Alama mpya za ufaulu zapingwa

Alama mpya za ufaulu zapingwa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,329
Alama mpya za ufaulu zapingwa

na Waandishi wetu
Tanzania Daima

SIKU moja baada ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya marekebisho katika upangaji wa viwango vya alama za matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne na sita kwa kufutwa daraja sifuri na kuwekwa daraja la tano, wadau na wasomi wameponda mfumo huo.
Wakizungumza na gazeti hili, wadau hao walisema kuwa tatizo si kushuka kwa kiwango cha ufaulu, bali uwepo wa elimu bora nchini.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema kuna mifumo miwili ya elimu nchini inayotumika, ambayo ni ule wa watu masikini na wenye nafuu ya maisha.
Alisema hali hiyo inaanzia chekechea hadi vyuo vikuu, huku akihoji wizara husika mfumo wa aina hiyo unamlenga nani, kwamba tatizo lililopo ni ubora wa elimu hasa katika shule za umma.
Bashiru alisema kwenye mifumo hiyo inayotumika, ule wa masikini upo kwenye shule nyingi za umma ambako ndiko kwenye watoto wengi wanaofeli kutokana na kukosa vifaa vya kufundishia, maabara na walimu.

“Katika shule za umma watoto wengi hawasomi, hawana maabara, sasa wizara inawatahini nini? Mageuzi yoyote ambayo yatashindwa kuondoa matabaka hayawezi kuleta elimu tunayoitaka,” alisema.
Alisema ubora wa elimu utawahusu wanafunzi hao wanaosoma shule za michepuo ya Kiingereza, kwani ndio watakaokuwa wanafaulu kwa kuwa shule zao zina mfumo mzuri unaoeleweka na viwango walivyojiwekea kama mwanafunzi hatafikia atarudia darasa ama kuachishwa shule.


Naye mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Prof. Herme Mosha, alisema kama wizara inataka kuongeza idadi ya watu katika ufaulu waliofanya mtihani, inapaswa kuboresha elimu.
“Sio mara ya kwanza tumechezea vigezo, 2007 tulibadilisha viwango tulivyokuwa navyo tukaweka alama za chini, wanafunzi wengi wakachaguliwa, matokeo yake mtihani wa mwisho wa kidato cha nne kukawa na matokeo mabaya,” alisema.
Alisema lililofanyika sio utatuzi wa tatizo, bali wizara iangalie nini kinasababisha ubora wa elimu kushuka.
Kwa mujibu wa Prof. Mosha, wizara husika iangalie ni nini kinachowafanya wanafunzi wasisome badala ya kupandisha viwango kwa aina hiyo waliyoitumia.

Dk. Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema tatizo lililopo ni mfumo mbaya wa ufundishaji, kwani kupanga madaraja kwa aina hiyo si suluhu ya kutatua changamoto iliyopo.
Alisisitiza kuwa kwa staili hiyo, serikali haitoi tatizo bali inajaribu kuficha tatizo, hivyo hakuna cha kushangilia kwa mfumo huo walioutangaza.

Mwalimu wa sekondari, Josephat Ammy, alieleza kuwa mfumo huo utamfanya mwanafunzi kubweteka na kutochukulia umuhimu suala la elimu kwa kudhani kuwa uwezo wa kufaulu anao.
“Wao walitakiwa waje na suluhisho la elimu na kujua kwanini wanafunzi wanafeli, sasa wanachofanya nini? Wanaondoa daraja ziro halafu hao wa daraja la tano wanakwenda wapi?” alihoji.
Naye mmiliki wa shule za Green Acres, Julian Bujugo, alisema kuwa mfumo huo sio mbaya kwani wanafunzi watafanya mtihani kwa kutumia mitaala.
“Mfumo huu ulikuwepo hapo awali kabla ya kutolewa, sioni kama una ubaya. Ni mzuri, utasaidia kwa wanafunzi tofauti na mwaka jana walitunga mitihani ambayo haikuwa kwenye mitaala,” alisema.

Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gracian Mukoba, alisema kuwa kubadilisha alama itakayowasaidia watoto wengi kuonekana wamefaulu haisaidii kwani ndiyo kwanza kunaongeza zao la ujinga.
Alisema kama walikuwa wanatafuta kufurahiwa na wazazi na wanafunzi, basi wangeweka alama A, B, C plus bila kuwa na alama hizo za daraja hadi la tano.

Kwa mujibu wa Mkoba, kilichofanyika ni siasa tu na kucheza na saikolojia za wazazi, ambazo tayari zimeathiriwa na mfumo mbaya wa elimu ambapo idadi kubwa ya watoto wanaofeli inaongezeka kila kukicha.
“Yaani hapa ni kama bomba, unakuta linatoa maji machafu ya tope. Baada ya kuangalia nini chanzo chake wewe unaamua kubadilisha koki na kuweka nyingine wakati si suluhisho,” alisema.
Mukoba alisema njia sahihi za kuboresha elimu serikali inazijua kwa kuwa tayari walishatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuunda tume, kufanya utafiti, hivyo majibu tayari wanayo.

Naye mwalimu wa vituo vya elimu ya Taasisi ya Watu Wazima, Stanslaus Sekuru, alisema kuwa mfumo huo utaboresha elimu kwa sababu hapo awali wanafunzi walikuwa wakiumia sana.
Alitolea mfano daraja la nne akisema mwanafunzi anakuwa na alama 26, lakini akiwa na alama C tatu anashindwa kuendelea na kidato cha tano na mwenye daraja la tatu mwenye alama 25 na C tatu yeye anapewa nafasi ya kuendelea.

Mwalimu Charles Mkwidu ambaye ni mratibu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima, alisema mpango huo ni mzuri ila uwekewe mkakati wa kuwasaidia wanafunzi kupenda kusoma, hasa masomo ya sayansi kwani wengi husoma wakati wa mitihani tu.
Naye mwanafunzi anayerudia mitihani, aliyeathiriwa na matokeo ya mwaka jana, Jesca Charles, alisema huenda ikawasaidia au la kwa kuwa mitaala ya elimu ndiyo iliyowaponza hadi wakafeli.
 
Halafu bado wanajiita "Serikali sikivu" wakati wanaharibu kila sekta nchini. Wataalamu wanaoweza kuipa Serikali hii ushauri mzuri wa kuboresha elimu nchini tunao kibao lakini hawasikilizwi, matokeo yake wanasiasa ambao hawajui chochote kuhusu elimu wanaendeleza usanii wao ambao unazidi kushusha kiwango cha elimu nchini.

Haya ni matokeo ya BIG RESULTS NOW. Kwa kuogopa aibu wanateremsha viwango vya ushindi ili ionekane kwamba wanafunzi wengi wameshinda na hayo ndio matarajio yao. Bado tunaendelea kuchezea elimu yetu. Ni lini tutajifunza?
 
"ZERO" kinadharia ni SUALA AIBU UNAPOKUWA UMEPATA KTK MTIHANI,MWANAFUNZI HUSOMA KWA BIDII SANA ILI AIEPUKE "ZERO",MBAYA ZAIDI NI PALE "ZERO" INAPOREMBWA NA KUPAMBWA, "KWA MANTIKI YA HUJAFELI SANA MAANA HUJAPATA "ZERO"hakika kiwango cha elimu na bidii za wanafunzi vimeshuka mpaka kuremba kwa mtindo huu,WHO PROGRAM THIS SHITS
 
tatizo si kuwa na division 5,tatizo unaondoka shule ukiwa na mchele kichwani au chuya.....
 
kuna msemao......Kila Shetani na mbuyu wake, yale yale ya Mh. Mungai wakati uleeeeeeee, sasa Mr. Dr Shukuru Kawambwa.......nadhani 2016.... tutarudi tena pale pale pa zamani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
kwanini hili lisiingizwe kwenye maajabu ya Tanzania watu wakaja wakaona wakalipia kivutio hiki kipya cha utalii.
Tuwaombe wizara waweke fees ndogo kwa watalii wa ndani na kubwa kiasi kwa wa nje watakaotaka kujua jinsi mfumo huu unavyostajabisha
 
Halafu bado wanajiita "Serikali sikivu" wakati wanaharibu kila sekta nchini. Wataalamu wanaoweza kuipa Serikali hii ushauri mzuri wa kuboresha elimu nchini tunao kibao lakini hawasikilizwi, matokeo yake wanasiasa ambao hawajui chochote kuhusu elimu wanaendeleza usanii wao ambao unazidi kushusha kiwango cha elimu nchini.

Ukitazama kwa jicho la kiuchumi na kijamii utapata kuona kuwa madaraja haya ya ufaulu yanafanana na madaraja ya kiuchumi na kijamii yanayojengeka kwa kasi hapa nchini. Kwa mfano, ni wazi ufaulu wa daraja la kwanza kwa kiasi kikubwa unaendana na daraja la kiuchumu na kijamii alilomo ama analotoka mwanafunzi husika, ingawaje mwanafunzi anayetoka daraja la tano la kijamii na kiuchumi anaweza kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza, lakini ni asilimia kidogo sana ya 5th class citizen anayweza kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza.

Nionavyo ni kuwa mataraja haya yana-akisi mgawanyo wa kiuchumi na kijamii nchini mwetu, tatizo ni kuwa hakuna jitihada za makusudi za kuwakwamua walionasa kwenye daraja la tano la kijamii kama alivyotanabaisha Bashiru Alli kuwa ufaulu wa daraja la kwanza utanufaisha wanaosoma kwenye mfumo wa elimu ya kimombo (private education system) ilhali wengi watakaonasa kwenye daraja la tano ni wale wa shule za umma (public schools). Inashtua sana maana serikali ya CCM ni kama imewasusa Watanzania walio wengi maana badala ya kupunguza pengo la umasikini, yenyewe inajenga misingi itakayo-ongeza pengo la umasikini na kujenga matabaka miongoni mwa jamii kwa kutumia mfumo wa elimu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Lakini wadau walishirikishwa. wakuu wa shule binafsi, viongozi wa vyuo vikuu binafsi na umma. Mabaraza ya ushauri vyuo vikuu.Tassisi ya Elimu nk.
40% CA ikisimamiwa vizuri mfumo huu ni mzuri.
 
Kuna mdau aliwahi kuulizia CV ya Mchome humu sijui alikuwa anachimba nini???!!!!

Huyo Sifuni mchome ni product ya UDSM, kasoma degree and masters hapo hapo (law) akaenda marekani for phD. Na amewahi kuwa dean hapo kitivoni udsm.

Jamaa ana akili sema watz hawataki mabadiliko which is th big problem now. Kama mabadiliko yana facts za kisayansi lazma tuyakubali hayo mabadiliko.
 
Lakini wadau walishirikishwa. wakuu wa shule binafsi, viongozi wa vyuo vikuu binafsi na umma. Mabaraza ya ushauri vyuo vikuu.Tassisi ya Elimu nk.
40% CA ikisimamiwa vizuri mfumo huu ni mzuri.

ipogolo mkuu mabadiliko yote yaliyofanyika ni mazuri sema watu hawajaelewa. Na ofcoz panakuwa na standard ambazo zinawachuja watoto wenye uwezo na wanajulikana mapema
 
Last edited by a moderator:
Huyo Sifuni mchome ni product ya UDSM, kasoma degree and masters hapo hapo (law) akaenda marekani for phD. Na amewahi kuwa dean hapo kitivoni udsm.

Jamaa ana akili sema watz hawataki mabadiliko which is th big problem now. Kama mabadiliko yana facts za kisayansi lazma tuyakubali hayo mabadiliko.

ok thanx,tuachane na utu wake!!!!

Kwa hiyo mabadiliko yenye facts za kisayansi ndio hii ya kuchakachua madaraja ya ufaulu badala ya kuongeza nguvu kwenye mashule,walimu na vitendea kazi????!!!!

Mmmmh haya! !!!!
 
ipogolo mkuu mabadiliko yote yaliyofanyika ni mazuri sema watu hawajaelewa. Na ofcoz panakuwa na standard ambazo zinawachuja watoto wenye uwezo na wanajulikana mapema

Kwa nini mnakomalia product badala ya process????!!!!
Kwa nini focus iwe standard za kuchuja na sio standard za kufundishia na vitendea kazi pamoja na mazingira husika?????
 
Last edited by a moderator:
Nimepokea kwa masikito namna ambavyo madaraja yamepangwa. Tunasema matokeo makubwa sasa kama mpango wa miaka 3. Matokeo makubwa katika sekta ya Elimu hayapatikani kwa mda mchache hivi. Ndio maana serikali imeamua ilazimishe kuyapata kwa kutanua goli kwa kiwango hichi. Cha kusikitisha wizara inasema wanasiasa, TAHLISO wamebariki mfumo huu mbovu.
 
Wana janvi,
Nimetafakari sana kuhusu msitakabali wa elimu yetu na sasa ninadhani njia pekee iliyobaki kuweza kuinusulu ni kuipiga chini serikali ya CCM.Hii ni kwa sababu moja kubwa;kwamba pamoja na ukweli kuwa hawana mipango yoyote ya kisera ya kuweza kuinusuru elimu lakini pia hawako tayari kusikiliza ushauri wowote wa wadau.Kwa bhati mbaya CCM wanadhani kuwa wakiwanyima watanzania elimu nzuri wao ndo watatawala milele(hii si kweli) na wanajidanganya tu.

Hebu kumbuka kuanzia Mungai alifuta bahadhi ya masomo "optional subjects" kama b/keeping,commace,f/art,music n.k kwa madai kuwa hayo yanaweza kusomwa kwenye ngazi za juu na aliunganisha masomo mengine(physics $chemistry),madhara ya maamzi hayo mpaka leo yanajionesha kwa sisi wadau wa elimu.

Wengine walijenga shule kwa jaziba na kujikuta hawana wanafunzi wa kuingia na wakaona kukabiliana na ilo na kufanya uhamisho wa moja kwa moja kutoka primary kwenda secondary na uhamisho huo ndo uliwezesha wanafunzi 5000 wasiojua kusoma na kuandika kwenda sekondari.Hapa serikali ikafanya kituko kingine eti inatoa mitihani ya kupima maarifa kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza(kkk); Rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa alimpatia mtoto wake wa darasa la kwanza mtihani huo na kumpa sharti la kusoma kuandika kwenye nafasi wazi bila kutumia karatasi ya pembeni alipata 48/50 na shuleni kwao wa kwanza alipata 48/50 wa mwisho 12/50 huku wengi wakicheza na ishirini.Alinieleza kuwa kwa maelekezo waliyopewa na serikali wote walikuwa wamefauru kwani wlionekana kujua kusoma,kuesabu na kuandika(Hata yule wa12 kwani aliweza kuandika jina lake,na kuesabu namba 1-25 kwa kuziandika)

KUkabiliana na hiyo hali wakafuta mitihani ya taifa kidato cha pili ifutwe,kelele za wananchi zimewafanya wairudishe kwa shingo upande ila sisi wadau wa elimu tunajua ni nini kinaendelea huku (NI GIZA TUPU).

Matokea ya kidato cha nne-2012 yalitoa pigo jingine na sasa wamejiandaa kudhibiti hali hiyo kutotokea tena (KAMA KAWAMBWA ALIVYOJIAPIZA KWENYE BUNGE LA BAJETI KUWA AHACHWE AJIPANGE ILI AHUKUMIWE KWA MATOKEO YA 2013) kwa kufanya uhalibifu mkubwa zaidi kuwai kutokea kwenye elimu ya tanzania.NDO HICHO MLIMUONA MCHOME ANAWASOMEA JUZI

Hakuna ziro na viwango vimebadilishwa ajabu ajabu

Yote 9 kidato cha sita ndo wamefanyia uhuni wa kutisha ni hii si bahati mbaya wanawajua wanafunzi waliowapeleka kidato cha tano-2013 na sasa wanawaandalia mazingira ya kufauru.Fikiria kwa utaratibu wa zamani mwanafunzi mwenye wasitani 54 alikuwa daraja D na kwa viwango vya sasa atakayekuwa na wasitani wa 50 atakuwa nadaraja B.HAYA NI MAJANGA.

NB;Wadau muhimu kama walimu katika hili hawajashirikishwa kwani madodoso waliyopewa ndo yanaendelea kukusanya na wengi wameyajaza wakati wa semina za kusimamia mitihani ya kidato cha nne.
 
ok thanx,tuachane na utu wake!!!!

Kwa hiyo mabadiliko yenye facts za kisayansi ndio hii ya kuchakachua madaraja ya ufaulu badala ya kuongeza nguvu kwenye mashule,walimu na vitendea kazi????!!!!

Mmmmh haya! !!!!

Mkuu kwani hayo mabadiliko ni kuchakachuliwa? Wizara imekusanya maoni kwa wadau mbali mbali eg kutoka vyuo vikuu, waalimu, wanasiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanafunzi. Mf zamani A km ilianzia 81 na sasa inaanzia 75 sio kuchakachua huko ni kupanga viwango ambavyo vinatengeneza stahiki halisi. Eg mitihani ile waliyofanya wanafunzi form four walipewa walimu wao wakafeli sana..hiyo unaitafsiri vipi? Na pia kupanga viwango vya madaraja haimaanishi ndio maboresho ya elimu yamesimama, bado ripoti inaelezea maslahi ya walimu, studying facilities etc.

Hivi kuna hoja kweli mtu unasoma form one hadi form iv then mtihani wa mwisho unapata 18 f katka masomo saba then unaambiwa umepata div ziro, ina mantiki? Hii ina tafsiri mbaya kabisa kwmba umefeli miserably lakini kuwepo kw continuous assesment, na kusema mtihan wa mwisho utacarry 60 percent ni sahihi. Huwezi kumpima mtoto aliekaa darasan kw miaka minne kwa mtihan wa masaa matatu na ukaconclude. Hata nchi za ulaya wanatumia huu mfumo.

Watz bado hatupendi kuridhia mabadiliko kwa sababu tunaogopa mabadiliko yatatudhuru. Vyuoni grade za ufaulu ndio hizi hizi lakini watu hawasemi
 
Wana janvi,
Nimetafakari sana kuhusu msitakabali wa elimu yetu na sasa ninadhani njia pekee iliyobaki kuweza kuinusulu ni kuipiga chini serikali ya CCM.Hii ni kwa sababu moja kubwa;kwamba pamoja na ukweli kuwa hawana mipango yoyote ya kisera ya kuweza kuinusuru elimu lakini pia hawako tayari kusikiliza ushauri wowote wa wadau.
Halafu tukishawaondoa hao wanaokuja wana mkakati juu ya elimu? weka sera zao kuhusu elimu tuzisome!
 
Halafu ukitaka kujua kuwa watanzania walio wengi hata hawajui kilichoongelewa wala kinachoendelea angalia kila mmoja kanyamaza like kwamba mzizi wa tatizo umepatikana!

Kutatua tatizo la ufaulu duni la ufaulu linatatuliwa kwa kubadili tena kwa kushusha madaraja ya ufaulu?!

Eti madaraja ya A na B ni nusu ya maksi zote 100%?!! jaman tuliona wapi hiki kitu?!

Eti kwamba pamoja na kushusha maksi katika madaraja bado zile division zikaongezwa upana (kuelekea madaraja ya chini) pia ili kulazimisha 'ufaulu'!!

Nashangaa maprofesa ndio waliotangaza hilo, kweli hawaoni kuwa tumeongeza upana wa goli ili kulazimisha matokeo?!

Mungu atusaidie tu! Naanza kuamini kuwa wasomi ndio walioifikisha hii nchi hapa ilipo, kimatendo ama kwa maneno potofu nao kukaa kimya ama kwa kutotimiza vyema wajibu wao!

TAHLISO wao ishu kubwa kwao ni boom na siasa! Sote ni mashahidi walienda kumtangaza Makamba Jr kuwa ndio wameona anafaa badala ya kuongelea matatizo ya msingi katika taifa!

Niliwahi kukaa na mtu mmoja ambaye yee anasema kuwa matatizo ya nchi yetu ni ya 'kiroho' so tunaweza kuwa na watu bora na bado tukashindwa kuyaondoa matatizo yetu, naanza kumuamini huyo jamaa aisee!
 
Back
Top Bottom