibu huu mya si yote ni mabaya. Mpango huu ni WIN win kwa wote na unaongeza wigo mrefu kwa wale wanojua toka awali wanataka kufanya nini baada ya kumaliza masomo yao.

Kwa mfano, kwa utaratibu wa zamani kama kijana kapata kidato cha nne, Fizikia-C, Kemia-C, Baioloji-B, Hisabati-D, Civics-D, Kiingereza-F, Kiswahili-F. Huyu anapoint 26 dv 4. Kwa sheria za NECTA hawezi kuendelea na masomo A level. Lakini mwingine atayepata kiswahili D katika mtiririko huo atakuwa na Point 25 div 3 na kwa kanuni za Necta atachaguliwa kwenda A level.

Lakini hawa wanafunzi wawili watapokutana A level (PCB) wote ufaulu wao ni sawa yaani fizikia-C, Kemia-C na Baioloji-B) Hivyo kuwa na uwezo wa kimasomo sawa. Hakuna kilichoshuka hapa.

Nani ni mshindi katika hili: Ushindi ni kwa shule zile zitazojiona zinaupungufu wa walimu wa masomo fulani na kuwaelekeza wanafunzi wao wasome kikombi zaidi kwa kulenga lengo kuu la kujua watafanya kazi gani baada ya masomo.

Utaratibu huu kimsingi si mpya baadhi ya vyuo vikuu umekuwa ukiutumia katika kuchagua wanafunzi kuanza mwaka wa kwanza. Kwa mfano kwa wanafunzi wa udaktari waendao Bugando, KCMC, Kairuki n.k Katika masomo ya msingi yaani PCB, vyuo hivyo vyote vimeitupilia mbali Fizikia na unaweza kuingia kwenye kozi hiyo hata kama Fizikia umepata "F". Ni Muhibili univ tu ndio imekazania Fizikia kuwa uwe na min "E".

Hali hii tutaendelea kuiona katika vyuo vingi kwani mfumo wetu wa elimu umewabebesha mzigo mzito sana wanafuzi hata masomo yasiyo na lazima. Soko la kazi ndio muamuzi, na vyuo ndio watayarishaji wa mwisho wa wanafunzi kuelekea kazini.

Ni kihitimisha napenda kusema tu kuwa mfumo wetu wa elimu unahitaji mabadiko makubwa sana yanayoendana na wakati. Hata yaliyofanyika ni madogo bado tuna safari ndefu. Tujifunze toka kwa wenzetu.
 
Huyo Sifuni mchome ni product ya UDSM, kasoma degree and masters hapo hapo (law) akaenda marekani for phD. Na amewahi kuwa dean hapo kitivoni udsm.

Jamaa ana akili sema watz hawataki mabadiliko which is th big problem now. Kama mabadiliko yana facts za kisayansi lazma tuyakubali hayo mabadiliko.

mkuu kuteremsha viwango vya ufaulu kuwafanya wanafunzi wengi (hata wasiojua kusoma na kuandika) waonekane kuwa wamefaulu ili kuwafurahisha wazazi (wapiga kura) ni fact ya kisiasa au kisayansi? hebu onesha hio fact yako ya kisayansi ni ipi sio unapayuka tu.
 
mkuu kuteremsha viwango vya ufaulu kuwafanya wanafunzi wengi (hata wasiojua kusoma na kuandika) waonekane kuwa wamefaulu ili kuwafurahisha wazazi (wapiga kura) ni fact ya kisiasa au kisayansi? hebu onesha hio fact yako ya kisayansi ni ipi sio unapayuka tu.

Soma vizuri niliyoandika between the lines ndio unijibu. Kweli kuna wataopata na kuna wataopoteza, jaribu kuangalia kwanza wataopata kwa mfano nilioutoa, bila kusahau yale ya vyuo vikuu. Jibu kwa marefu, tafadhali.
 
ikiwa wanafunzi wanaanza form one hadi wanamaliza form four bila kuwa na mwalimu wa somo la biology, hivi marks za CA za wanafunzi kwa somo kama hilo huwa zinapatikanaje?
 
Back
Top Bottom