Akina Mama mna maoni gani kuhusu mila za 'Chagulaga'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akina Mama mna maoni gani kuhusu mila za 'Chagulaga'?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 29, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Akina Baba pia muwe huru kuchangia mawazo yenu.

  Date::10/29/2008
  Kikwete atetea mila ya 'chagulaga' kwa vijana kujipatia wachumba
  Na Mwandishi Maalum, Tabora
  Mwananchi

  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametetea mila ya chagulaga kuwa haisababishi wasichana wengi kupata mimba kabla ya wakati, huku akionya dhidi ya vitendo vya viongozi kugeuza mila za watu kuwa adui, na kuziua kwa kisingizio cha kutatua matatizo.

  Chagulaga ni kati ya mila za wenyeji wa mkoa wa Tabora ambayo huhusisha wasichana kujipanga ili kuwapa nafasi wavulana kuwaendea na kuchagua wachumba, lakini mamlaka za mjini hapa zimeichukulia kama moja ya njia zinazoongeza idadi ya wanafunzi wa kike kupata mimba wilayani Uyui.

  "Haya ndiyo maisha ya watu hawa miaka yote" alisema Rais Kikwete wakati akipokea taarifa ya utendaji wa serikali wilayani Uyui iliyoonyesha kuwa wanafunzi wengi hupata mimba kabla ya wakati wao na hivyo kujikuta wakipoteza nafasi ya kuendelea mbele kimasomo.

  "Tusije kugeuza mila za watu kuwa adui na tukaanza kuua mila hizo kwa kisingizio cha kujaribu kutafuta majawabu ya baadhi ya matatizo yanayotukabili," Rais aliwaambia viongozi wa wilaya hiyo juzi asubuhi ikiwa ni siku ya tano ya ziara yake mkoani Tabora.

  "Haya ndio maisha yao ya miaka yote? Hapa mjini watoto wa kike wa shule wanapata mimba na wala hakuna Chagulaga. Tusije tukageuza mila kuwa ndiyo adui. Inawezekana kuwa mila hiyo inawezesha tatizo hilo, lakini ngoma zimekuwepo miaka na miaka, na tatizo la mimba siyo la miaka mingi kiasi hicho.

  "Sote hapa tumecheza ngoma, tena usiku. Ni ngoma tu za kawaida za makabila yetu. Na wale wanaowapa mimba watoto wa shule pengine hata kwenye ngoma hawaji. Inawezekana kabisa kuwa watu wanaowapa mimba watoto hawa ni mizee ambayo hata kwenye ngoma haendi. Na je si kweli kuwa sisi sote tumecheza dansi na disko, na si tulirudi nyumbani salama."

  Rais alisema kuwa ni kweli kwamba tatizo lipo "laakini tulichambue zaidi ili kupata kiini chake cha msingi. Tusije tukaua mila za watu kwa visingizio tu. Hata kwetu kule tunayo mila ya kuchengula, na wala haina madhara ya kimaendeleo".

  Rais Kikwete, ambaye anatokea mkoa wa Pwani unaosifika kwa ngoma za sherehe, alisisitiza kuwa kwa jadi ya Waafrika kupata mimba nje ya ndoa ni aibu kubwa kwa familia yoyote na kwamba suala hilo halihusiani na mila yoyote.

  "Na wala msije kukimbilia kupiga marufuku ngoma za watu, kwa sababu inawezekana kabisa ukasimamisha ngoma, lakini mimba zikaendelea. Kule Chunya (mkoa wa Mbeya) kuna mimba nyingi sana za watoto wa shule kuliko hata hapa, lakini hakuna Chagulaga," alisema Rais Kikwete.

  Awali, mkuu wa wilaya hiyo, Doreen Semali Kisamo alimwambia Rais Kikwete kuwa mila hiyo ya Chagulaga ni moja ya sababu ya mimba nyingi kwa watoto wa kike katika shule za sekondari wilayani humo.

  Lakini alikuwa ameelezwa na viongozi wa wilaya hiyo awali kuwa moja ya sababu za kuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba ni mila za wakazi wa eneo hilo, hasa vijijini, ikiwamo ile ya Chagulaga.

  Akiwa Tabora, Rais Kikwete alisimamisha kwa muda ziara yake Jumapili na kwenda Afrika Kusini kufungua kikao cha 10 cha Bunge la Afrika. Rais alirejea Dar es Salaam Jumatatu jioni na kurudi Tabora juzi asubuhi kuendelea na ziara yake.

  Katika miaka miwili iliyopita, kiasi cha wanafunzi 44 wa kike wilayani humo walipata mimba.

  Pia Rais Kikwete alishtushwa na ongezeko kubwa la watu wilayani humo na kutaka wahusika wa programu ya uzazi wa mpango, maarufu kama "Nyota ya Kijani" kuitupia macho wilaya hiyo.

  Rais alielezwa kuwa ongezeko la watu katika wilaya hiyo kwa njia ya kuzaliana ni wastani wa asilimia 4.8 ikiwa ni kiwango cha juu sana ukilinganisha na cha taifa ambacho ni asilimia 2.8.

  "Hizi ni takwimu si za kawaida. Ongezeko la asilimia 4.8 pengine ni kubwa kuliko katika eneo lolote nchini kwa sababu wastani wa taifa ni asilimia 2.8. Hii ni mara mbili ya wastani wa taifa," alisema Kikwete.

  Baada ya maelekezo hayo ya Rais, mzee mmoja kwenye mkutano huo alimweleza Rais Kikwete kuwa wakazi wa Uyui wanazaana sana kwa sababu "tunakula sana, na tunazaana sana, mkuu".

  Lakini rais akasema: "Hili siyo jambo jema sana. It is striking (linastua). Wastani wa taifa ni asilimia 2.8. Nyota ya kijani lazima iangaze huku."


  Rais pia alionekana kushtushwa na idadi ya mauaji katika wilaya hiyo baada ya kutaarifiwa kuwa watu 34 wameauwa katika miezi sita iliyopita.

  "Kwa nini mauaji ni mengi mno kiasi hiki? Watu 34 katika miezi sita ni wengi sana katika wilaya moja. Wilaya nyingine zinakaa mwaka mzima bila hata kuuawa mtu yoyote."

  Jana asubuhi, Rais Kikwete alitembelea kijiji cha Kigwa ambako aliweka jiwe la msingi kwenye soko jipya la kijiji/mji hicho katika shughuli iliyohudhuriwa na mamia ya watu.

  Akijibu maombi ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kumtaka atoe maagizo ili kijiji hicho kiwe na hadhi ya kata, Rais Kikwete alisema:

  "Kazi yangu si kugawa kata, na wala kata haigawanywi katikati ya kipindi cha uchaguzi. Kwa sababu tukigawa kata katikati ya kipindi cha uchaguzi ni lazima tufanye uchaguzi mpya wa madiwani. Hata hivyo, kugawa kata siyo tatizo, ili mradi tu mfuate taratibu za ugawaji kata."

  Katika kijiji cha mfano cha Milenia cha Mbola, tarafa ya Ilolangula, Rais alikagua miradi inayofanyika chini ya dhana hiyo mpya ya kuendeleza vijiji na kuzungumza na wananchi.

  Rais aliwaambia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho kuwa wakazi wa kijiji Milenia wanaokataa kuchangia magunia mawili ya mahindi kwa ajili ya chakula cha watoto wa shule wa kijiji hicho, wasipewe mbolea ya bure mpaka wametimiza masharti hayo.

  "Nasikia baadhi yetu hamjachangia magunia mawili ya mahindi kutokana na mazao yenu kama yanavyosema masharti ya uzalishaji katika kijiji hiki. Sasa wale wanaokataa kuchangia kama ilivyokubaliwa, wanyimwe mbolea ya bure kuanzia sasa," alisema.

  Moja ya masharti ya misaada ya Milenia kwa kijiji hicho ni wakulima kupewa mbolea ya bure. Mradi huo unafadhiliwa na wafadhili mbali mbali.

  Rais pia aliwaambia wakazi wa kijiji hicho kuthamini elimu kwa watoto wao. "Halitakuwa jambo linalowezekana kuwarithisha watoto wenu fimbo za kuchungia ng'ombe. Bila elimu watoto wenu watapata taabu sana katika miaka ijayo," alisema.

  Kijiji cha Ilolangula ndiko alikozaliwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sure, kuna maamuzi ya viongozi ya ovyo ovyo tena kwa kukurupuka hata nyakati ambapo ni vyema kufanya simple research kabla ya maamuzi.

  Huwa nanyosha kidole kwa wazazi kwanza. Wazazi huu ni ujumbe kwenu: Siku hizi mwalimu hana muda wa kufikiria kumlea mwanao. Motisha ya kumfundisha pia hana - atoe wapi!


   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa vizuri hii mila, labda mtu anielimishe. Wanajipanga halafu unachagua, halafu mnafanye nini? Mnafunga ndoa or?
   
 4. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ni sehemu tu ya Mila,sijui kwa undani sana ila wana jipanga mabint then vidume vinachagua wachumba.
  Ukiichukulia kilahisi unaweza kuona kama jambo moja la kihuni,ila hilo limekuwepo toka tangu na tangu kama sehemu ya kuwakutanisha wasichana na wavulana walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia.
  Ila wazee wa zamani waliheshimu sana kwamab vijana wajuane na ndipo mamabo ya ndoa yafate baadae kwa dhama hizi ni kama kuwaruhusu watoto kujamiian kutokana na maadiri kuporomoka
   
 5. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Haya mambo ya "chagulaga" yako namna hii: Kawaida kwenye maeneo ya vijijini usukumani na unyamwezini huwa kuna ngoma za kitamaduni katika nyakati maalumu na zaidi sana hufanywa kipindi cha mavuno au baada ya mavuno au hata nyakati za sherehe za kijadi. Sasa katika ngoma hizi watu wa rika zote uhudhuria waume kwa wake. Ngoma zinapofikia tamati na mara nyungi huwa nyakati za jioni jua likianza kuchwa, watu huanza kurejea majumbani kwao na katika harakati hizi za kurejea makwao, hutokea mgawanyiko wa kimakundi, vijana wa kike huwa kundi moja wao peke yao na vijana wa kiume pia huwa peke yao, hawa ni vijana ambao bado hawjaoa wala kuolewa. Wakati huo wale wengine watu wazima nao hujiondokea kivyao kwenda nyumbani.

  Sasa huko njiani makundi ya vijana hukaa njiani wakisubiri wasichana wanaorudi nyumbani, na mara vijana wanapowaona kwa mbali basi kila kijana huanza kwanza kujichagulia, kama hivi, yule ni wangu, yule ni wangu n.k.

  Wasichana wakishafika karibu na hawa vijana, ili kuwakwepa huanza kukimbia na vijana nao huanza kuwafukuza kila kijana akimlenga yule wa kwake aliyekwisha jichagulia. Hapo ndo jina "Chagulaga". Kijana akifanikiwa kumkamata binti, basi anambeba anaenda naye kwake na baadaye nadhani ndo mambo ya ndoa huanzia hapo.

  Hii ni kulingana na uelewa wangu wa suala lenyewe, maana mie siyo mkazi wa huko. Suala hili liliwahi kutolewa ufafanuzi BBC na mmoja wa wenyeji wa huko anae elewa mila na desturi za wasukuma na wanyamwezi, na maelezo niliyoyatoa ndo habari yenyewe. Habari ndiyo hiyoooo!!!
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ama kweli, 'chagulaga' ni moja ya mila potofu inayofaa kupingwa kwa nguvu zote kwani haina tofauti na kuhalalisha ubakaji, duh :( !!!
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapo mnasahau kuwa kuna watu wawili weye misimamo na mitazamo inayokinzana kuhusu ngoma. Mkuu wa wilaya tumeambiwa anaitwa Doreen Semali Kisamo, mchaga huyu. Kule kwao ngoma za asili walizipuuzilia mbali tangu zamani, wakachagua nyimbo za "kizungu", ati za kujifunzia kiingereza! Utakuta mtoto wa kichaga anakuja shuleni na daftari la babake la mwaka 1964 lenye nyimbo za kina Jim Reeves, Cliff Richards, na wengine kama hao, huku akiwa hajui wimbo hata mmoja wa kabila lao, maana wamefundishwa kuwa ni za "kishenzi". Sasa huyu mama amekuzwa kuelewa kuwa ngoma ni "ujinga", zinarudisha nyuma maendeleo nk. Kumbe Rais wake, mkwere huyu, ni tofauti. Amekulia katika mazingira ambayo ngoma zimeheshimika, na ameona zikichangia katika kuijenga jamii yake akiwemo yeye mwenyewe, kwa hiyo kwanza hawezi kupuuza au kudharau ngoma, na pili anajisikia vibaya kuona inahusishwa na jambo baya kama hilo la kuwapa mimba watoto wa shule.

  Kwa hiyo hawa viongozi wa wilaya waipokee tu hiyo changamoto, waache kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu. Wafanye utafiti wabaini chanzo cha tatizo badala ya kuliendea kwa "kudhani" tu.
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ngereja,
  Kidogo umepatia ingawa mwisho umeharibu na kuchanganya mila. Waoabeba wasichana begani na kuwaficha kwao ni Watusi (changanya na Wamasaai, Wasomali, Wa-Ethiopia etc). Wasukuma kama wabantu hawana hii tabia.
  Kinachofanyika wakati wasukuma wakianza kucheza ngoma zao (mashindano) ni kuwa kivumbi huwa kinawaka. Miaka hiyoo (kumbuka mwana Malundi) walikuwa wakishindana kwa kutumia madawa na siku ya mwisho wale viongozi au kundi dhaifu walikuwa wanauwawa kimiujiza. Kumbuka Mwana Malundi inasemekana akiwa kachanganyikiwa na ngoma na ulozi, walimuambia kuwa hakuna kuni. Na yeye akasema si miti hiyo mkate? Basi miti yote aliyoinyooshea kidole, ilinyauka palepale.
  Sasa kutokana na hii shughuli kufanywa usiku na mchana, chakula huwa kinapikwa nyumbani na akina mama na kuwaletea NGOSHA pale. Ahhh, enzi hizo na mimi nilishaanza kuwa mzuri sana kwa kusema "Chini Mgongo chini mgongo..." Chakula cha jioni kikiletwa, akina mama nao wanajiunga na kuanza kucheza. Sasa ikifika mida ya saa 18/19 jioni, ghafla akina dada wanaanza kuondoka mmoja mmoja kama vile wanaenda kuchimba dawa. Vijana wakija shituka, wanaona kwa mbali vumbi linatimka na totozi ndiyo zinayoyoma. Basi vijana wanaacha ngoma na kuanza kuwafukuza. Atakayepatwa anasimamishwa na vijana wote na wanamzunguka na kumuwekea mikono kwa juu na kuanza kusema "Chagulaga mwana mayu" yaani "mwana mama chagua". Sasa dada anachofanya huwa ni kunyenyua mkono na kukamata mmoja wapo. Jamaa hupewa dakika tano ya kutongoza. Huwa wanakubaliana siku gani na wapi wakutane kwa maelezo zaidi. Jamaa akishamaliza, wengine humpa dakika kadhaa na kuanza kumfukuza tena. Wakimpata somo linaendelea. Hii itafanyika kila siku wakati ngoma inachezwa. Na huweza cheza hata mwezi mzima. Sasa binti kama katika hao jamaa kuna mmoja kampenda, atakwenda kumsubiri katika eneo walilokubaliana. Hapo ndipo mipango ya ndoa au kuishi pamoja huanza. Mshenga huenda kuuliza ng'ombe wangapi walipwe na sherehe kwa ujumla.
  Ila hiyo ilikuwa ni OLD school. Unaweza kukuta siku hizi hawa New Generation wanamalizana na mtoto hapo hapo. Sasa kama mtoto atakuwa kila siku au kila siku mbili anabwana mmoja, akiupata mdudu kweli NGOSHA watakufa wengi na kuacha NUMBU (viazi vitamu). And this is too sad.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kithuku,
  Si kweli kuwa Wachaga hawana nyimbo. Wana wimbo mmoja tu na huo wanauheshimu kweli. Kwenye kila sherehe wanaimba "Urere Urere, ahhh kwacha ahhh........."
  Ukija kwa Kikwete, kumbuka Wakwere ni Wanyamwezi waliozamnia Bagamoyo na kukataa kurudi Unyamwezini. Sasa hawa jamaa ngoma iko kwenye damu tangu hawajaondoka unyamwezini.
  Nafikiri ukweli uko katikati. Inabidi uchunguzi mzuri ufanyike na suluhisho litoke na ikibidi somo kwa vijana kupitia wazee lifanyika vilevile. Vinginevyo, Tabora hata shule watapiga marufuku kwani huko nako AIDS inaambukizwa.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuiona ngoma hii pale Igunga, Tabora na siyo kweli kwamba wasichana wanajipanga halafu vijana wakiume wanachagua, labda mila hiyo iwe imefanyiwa mabadiliko ili kuendana na wakati. Kunakuwa na ngoma inayochezwa usiku wakati wa ngoma hiyo inayohudhuriwa na vijana wa kiume na wasichana wanaume huwa wanachagua ni yupi katika wasichana waliokuwapo hapo waliyempenda. Baada ya ngoma basi wasichana hukimbia na wavulana huwakimbiza kila mvulana akimkimbiza yule aliyempenda pale ngomani. Nasikia akimkamata huwa anambaka (sina uhakika na hili) na kisha huyo msichana haruhusiwi tena kurudi nyumbani maana kishaharibiwa. Basi hapo wazee wa pande zote hukaa ili kuandaa harusi ya vijana hao. Nadhani kama tuna mnyamwezi/wanyamwezi hapa ukumbini wanaweza kuielezea vizuri zaidi maana ni mila yao.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Bubu Ataka kusema,
  Soma maelezo yangu ya mwanzo. Naona na wewe uechanyanya mila za hawa "Narots???" yaani Watusi, Wasomalia, Wa-Ethiopia, Wachaga?? Etc. Watusi kweli humvizia mtoto na kumfukuza. Ukimkamata na kumbeba hadi kwako basi huyo wako. Pale kwetu alikuwepo mtoto mmoja wa Kitusi, mama yangu weee. Jinga moja likamvizia (na jamaa pia alikuwa mtusi) na likamfukuza mara ya kwanza halikuona kitu. Mara ya pili likawa limejiandaa na kula zoezi la nguvu. Likampata na kumbeba. Baadaye ilikuwa harusi tu na usiku mzima tukawa tunaona wanavyoimba na kucheza "Inka yangu, Ikonyi yangu .... " sijui ndiyo nini?
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Haya maelezo yako yanafanana sana na maelezo ambayo mimi pia nilipewa na wenyeji pale Igunga, Tabora.
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  So far, inaonekana hakuna anaejua.

  Ngereja kaanza "mambo ya chagulaga yako namna hii…" Akatoa habari kama ya kurepu repu hivi, "Kijana akifanikiwa kumkamata binti, basi anambeba anaenda naye kwake na baadaye nadhani ndo mambo ya ndoa huanzia hapo." Tena anasema "hii ni kulingana na uelewa wangu wa suala lenyewe, maana mie siyo mkazi wa huko…" Kwa hiyo hajui. Na baada ya kuonyesha hajui akasema akamalizia "ndo habari yenyewe. Habari ndiyo hiyoooo." Yani sio tu hajui, ila yuko incoherent. Ukishasema "nadhani," "ndio uelewa wangu," huwezi sema habari ndio hiyo. Hajui!!

  Akaja Sikonge, anatueleza ngoma za Wasukuma, tena za enzi hizo. Wakati tunataka kujua kinachoendelea sasa hivi Uyui, Tabora, ambacho local leaders wanasema kinasababisha huku kujamiana jamiana ovyo. Sikonge alichoeleza ni kama ndoa za hiari hiari hivi, hatuelezwi hizo ngono ya ovyo ovyo zinavyotokea. Anasema "hiyo ilikuwa ni OLD school. Unaweza kukuta siku hizi hawa New Generation wanamalizana na mtoto hapo hapo." Kwa hiyo nae hajui.

  Enter Bubu Ataka Kusema:

  Bubu kaanza kwa kusema alikuwepo ngomani Igunga, Tabora. Kaanza kwa kukosoa hadithi za kujipanga mistari. Nikasema, yes, eye witness to history si ndio huyu. Hajakaa sawa akaanza "Nasikia akimkamata huwa anambaka (sina uhakika na hili)" Nikasema ooooh, yale yale! Halafu akamalizia "Nadhani kama tuna mnyamwezi/wanyamwezi hapa ukumbini wanaweza kuielezea vizuri zaidi maana ni mila yao." Nikawa nishaishiwa nguvu tena. Sasa they are going after each other!!

  Lakini mi siwalaumu Ngeleja, Sikonge na Bubu kwa ku purport wanajua chagulaga kumbe wanabahatisha.

  Tatizo ni la hili gazeti. Ilibidi waandishi watueleze ni kwa nini Distric Commisioner amemwambia Kikwete kwamba chagulaga ndio inaleta kujamiana jamiana ovyo. Wasituambie tu Rais alivyopinga. Tupeni ka analysis ka paragraph moja tu, kueleza hii chagulaga ni kwa nini inadhaniwa kuzambaza mimba. How does it work? Kwa nini local government wanafikiri hivyo. Gazeti ilibidi liseme.

  Lakini hawawezi, hatuna press. Angalia jinsi walivyoandika kwamba wilayani Uyui kuna record murder rate ya watu 34 kwa miezi sita. Well, hizo murder za nini hizo, gun violence, wachawi, vita vya ng'ombe, mauaji ya albino, ujambazi, au rape victims wa chagulaga, what is it ? Wameiacha hewani hewani tu. Watu 34 wameuawa, a record rate. Na nini, Ukimwi wa chagulaga?

  Apparently, hakuna anaejua hiyo chagulaga chagulaga ni kitu gani.
   
 14. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2008
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa hii mila ina tofauti gani na ile ya kichaga ya kubeba msichana juu kwa juu nasikia kwenye migomba na kahawa baunsa anabeba mpaka kwako, unambaka halafu ndio tayari harudi kwao umeshaoa, anataka hataki. Kwa sasa sidhani kama hata hawa vijana wa Tabora watakuwa wanachagulaga, nadhani wanasomeshana tu na kuanza.

  Ila simshangai mheshimiwa kusema mila hii ni nzuri hata kama hana data sana ya nini kinafanyika. Katika ngoma za wazaramo, nasikia kama inapigwa karibu na shamba lako basi mwaka huo utakufa njaa maana mihogo yote wataua, shamba ndio hiding place wanaendelea hadi ngoma iishe na hiyo ni wiki nzima.

  Nadhani tufike wakati tuachane na mila zote zinazopelekea katika ngono, hasa kwa hawa vijana. Utata ni pale ambapo mtoto haendi kwenye ngoma na anaona kila kitu katika TV yako nyumbani, uozo mtupu!
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Oct 30, 2008
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sasa hapa rais anaonyesha nidhamu gani kwa viongozi wa serikali?. Kama unamkosoa mkuu wa wilaya juu ya hili mbele ya wananchi kuna atakalolisema akasikilizwa kweli?

  Inanishangaza sana kuona jinsi alivyomakini na mwepesi kutoa maamuzi juu ya vitu visivyo na kichwa wala miguu. wakati mambo ya maana yanayohitaji uamuzi ameyakalia.

  Mheshimiwa mama Doreen sidhani kama alikurupuka tu na kusema chagulaga inachangia mimba ni wazi alishathibitisha na ndio maana akaliona kama moja ya mambo yanayochangia tatizo hilo.

  Inawezekana tusilione hilo kwa kuwa tunaichukulia chagulaga kwa namna tunavyoifahamu tangu zamani ila tukubaliane jamani kuwa mambo yamebadilika katika dunia ya sasa tusitegemee kuwafungia watoto wetu chumbani wakiwa wawili kisha tukute hawajabanjuka, maadili haya hayapotena sasa tunapoashumu hao vijana waliochagulana wanaishia kupanga siku ya kuongea zaidi na kisha kutafuta mshanga bila KUONJANA tunajidanganya.
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mbaya zaidi ana kauli mbiu kuwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, itawezekana wapi iwapo 'Chagulaga' anaitafsiri kama mwendo mdundo?

  Ndio, mdharau mila na desturi za kwao ni sawa na mtumwa, lakini Elimu ni bahari, katika Chagulaga ya miaka hii kuna kila kilicho kinyume na maadili ya haki za binadamu, haki za mtoto wa kike/mwanamke kuchagua, kusoma na kujiendeleza, na kujikinga na ngono zembe inayoweza sababisha mimba na hata magonjwa ya zinaa.

  Ndivyo tulivyo, lakini tunaweza kubadilika, TUKITAKA!
   
 17. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aaaah, kwani JK na Salma lao si moja tu. Si unakumbuka mkewe alivyoshupalia zile Ngoma za Kiswazi za mfalme kuchukua mabikira?

  Nchi inaendeshwa kwa 'chagulaga' na 'ngoma za mafiga matatu hivi sasa.

  Mambo ya Pwani hayo!


  Asha
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ehh, makubwa haya.
  Kumbe kazi ya uandishi ni ngumu sana hasa unapoandika kwenye forum. Mtu anabisha tu bila ya kusoma maelezo kwa ujumla. Nimeeleza waziwazi kuwa hiyo ngoma ya PUVA, huchezwa kwa muda mrefu na wazazi wote huwa wanakuwepo kwenye ngoma, na kaka zao, wajomba nk. Inakuwa ni familia nzima. Hii ngoma huchezwa na WASUKUMA tu yaani watu wa KASKAZINI na sisi WADAKAMA yaani WA KASKAZINI huwa tunakuwa watazamaji (sisi tuna yetu iitwayo Hiari ya Moyo - mwamkumbuka MWINAMILA??). Siku moja nusura jamaa (Mdakama) apigwe kwani alivamia mduara wa Chagulaga na binti akamshika mkono wake.
  Kumbukeni kuwa hii hufanywa kwenye ngoma tu na ni wakati wa summer au tuseme wakishavuna. Kipindi chote cha masika huwa wako busy na kilimo. Wakati wa summer kuna mikusanyiko ya aina nyingi sana ambayo kijana mtongozaji "MJENGI" au "KAJENGI" huwa wanakuwa na fursa za kukutana na mabinti. Wenye kutongoza hutongoza na wenye kutoa hutoa na hapo ndiyo baadaye zinakuwa MIMBA. Huko shuleni hasa hizi secondary za Lowassa ndiyo usiseme. Vijana wanaangalia Video za USA na wao wakitoka hapo ni kula denda kama kazi.
  Hii ngoma hufanyika kweli ila ingelikuwa hivyo, nafikiri kigezo kikubwa ingelikuwa kwamba mara baada ya ngoma, miezi tisa baadaye wasichana wengi huzaa. Unaweza kukuta hawa huzaa hata wakati wa kiangazi, jambo liashirialo kuwa walikamatwa shanga wakati wa Masika, wakati ambao hamna chagulaga.
  Hivi nyie mnafikiri Wasukuma ni kama Wazaramo yaani ngoma mwaka mzima? Wale jamaa wakati wa masika hawana mchezo. Ukisikia ngoma mchana ujue kwamba wamekutana watu wengi, mmoja au wawili wanapiga ngoma na wengine wanalima kwa kufuata mapigo yake. Huanza saa 12 ausubuhi hadi saa 12 jioni na baada ya hapo, sidhani kama hivi Vijengi vinakuwa na hamu ya chagulaga.
  Yes ni tatizo fulani. Ila linachangia kidogo sana. Kuna vitu vingine vya kudhibiti. Watoto waanze kupata masomo jinsi ya kujikinga na maradhi na kuacha ngono nzembe. Kama wanataka kupiga marufuku ngoma ya PUVA inayopelekea jioni kuwa na Chagulaga, basi na shule zao zipigwe marufuku, minada, sherehe za chama na serikali, na kila makusanyiko ya watu ambayo yatasababisha mabinti wawe mbali na wazazi na huko wakabakwa. Na Mkumbuke kuwa kama ukibaka Mwanamke au ukimtorosha, hiyo siyo CHAGULAGA. Chagulaga ni KUCHAGUA MWANAUME. Sasa ukibaka...... kuchagua gani huko? Nafikiri huyu DC kapata maelezo MABOVU kama hayo ya Wanaume wanajipanga na binti anachagua na hapohapo wanamalizana - SI KWELI. Ehh, Tabora hamna mila ya ORGY. Kama hamna uhakika heri wala msiandike. Watu huamini hizo story feki na kuziweka kichwani kuliko ukweli halisi.
   
 19. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mchongoma,
  Mimi nimeelewa kwamba Raisi hakuona au kupewa sababu za kuridhisha kufikiwa uamuzi wa kufuka mila za watu. Akaona ni vyema atoe tahadhari. Mila zinaweza kuboreshwa au sio? (tuna modern Taarabu siku hizi)


  Hata kama hizi ngoma namna vinavyochezwa leo, ni sababu mojawapo inayochangia kungonoana, kuzifuta ni njia ya mkato. Imeshindikana kuboresha?

  .
   
 20. w

  wajinga Senior Member

  #20
  Oct 30, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wachaga wananyimbo nyingi tu na wala sio kama hawana mila zao. Nyimbo maja ambayo nakumbuka sana ilikuwa ya nguvu kazi. ...Thomasi kawambalewayo ire kawamba lumkape matuta iyo matuta mali ya serekali miyo oooh yale ileleleileile mangiyo.
   
Loading...