Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

makufuli

JF-Expert Member
Jun 18, 2016
428
500
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
Umecha-(kazwa)
 
kadeti

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
738
500
Huyu atapinda huo mdomo kama Seif Khatib siku sio nyingi

Ila mbona kama nimemuelewa Makonda ,Alisema mimi nikisamama mahali Mungu amesimama ,yaani kwamba alipo yeye Mungu yupo naye au mimi ndio sielewi ?

Hakuna sekta ilikuwa imeoza kama ardhi ,alitakiwa awatie vibao kabisa hao washenzi
upo sahii sana mkuu tatizo watu wanapiliza mihemko
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?
=======
Wote ni miungu!

Please remember this, the spirit of a person/leader creates and permeates the atmosphere of his/her influence. So you can trace the exact roots to His Majesty who resides under the sun!
 
wigo

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
917
500
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
Makonda (Salalah Allah wasalaam)
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,087
2,000
Mkuu HATUJUANI wala sijawahi kukutana naye.
Bali naangalia mambo kwa MAPANA na MAREFU! Kama wewe!
Ama hujasikiliza maneno aliyoyatamka Makonda kwa lugha ya Kiswahili au huna uwezo wa kuelewa. Watu kama wewe wasio na uwezo wa kuelewa jambo wapo wengi tu na sababu ziko nyingi zilizowasababishia tatizo hilo. Tafuta msaada haraka na kama utakuwa hujachelewa tatizo lako linaweza kushughulikiwa ukapona kabisa. Kwa ukumbusho tu haya ndiyo maneno ya huyo Makonda na nitakuomba uyasome tena...

Makonda: Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama ...kichaa...unanisikia, hauna wa kukutetea...
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,677
2,000
Kuna watu wanataka tuamini Makonda alichofanya ni sahihi

Hapana, si sahihi na si mara ya kwanza. Kumwita mtumishi kichaa ni dharau na dhalili

Utumishi wa una taratibu zake, na wala si kusimama na kuropoka au kukaripia watu

Alichotaka Makonda ni kiki tu ya kwamba anatatua kero za wananchi bila kujali madhara

Ukimsikiliza yule mama anaonekana kukasirishwa, na wafanyakazi wanachoshwa

Huwezi kutukana mbele ya kadamnasi,uliyetukana usiwe mwendawazimu!!

Makonda huyu tunaona ajabu gani ikiwa ndiye aliyeongoza ''genge' kwenda kumfanyia vurugu Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri mkuu mstaafu pale ubungo plaza?

Alikuwa na 'gati', seuse afisa ardhi!

Wengine tulihoji hata U-DC alipataje achilia mbali RC.

Makonda ana reflect aina ya uongozi.

Fikiria waliompa nafasi hawashtushwi na matendo ya Makonda kama kuamuru Polisi wapige, na sasa kutukana watumishi.

Hivi wanapokaa pamoja huko wanatuonaje sisi wananchi?

Hili la Makonda linakwenda mbali na kutueleza mengi, hasa wenye dhamana
 
SassyS

Member
Nov 15, 2016
46
125
It's a Freudian slip. Madaraka yamempanda kichwani, anadhani yeye ni Mungu. Akisema kuwa, huwa!

Bwana Yule alitangaza Tanzania nzima kuwa kamuota Makonda usingizini, ndio akampa cheo.
Who does that? Let alone a president!
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,087
2,000
Wote ni miungu!

Please remember this, the spirit of a person/leader creates and permeates the atmosphere of his/her influence. So you can trace the exact roots to His Majesty who resides under the sun!
Ndio sababu yangu ya kuuliza hivi; akisimama Makonda kasimama mungu, je akisimama Magufuli? Wote wawili tunaelewa hawajaribiwi na wameonya sana kuhusu hilo. Ukweli pia ni kwamba hawalingani kwani moja alichaguliwa na mwingine kuteuliwa...sasa kama aliyeteuliwa akisimama mungu kasimama, je mteuzi akisimama? Lakini ukweli mchungu zaidi kwangu ni ukimya wa mteuzi kauli hovyo za kufuru kama hizi zinapotolewa.
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,822
2,000
Mag3
Mbona unakuwa too personal na kuanza kunimwagia hasira zako nyingi as if kichwa changu hakiko sawa?
Mimi na wewe hatukuweko wakati matamshi hayo yanayodaiwa kutamk.
Na kama aliteleza katika kutozi meneji emotions zake hapo ndo tuzungumze.

Wewe pia ni kiongozi IN YOUR OWN RIGHT.
Lakini umenishushia na kusema "Watu kama SISI tuchughulikiwe kichwani na tutapona". Surely hiyo si sentensi ya mada bali ni ya shari!

Tayari UMESHINDWA kutawala emotions zako. Hivyo basi hata WEWE unahitaji msaada mkubwa badala ya KUMLAUMU Makonda!
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,677
2,000
Mag3
Mimi na wewe hatukuweko wakati matamshi hayo yanayodaiwa kutamk.
Na kama aliteleza katika kutozi meneji emotions zake hapo ndo tuzungumze.
Video ipo hapo, makundi ya jamii yameonyesha kukasirishwa, leo unataka tuamini hakusema! please

Hii kauli ya kuteleza si kweli. Haiwezekani Makonda ateleze kila siku. Tumekupa historia yake katika utumishi. Kuanzia akiwa Chipukizi, akaja kwa Lowassa, akaenda kwa Warioba, akarudi kwa Polisi kupiga tu atajibu, akahamia kwa Kamanda na 5M, na sasa watumishi.

Kila siku anateleza tu na mnadhani ni bahati mbaya. Kuteleza gani huku?

Kama RC hajui taratibu za utumishi, tumwache tu ateleze kila siku.
Hapana! tutasema hata kama watamwacha katika nafasi hiyo. Hili limepita mipaka

Makonda alikuwa na fursa ya kuwaita watumishi kwa vielelezo na kutolea maamuzi ofisini si kwenda katika mikutano na kuanza kurusha kashfa kwa viongozi wenzake

Ipo siku atakwenda hospitali na kuamuru kwanini Daktari hakufanya operesheni , atoe maelezo hata kama mgonjwa ana mafua. Hapana this is too much!

Kinachoshangaza hakuna anayeonekana kushtuka.

Tunasikia kauli za kurudisha nidhamu kazini, hivi kwa kuita watumishi vichaa ndiyo nidhamu tunayoambiwa hiyo

Hakuna anayeshtuka ! hilo ndilo linatisha kuliko matusi ya Makonda kwa watumishi
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,901
2,000
Ama hujasikiliza maneno aliyoyatamka Makonda kwa lugha ya Kiswahili au huna uwezo wa kuelewa. Watu kama wewe wasio na uwezo wa kuelewa jambo wapo wengi tu na sababu ziko nyingi zilizowasababishia tatizo hilo. Tafuta msaada haraka na kama utakuwa hujachelewa tatizo lako linaweza kushughulikiwa ukapona kabisa. Kwa ukumbusho tu haya ndiyo maneno ya huyo Makonda na nitakuomba uyasome tena...

Makonda: Ardhi Kinondoni nitawashughulikia.., hadi mtajuta kuzaliwa..., mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu..., sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama ...kichaa...unanisikia, hauna wa kukutetea...
Nikikumbuka miaka miwili tuu iliyopita ni huyuhuyu ambaye pamoja na kulipwa per diem ya laki tatu kwa siku alikuwa na tuhuma chafu sana za kuiba simu za wajumbe wa kike wa Bunge Maalum la Katiba na akatetewa na issue kupotezwa na Mtu ambaye majuzi tuu baada ya kufariki ndio tunajua kuwa alikuwa baba yake mlezi baada ya kumuokota huko ajuako mwenyewe, basi nashindwa kuzielewa akili za mwanadamu apatapo kawadhifa ka kubebwa anakuwaje.
Huyu jamaa hakuwa mtu wa kutoa kauli za aina hii kama angekuwa anakumbuka asili yake.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
28,745
2,000
Najua Makonda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Najua pia kwamba Rais Magufuli aliyemteua Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, yeye mwenyewe alikatataliwa na wana Dar es Salaam. Sasa Makonda anapowataka wana Dar es Salaam wamtambue kama mungu na kwamba akisimama kuongea nao ni mungu kasimama...je mteuzi mwenyewe akisimama kuongea na wana Dar es Salaam, wamchukulie vipi?

Najua wengi hili jambo mnalichukulia kimatani lakini ukweli ni kwamba kuna aina mbili tu za watu wanaoweza kutoa kauli kama aliyoitoa Makonda. Ama ni mwathirika wa madawa ya kulevya au ni mwathirika wa ugonjwa wa akili. Mtu mwenye akili timamu hawezi kwa namna yoyote ile kutamka maneno aliyotamka Makonda. Hapa yabidi tujiulize kwa nini mpaka dakika hii mteuzi wake hajachukua hatua yoyote kutunusuru raia na kadhia hii?

Najua pia kumetokea si mara moja ama mbili tu Makonda, ameamrisha Jeshi letu la Polisi, kutii amri zake zisizo na uhalali wowote. Bila shaka haya yote yemewezekana kwa sababu Makonda akitamka, mungu katamka. Hii imewajengea wengi taswira kwamba kila anachofanya Makonda kina baraka za aliyemteua ambaye pia ndiye Jemadari Mkuu wa Taifa kikatiba. Sasa kama Makonda ni mungu, Rais Magufuli pia ni moja katika waumini wake?

=======
Wee jamaa ni mjingga sana, unastahili kuwekwa unapostahili. Hivi hujamuelewa kweli nini kamaanisha au umeweka mabonge ya barafu kwenye ubongo wako?
 
majebere

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
4,722
2,000
Huyu makonda ni wa kumtazama tu, hizi kelele zake ni njaa ya uwaziri,llakini mwisho wake ni ukuu wa mkoa tu.
 
Kitimbwisi

Senior Member
Feb 5, 2013
161
225
Wee jamaa ni mjingga sana, unastahili kuwekwa unapostahili. Hivi hujamuelewa kweli nini kamaanisha au umeweka mabonge ya barafu kwenye ubongo wako?
Kwa uwezo wangu mdogo niliojaaliwa na Mwenyezi Mungu,
Wewe kama sio huyu basi tutarajie mwingine ajaye.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,172
2,000
Nikikumbuka miaka miwili tuu iliyopita ni huyuhuyu ambaye pamoja na kulipwa per diem ya laki tatu kwa siku alikuwa na tuhuma chafu sana za kuiba simu za wajumbe wa kike wa Bunge Maalum la Katiba na akatetewa na issue kupotezwa na Mtu ambaye majuzi tuu baada ya kufariki ndio tunajua kuwa alikuwa baba yake mlezi baada ya kumuokota huko ajuako mwenyewe, basi nashindwa kuzielewa akili za mwanadamu apatapo kawadhifa ka kubebwa anakuwaje.
Huyu jamaa hakuwa mtu wa kutoa kauli za aina hii kama angekuwa anakumbuka asili yake.
Mkuu ni swala la muda tu! Wahenga walisema "All power corrupts, and absolute power corrupts absolutely"!!! Kapigiwa simu live na mtukufu Rais juzi kati tayari mapembe yameota anasahau cheo chake ni cha kuteuliwa tu!
 
eddye

Member
Oct 12, 2016
52
95
Watu wengine bwaana sasa na ww kwa akili yako umeichukulia cliac kabisa mpaka umeanza kumtangaza jaribuni kuwaza nje ya box acheni kutafacli kwa mtazamo hasi ujui kuwa ww ndio unaemtangaza kuwa ni mungu
amekosea bwana ht ukiwa nje ya box lzm umtafakari
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,139
2,000
Jamaa ana akili za ajabu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
Soon atachanganyikiwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom