TEAMO wa AMANIhahahaha...busara za Teamo!
Mwanakijiji asante kwa vina,,,umeniwezesha pia kutambua waliokuwa hawavumi lkn wamo Asprin na Teamo!
Nashukuru mjukuu, tunu kunitunikia,
Wala hauna makuu, babuyo kumsifia,
Na hii nainukuu, badae ntaipitia,
Uzuri ulionao, kama ndege aimbaye.
Anayetunguliwa na babu,,,lol
Nashukuru mjukuu, tunu kunitunikia,
Wala hauna makuu, babuyo kumsifia,
Na hii nainukuu, badae ntaipitia,
Uzuri ulionao, kama ndege aimbaye.
BABU NAOMBA CHANGIA,kwenye hili umenigusa
KWENYE HII TASINIA,hakika umebobea
KWAKO SIFA NAZIMWAGA,hakika umebobea
ANGALIZO WAZI NAWEKA,wiselady uniachie
KAMA LOVE NI KUSAFA,walau sasa nitulie
BABU HUYO MTU ACHA,tena usichakachue
ANGALIZO NAWEKA WAZI,wiselady uniachie
Sijawahi kusikia, ndege kuwa akilia,
Ndege zake kuimbia, hakuna kulialia,
Mtini akitulia, sauti nzuri atoa,
Mandege yanayolia, hayo mandege haramu.
Kikaa zake mtini, ndege kwa raha huimba,
Sauti toka kooni, na machoye kayafumba,
Miguu shika tawini, hakika Mungu kaumba,
Vindege vinavyoimba, hakika ndivyo vya kula.
Skulimeti,
Kumbe yule mwalimu wa Kiswahili (Mrs. Malisa?) ulikuwa unampata vizuri? Duh sikujua kama kwenye mashairi nako upo!!!
Wakiiji zangu salamu,nikushukuru kwa hili
Nami nishike yangu kalamu, niseme moja mawili
Umesema yalo adimu, yenye mwanga kandili
Milio mingine feki, usivutike sauti
Kuna videge vizushi,kama kunguru mwangapwani
Vyashika wako utashi, Kwa milio vikighani
Sauti zao chekeshi,weza hisi umewini
Mioyo yao beleshi,utachotwa masikini.
Kuna vingine vidogo, vyafanana na shomoro
Vyapatikana ugogo, sauti zao si kero
Ila vipe tu kisogo, vyatunguliwa kwa jero
Hivi angalau kidogo, Anajua kaka Melo
Na kuna makorobindo, ya zamani sio leo
Sauti zao kishindo, yamekwepa makombeo
Manati kwao msondo, labda uje na komeo
Niliyaona Kibondo, kwa kaka Batolomeo
Duh! Kuna vichokoriko,Hivi kula kwangu mwiko
Vinalia dikodiko, Lakini,mmh! mevipiga kiwiko
Tatizo lao chereko,shebedua na vicheko
Hawa kwangu mwiko!
Kuna ndege sisubiri, alie wala acheke
Mhozo-habeshi nikiri, huyu hana makeke
Kazidi makhirikhiri,machejo na pozi zake.
Huyu mtini simtungui, Nampandia namchukua!!
Hahahaaaaaa, Nicheke mie!!!!Kikaa zake mtini, ndege kwa raha huimba,
Sauti toka kooni, na machoye kayafumba,
Miguu shika tawini, hakika Mungu kaumba,
Vindege vinavyoimba, hakika ndivyo vya kula.
Hahahaaaaaa, Nicheke mie!!!!
Vindege vinavyoimba, ujue vimeachishwa,
vipo pia viliavyo, havijaota mabawa
Kulia sio kwa Bundi, Na wao pia huimba
Bali kwa ndege Wachanga, Kulia kwao ni jadi
Kidege kinachoimba, Jua kimeshakomaa.
Msaada tutani ,hapo iyo ndio nini?Mwanakijiji kaopoa kunguru imekuwa tabu mtaani, jee angepata ziwarde!
Huyo ndege analia, machozi yake liona?
Ndege hajui kulia, mimi sijapata ona,
Ukimuona kilia, hiyo yako laana,
Ndege huyo ndege gani, anayelia mtini?