Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,196
- Thread starter
- #101
Niliwahi kusema hapa TISS ilipaswa kuwa na kitengo kwaajili ya uchumi, ona sasa Kenya walivyochangamkia Sudan Kusini sisi tumelala ukisikia tuko huko ni juhudi zetu wenyewe lakini ukweli ni kwamba hiyo nchi ina-import skilled labour sasa hivi na wanaofaidi hilo ni Kenya.
Kama tungekuwa na TISS imara kwenye economics changanya na utulivu uliopo nchini kwetu tungekuwa na mashirika mengi ya kimataifa hapa kuliko Kenya na kampuni nyingi za kimataifa, hakika ingesukuma gurudumu letu la maendeleo mbele, lakini jamaa wapo kwa kulinda viongozi mafisadi na wanatumia nguvu kubwa sana kuhakikisha mafisadi hawatoki madarakani.
Mkuu hili ni tatizo kubwa tulilonalo. Sisi outsiders hatujui wanafanya nini, wao insiders wanajua wanafanya nini. Lakini tukiangalia kwenye upande wa ulinzi wa viongozi naweza kusema wanafanya kazi yao maana tunaona mafisadi wanalindwa, lakini kwenye upande wa uchumi naona mambo ni sifuri. Ina maana hakuna kitengo kinachoshughulikia suala hili.
Clearly tunaona jinsi Kenya ilivyospearhead kujitenga kwa Sudan Kusini tayari wanaanza kupata huge benefits, sijui sisi tunafanya nini. Au ndio yale yale kujisifia kuwa kisiwa cha amani, lakisiwa kilichojaa uzembe na ubabaishaji.....