Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
19,000
2,000
Mkuu ni swala la muda tu! Wahenga walisema "All power corrupts, and absolute power corrupts absolutely"!!! Kapigiwa simu live na mtukufu Rais juzi kati tayari mapembe yameota anasahau cheo chake ni cha kuteuliwa tu!
Na lift Jana mkulu kampa ktk gari yake
 

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,087
2,000
Wee jamaa ni mjingga sana,
Unaonekana wewe ni pacha wa Makonda? Kweli mikesha ya mwenge imetuachia majanga makubwa kitaifa.
unastahili kuwekwa unapostahili.
Hapa tatizo ni kichaa kupewa rungu. Ni wapi huko ninapostahili? Na wewe ni mungu mwingine?
Hivi hujamuelewa kweli nini kamaanisha au umeweka mabonge ya barafu kwenye ubongo wako?
Hebu punguza mhemko ueleze unaelewa nini aliposema Makonda na nanukuu. "mimi nikisimama hapa, amesimama mungu." Je vipi kama angesema, "mimi nikitenda, ametenda mungu."
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,677
2,000
Hili suala ni pana kuliko linavyo onekana
Makonda anatisha kuwaweka watumishi wa umma ndani.
Bila kujali sheria au kufuata taratibu anawatishia kuwaweka ndani

Makonda amemwita mtumishi wa umma kichaa.
Hili ni tusi kwasababu hakuna ushahidi mtumishi huyo ni mgonjwa

Makonda ametumia neno kichaa kama dharau.

Ukiachaa ni maradhi na wapo wengi wameumia, wapo mahospitalini na wengine wanatumia dawa. Leo wanajisikiaje serikali kupitia Makonda inapotoa kauli kama hizi

Hili ni tatizo la kiafya na kuawanyanyapaa ni kosa kubwa kiutumishi

Vyama vya wafanyakazi

Hatujasikia vikikemea tabia ya wanasiasa kuwaweka ndani watumishi bila kufuata taratibu

Hatuvisikii vikikemea tabia ya watumishi kudharauliwa na kudhalilishwa hadharani.

Kwavile Rais ni mtumishi namba moja , ndiye mwajiri mkuu wa Makonda na afisa ardhi, ni wakati tusikie kauli yake

Vyama vya wafanyakazi mkikaa kimya ni hili la Makonda, basi msijesikika tena mkikemea jingine hata kama wafanyakazi wataanza kuchapwa viboko achilia mbali kuwekwa sero kwa sababu zinazotokana na utumishi

Makonda, atoke hadharani na kumsafisha afisa ardhi si kwa matatizo bali kwa tusi

Kama hatafanya, tutajiuliza nani mwenye tatizo kati ya kichaa na anayetukana kichaa!

Hili ni baya sana na hakika linaitia serikali aibu kubwa sana

Huyu ni mwakilishi wa Rais ngazi ya mkoa!

Hii ndiyo nidhamu ya kazi tunayoambiwa kila siku?
 

lamosai langasani

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
229
500
Just imagine huyo mjane aliyebadilishiwa umiliki wake ni dada yako au mama yako na viongozi wapo.mimi sijaona kosa la mkuu wa mkoa.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,677
2,000
Just imagine huyo mjane aliyebadilishiwa umiliki wake ni dada yako au mama yako na viongozi wapo.mimi sijaona kosa la mkuu wa mkoa.
Hatuongelei tatizo lililopo kwasababu hatuna information za kutosha

Pili, matatizo makubwa kama ya huyo mjane yanatatuliwa ofisini kwa kutoa fursa za maelezo na ushahidi wa kutosha kutoka pande zote, si karipio mikutanoni

Tatu, sheria za utumishi zipo na ndizo zilipaswa kumuongoza Makonda wakati amesimama na Mola muumba pamoja

Nne, Makonda hawezi kumtukana mtumishi wa umma kichaa bila uthibitisho wa daktari

Kama aligundua mtumishi ni kichaa, alipaswa kuchukua hatua za kumsaidia katika matibabu na ajira na si kutukana jamii nzima ya wagonjwa wa akili

Tano, Makonda hana mamlaka ya kuwaweka watu ndani kwasababu tu ni RC.

Kuna kanuni na sheria za utumishi zinazoweza kumfikisha mtuhumiwa mahabusu na kisha mahakamani , si mayowe ya mikutano ya hadhara

Sita, Makonda naposimama na Mungu kisha kuporomosha mitusi ni kauli yenye maudhi sana kwa jamii
 

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,638
2,000
Mungu anaona. Labda ndio maana anachungulia mara ukatholilikini, mara kwa upako, mara msikitini, mara uhindini kwa mabuda et al. mpaka amekuwa ndiye mungu mwenyewe, Japo hata Yesu yule mwanae hakuthubutu kusema hayo.
 

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,638
2,000
Mungu anaona. Labda ndio maana anachungulia mara ukatholilikini, mara kwa upako, mara msikitini, mara uhindini kwa mabuda et al. mpaka amekuwa ndiye mungu mwenyewe, Japo hata Yesu yule mwanae hakuthubutu kusema hayo.
 

SAMORE

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
344
500
*Tangazo tangazo tangazo*

*mwenye gari namba*
*T 2016 JPM* *akalisogeze watu wanashindwa kufanya mambo yao*
 

Alfan issa

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,153
2,000
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
Kweli kabisa, maana hawana sera waminywea wanaanza kucngizia et ni mngu wabongo bwana
 

Alfan issa

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,153
2,000
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
Mkiambiwa ukweli mnakuwa, wakali wee utamnanishaje na mngu
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,486
2,000
~~~>>>Hawa watu wa ardhi wamekuwa chanzo cha Migogoro mingi ktk Jamii.......... Halafu yule mama afisa gani wa ardhi asiyejua matatizo ya Jamii anayoihudumia???


~~~~>>>>>Makonda piga kazi, Wanyonge nao watapata fursa ya kufurahia mema ya nchi yao.
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,486
2,000
Huyo mama afisa ardhi inavyoonekana hajui hata lolote hapo
~~~>>>>Huo ndio ukichaa sasa....... Afisa Ardhi hujui matatizo yanayoikumba Jamii unayoihudumia unafanya nini ofisini?????


Hongera sana Makonda, next time tandika makofi hao vichaa........
 

Mzee wa Wima

JF-Expert Member
Mar 20, 2016
541
500
MKUU kwa hapa ilipofikia hakuna jinsi mamlaka hiyo hiyo inayomsifia itamtumbua mda si mrefu.Kaka tulia ni swala la mda tu,kwani hajui MKUU was kaya hana Urafiki wala ushkaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom