Hivi vikundi vya Al shaabab na venginevyo ni machine ya USA kwa ajili ya kuifanya Africa, MidEast kuwa mahali pa vita tu bila ya amani. Hii ndiyo inaitwa New World Order.
Mchina sasa hivi anaitaka Africa, na keshaichukua Africa kiuchumi-investments kwa asilimia kubwa sana. Hivi unadhani Wazungu-West watakubali hivi hivi tu waikose Africa?
Dawa- ni kuanzisha vita ili mikataba mipya ianze kusaigniwa. Tumeona Libya-Wazungu walipoona wameshaanza kuikosa kwa Mchina- dawa ni regime change. Sasa hivi Libya ipo mikononi mwao.
Sasa hivi wanaitaka East Africa. Kwa nini? Kuna port kubwa inayoingiza na kutoa mali kwenda na kurudi kutoka China na Asia. Dawa- anzisha vita. Kama hamna amani hamna biashara.
USA tayari wanazo Drones-Attack ktk East Africa ambayo inaweza kuattak popote pale kama wakipata target ya Al shaabab.
Kazi tunayo EA. Hatuna Amani tena
Kama kuna tatizo ambalo ni kubwa hapa Afrika ni kujaribu ku-link kila tukutanacho na watu wa Magharibi. Sasa tunakuwa kama tumesahau kuwa Somalia ni nchi isiyokuwa na serikali kwa miaka zaidi ya 20 na sisi waafrika tunaona sawa tu!. Nionavyo mie huu sasa ndiyo muda wa kuona matunda ya kutokuwapo serikali pale nchini Somalia. Wale usidhani ni US au China au nani...!
Wale wasomali waliozawa miaka ya 80 na 90 walikuta hakuna mfumo wa kielimu na kijamii, hawakupata fulsa kama unazopata wewe hivyo wamekua bila matumaini na sasa wanajaribu ku-survive. Tukiri makosa yetu kwa kuacha Somalia iangamie kwa miaka yote. Na kama hakutakuwepo na serikali pale Somalia kwa miaka ijayo basi tatizo la wasomali litakuwa kubwa kuliko tuonavyo sasa.