Wakuu nilipost thread kule kwenye jamii intelligence naona imefinywa. Ilikuwa ni kuuliza ni kwanini mashirika karibu yote yanafungua ofisi zake Nairobi na sio Mwanza, Arusha au hapa Dar es salaam? Je TISS wanakuwa na taarifa in advance kuwa jamaa wanataka kufungua ofisi hizo? wana lobby ili jamaa wafungue ofisi hizo Tanzania? Ofisi hizo ni mzingo kwa nchi au ni advantage? Najua kuna watu hapa wenye uelewa kuhusu issue hii, ni vizuri tukiwa na TISS inayendana na wakati na sio inayfanya kazi kama za miaka ya karne ya 19
WA KULAUMIWA sio TISS, bali ni mimi hapa ila naomba mnisamehe kwa wale ambao mngependelea Al_jazeera wangekuwa hapa Dar. Bosi mkuu wa Al-Jazeera alinipa kazi ya kutathimini potentiality ya Dar kama ingeweza kuwa makao makuu ya Al_jazeera kiswahili. baada ya kufanya utafiti wangu nikagundua yafuatayo ambayo niliandikia ripoti na kuipeleka kwa BIG BOSS wa Al_Jazeera:
1. Hakuna dalili ya kuwapo kwa wanaataluma kwenye tasnia ya habari wenye shahada ya uzamivu (PhD) ambao wapo kwenye game.
2.Hata wanahabari wenye shahada ya uzamili (Masterz) nao ni wa kutafuta
3.Source kubwa ya waandishi wa habari ni pale mitaa ya Ilala/Buguruni al-maarufu DSJ
4. Waandishi karibu wote ni ama Chadema au CCM na hawawezi kuficha hisia zao za ushabiki wa vyama kwenye vyama hivi
5.Source yao kubwa ya habari ni Press Conferences
6.Waandishi wengi hawavutiwi na Press Conferences zisizo na bahasha.
7. Baadhi ya waandishi hawaoni taabu kunyofoa habari za mitandao ya kijamii kama JF na kuzifanya ndio habari za kwenye vyombo vyao
8.Waandishi wengi ni vigeu geu; hawana uhuru wa maoni na hawana tofauti yoyote ile na wanasiasa! Kwamba, leo akiandikia Tanzania daima ataisifia CHADEMA na kesho akiwa UHURU ataisifia CCM! In short, ni kama waganga njaa!
9........ Hii ya tisa, sitaisema, naogopa kuwatoa watu mapovu
10. Standby generators 24/7
Baada ya kupeleka hiyo ripoti, sikupata feedbback hadi niliposikia kwamba wameamua kuwa Nairobi! Nisameheni kwa kukosa uzalendo!
hayo mambo nitaya-turn upside down endapo CNN watakuja na kunipa kazi kama hiyo tena!!!