By
NasDaz
WA KULAUMIWA sio TISS, bali ni mimi hapa ila naomba mnisamehe kwa wale ambao mngependelea Al_jazeera wangekuwa hapa Dar.
Bosi mkuu wa Al-Jazeera alinipa kazi ya kutathimini potentiality ya Dar kama ingeweza kuwa makao makuu ya Al_jazeera kiswahili. baada ya kufanya utafiti wangu nikagundua yafuatayo ambayo niliandikia ripoti na kuipeleka kwa BIG BOSS wa Al_Jazeera:
1. Hakuna dalili ya kuwapo kwa wanaataluma kwenye tasnia ya habari wenye shahada ya uzamivu (PhD) ambao wapo kwenye game.
2.Hata wanahabari wenye shahada ya uzamili (Masterz) nao ni wa kutafuta
3.Source kubwa ya waandishi wa habari ni pale mitaa ya Ilala/Buguruni al-maarufu DSJ
4. Waandishi karibu wote ni ama Chadema au CCM na hawawezi kuficha hisia zao za ushabiki wa vyama kwenye vyama hivi
5.Source yao kubwa ya habari ni Press Conferences
6.Waandishi wengi hawavutiwi na Press Conferences zisizo na bahasha.
7. Baadhi ya waandishi hawaoni taabu kunyofoa habari za mitandao ya kijamii kama JF na kuzifanya ndio habari za kwenye vyombo vyao
8.Waandishi wengi ni vigeu geu; hawana uhuru wa maoni na hawana tofauti yoyote ile na wanasiasa! Kwamba, leo akiandikia Tanzania daima ataisifia CHADEMA na kesho akiwa UHURU ataisifia CCM! In short, ni kama waganga njaa!
9........ Hii ya tisa, sitaisema, naogopa kuwatoa watu mapovu
10. Standby generators 24/7
Baada ya kupeleka hiyo ripoti, sikupata feedbback hadi niliposikia kwamba wameamua kuwa Nairobi! Nisameheni kwa kukosa uzalendo!
hayo mambo nitaya-turn upside down endapo CNN watakuja na kunipa kazi kama hiyo tena!!!
Nakuunga mkono kwa asilimia 90 kwa hoja zako hapa. Ni kweli quality ya waandishi wa habari wa Tanzania inasikitisha mno. Kiwango chao ni cha chini kabisa. Hawana mwelekeo wa kuandika habari za uchambuzi zaidi ya kuelekea kuandika habari za 'reporting' and not 'analysis'. Ndio maana magazeti mengi yamejaa habari za ...fulani alisema hivi na vile. Para ya pili akizungumza jana Dar es salaam huyo alisema kwamba....
Yaani ni uandishi wa habari wa ajabu kabisa. Gazeti peke ambalo angalau linajaribu kuandika analysis ni MwanaHalisi lakini nalo siku hizi limeingiliwa na mafisadi ambao inaelekea wamelinunua ndiyo maana unaona limeanza kuwaandama akina NAPE.
Gazeti la MTANZANIA ndiyo ni la ajabu kabisa limejaa longolongo za mafisadi yaani mara elfu hata UHURU la CCM.
Kwamba waandishi wa habari wa Tanzania wamejaa ubabaishaji n i matokeo ya jamii yetu. Huwezi kuwatenga waandishi wa habari na 'society' tuliyomo. Society yetu ikoje? Ni 'society' iliyojaa uvivu; wivu; majungu; maneno mengi; rushwa; kutaka vitu vya urahisi; uswahili; mbwembwe; kujisifu kwingi pasipo maana; umbumbumbu; ulimbukeni wa kuiga watu wengine; rushwa ya wazi wazi; unafiki; ujinga. na kadhalika. Haya ndiyo baadhi ya mambo yayoididimiza Tanzania. Watu wameingia mikataba hewa na wameiba mamilioni eti wanaachiwa hivi hivi ingekuwa China wangekula risasi. Mtu kama Lowassa ameruhusu Richmond ituibie na bado anataka urahisi na wako watanzania wanaomuunga mkono. Akina NAPE wanaotaka kuisafisha CCM eti nao sasa wanaandamwa kwa kuwa tu baadhi ya waandishi wa habari wamehongwa na mafisadi na ambao baada ya kupata laki tatu tatu wanashindwa kupiga picha ya mwarabu wa richmond.
Watu wamekula UDA lakini hakuna mwandishi wa habari anayeandika kwa kina wamekulaje. Utaona blahblah tu kwenye magazeti wanakazania tu kuandika maneno ya Masaburi kwamba eti wengine wanafikiri kwa makalio. Yaani mwandishi wa habari anaona hiyo ndiyo habari na wasomaji wanaishabikia lakini siyo issues zile za kina.
Slaa naye eti anapigiwa upatu awe Rais wa nchi hii. Mbowe naye eti ni tishio kwa CCM na TUNDU LISSU ni kiboko na pia eti LEMA. waandishi wa habari ndio wanaoaandika habari za udaku na ku-swet agenda kwa mambumbumbu watanzania.
mambo ya maana ya maendeleo hayaandikwi. Huoni makala kwenye magazeti za uchambuzi wa issues. Huoni makala zinazoandika umhimu wa kuwa na reli ya kutoka Dar hadi Kigoma, makala zenye data za kiuchumi na. Huoni makala kwenye magazeti zinazochambua umuhimu wa kujenga haraka babarabara kutoka Mbeya kwenda Sumbawanga na kadhalika. Huoni makala zinazochambua kwanini hakuna sababu tena ya ujenzi wa nyumba na ofisi katika jiji la Dar es Salaam badala yake tujenge mji mpya labda huko Kimara au Kibaha au Dodoma. Utaona makala za kijinga eti WanaCCJ wahamia Mbeya na sisi wasomaji tunashabikia habari za upuuzi. In Tanzania we do not have a think tank. Hatuna watu wa kufikiri. Watalaamu wapo lakini hawapati nafasi. Ma -DC wnaoteuliwa ni wacheza ngoma baadhi yao na ukiambiwa huyu ni DC unaweza kuingia uvunguni kwa aibu. DC gani ambaye ni mwakilishi wa Rais katika eneo analoongoza hajui hata maana ya uchumi na maendeleo ya kileo? Magazeti yetu hayaandiki kwa kuwa waandishi wa habari wengi ni uchwara kama ilivyo kwa watanzania wengi. Wanyarwanda wanakuja na kuvamia nchi yetu tunachekelea. Wakenya wanakuja nchini kwetu na kuona Wanawake wetu sisi tunachekelea na these isues you cant even see them in our newspaers. The kenyans want land and to do so they use or aplly a number of methods including marriages. sasa sisi tumebaki kujisifu Tanzania ni nchi ya amani. Watanzania hatuzalishi badala yake tumebaki kuwa wachuuzi wa bidhaa za Thailand. Pita katika barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo hadi Kibaha. Pembzoni zimejaa kiolsks za bia eti hiyo ndiyo biashara. UJINGA. magazeti hayaandiki. Nchi gani itaendelea kwa kila mtu kuwa na kosk pembezoni mwa barabara huku viti vya plastick vyekundu, kijani, njano,bluu na kila rangi vikiwa vimetanda. Singapore miaka 50 iliyopita ilikuwa kama Tanzania lakini nchi hiyo leo hii ni First world na sisi tumebaki hapa tulipo. Huko Singapore wana CCM ya huko ambayo iko madarakani tangu wakati hu. Lakini tofuati iliyopo ni kuwa CCM ya Singapore ina watu wa kufikiri tofauti na CCM ya Tanzania. Magazeti hayandiki haya tumekazania kuandika kikombe cha babu na watanzania wanapenda kusoma habari za kiombe cha babu na gamba la CCM. stupid.