Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?


Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,213
Points
2,000
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,213 2,000
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

=======
Wana JF, Nimejaribu kuifanyia analysis/ kuichambua kwa MAKINI kauli ya RC Makonda akimjibu yule afisa wa Ardhi na kupata yafuatayo.

1. Mkuu wa Mkoa alikuwa tayari na FACTS/Ukweli kuhusu maafisa wa ardhi kusuasua katika utendaji wao wa kazi na kuumiza wananchi!

2.ALIINUA sauti yake KIDOGO akitaka apate MAELEZO SAHIHI kutoka kwa yule mama afisa wa Ardhi.

Lakini naye akajibu kwa KUZUNGUKA ZUNGUKA jambo lililomuudhi Mkuu wa Mkoa.
Maana kama afisa wa Ardhi ni LAZIMA AJUE matatizo SUGU ya ardhi hasa YALIYOKAA miaka mingi bila KUSHUGHULIKIWA!

Hivyo alihitaji jibu lililojaa maadili na UKWELI!

3.TATIZO la mama MJANE kuzungushwa zungushwa na mafisa wa Ardhi kwa MIAKA mingi akitaka HAKI yake ndo kulimfanya makonda atumie neno

"Nikisimama nasimamia MUNGU"
ukii analyze hiyo sentensi ina maana "Nikisimama NASIMAMIA KWELI ya Mungu"
Tukumbuke jamani kuwa Mungu ni Mungu wa WAJANE
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
86,620
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
86,620 2,000
Jamaa ana akili za ajabu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
 
DEOD 360

DEOD 360

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Messages
2,627
Points
2,000
DEOD 360

DEOD 360

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2016
2,627 2,000
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
28,775
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
28,775 2,000
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
 
J

Jozi 1

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Messages
5,986
Points
2,000
J

Jozi 1

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2015
5,986 2,000
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
 
DEOD 360

DEOD 360

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Messages
2,627
Points
2,000
DEOD 360

DEOD 360

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2016
2,627 2,000
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
Tusifundishane kuandika maana ukunilipia ada yote kwa yote kama unaamini ndio Mungu basi
 
G

Getang'wan

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Messages
1,678
Points
2,000
G

Getang'wan

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2015
1,678 2,000
Jamaa ana akili mbovu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
Subirini tu kanusho. Atasema siyo yeye, na kama ni yeye hajayatamka hayo.....
 
Slim5

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Messages
21,461
Points
2,000
Slim5

Slim5

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2014
21,461 2,000
Aina yako ya uandishi inaonyesha kiwango cha ukomavu wako kiumri na kiakili.
Hili ni jukwaa lenye watu wazima wengi usiandike hayo mambo yenu ya "cliac"= serious; "kutafacli" kutafakari n.k
Haya tueleze wewe uliyaza nje ya box umepambanua nini huko?
Achana nae, ndio wale wale. Hata gharama ya mlo mmoja haijui!
 

Forum statistics

Threads 1,284,955
Members 494,371
Posts 30,845,946
Top