Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

mimi-mungu-jpg.441219
Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

=======

Kuna Mnyama mmoja anaitwa KOBE Si kila mtu anamjua yule anayetembea na jumba mgongoni. na mara nyingi anaishi kwenye maji na kando ya maji. Wanyama wengi huwa wanashindwa kumdhuru kwa sababu ana KINGA KUBWA yaani lile jumba gumu alilolibeba huwa anaingiza kichwa chake na Miguu yake na unaweza kubeba ukajua ni takataka hata anapokaribiwa na hatari hujiingiza kati lile jumba lake na adui kama nyoka, ndege nk wasiweze kumpata.

Siku moja Tai si mnamjua tai alivyo na akili? alijua kabisa huyu ni kobe na ni mzima ila kwa ujanja wake amejificha kwa kuwa Tai yule hakuna na mawindo yeyote na baada ya juhudi kubwa za kumla yule kobe kushindikana akasema janja yeke ipo. Alimshika yule kobe juu juu mpaka juu sana mawinguni akamuachia ... Weee yule kobe wangu wangu akadondoka chini juu ya jiwe akapasuka vipande vipande. Basi tai kiulaini akapata lishe yake.

Mkuu wa Mkoa Mungu yupo, tena anakuona. Usije ukafanana naye watu wakakusujudia atafanya kama Tai alivymfanyia Kobe.

Please Obey God!!
Don't be a GOD.
 
Acheni wivu mbona mazuri anayofanya kwenye hiyo mikutano hamsemi

Sent from my HUAWEI Y625-U32 using JamiiForums mobile app
Musa alifanya makubwa ambayo hakuna hata mmoja anae weza fanya na hadi kuongea na mungu lkn hakuwahi kujiita mungu sembuse ma tingo.
 
Jamaa ana akili za ajabu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
tatizo hamkumwelewa kijana mwenzenu, yeye km Makonda anamwamini Mungu anayemwabudu,kwamba popote anaposimama anasimama na MUNGU, kwaiyo siyo topic iyo! tupige kazi mazee tumuache jamaa arekebishe mambo.
 
Kama yeye akisimama mungu amesimama basi mwingine yeyote atakayesimama, shetani ndio atakuwa amesimama!
 
Wakati mwingine napo Makonda asilaumiwe sana kwa lugha chafu alizozitoa,pamoja na kwamba Makonda ana tabia ya kutoa lugha chafu lakini ujasiri wa yule binti wa kumkabiri Makonda bila woga,ulimfanya Makonda kupoteza netiwork na kuongea maneno machafu.
 
kuna link yeyote labda tusome au tuone clip Makonda akijifananisha na Mungu?
Mimi ninayo audio aliyosema hivyo akiwa Kinondoni juzi
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

mimi-mungu-jpg.441219
Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

=======
 
Ngoja nitafute kwana Milion 7 nikipata narudi. Mkiona kimya mjue bado nachanga.
 
Huwezi kutuharibia jukwaa kwa uandishi mbovu, wenye kuharibu lugha yetu adhimu tukuache tuu kisa hatujakulipia ada...
Nilimlipia mimi,usiwe na wasiwasi kumrekebisha maana hata hapa nyumbani anavyoongea anapotosha wadogo zake,Hana adabu na lugha ya Taifa
 
Halafu "nasikia" jana Mh Makonda alipewa 'lifti' na Rais wakati wanatoka airport. Inapokuja suala la kuchunga kauli hata aliyemteua pia anayo 'shida' hiyo hiyo.:D:D

Kwa hivyo, with due respect, mnaotegemea achukuliwe hatua pengine ndio inabidi "mpimwe akili" maana kesi ya ndedere ('kuhusu wizi wa mahindi') mnampelekea hakimu nyani ('na yeye huwa anaiba').....
 
PALE MWANADAMU ANAPO SAHAU NA KUJIKWEZA NA KUJIWEKA MAHALA SAWA NA MUNGU.

".., Umefuata nini hapa...., sasa nakuuliza unashanga shanga nini!? umefuata nini kwenye mkutano wangu kama hauna majibu...., sasa kilichokupa 'microphone' ni kipi wakati hauna majibu.., Hawa ndiyo vichaa tunaohangaika nao..., hebu toka hapa..,"

"..., msinijaribu.., Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama unanisikia, hauna wa kukutetea.., "

- Paul Makonda (RC), Dar es salaam.
Hata Mungu muumba wake hawezi kumtetea?No pls mheshimiwa Rc Count your word brother,you can fool people sometimes but not all the time
 
Nadhani tumetafsiri vibaya kauli ya Makonda. Kwa nilivyoitazama Mimi alidhamiria kuonesha kazi anayoifanya ya kutetea wanyonge hata Mungu anaifurahia hivyo anaposimama Makonda Mungu anakua upande wake. Sasa mlitaka aseme akisimama na shetani amesimama?.......Nani amemfuata Makonda ili atoe ufafanuzi juu ya kauli yake ? Acheni kumtoa kwenye hoja za msingi anazowasaidia wanyonge ili ajibu hoja mfu za kurudisha nyuma
 
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
 
Back
Top Bottom