Akilia sana, karibu kutunguliwa...!

Ndugu yangu klorokwini, ndege ulojipatia,
Usimtupe shimoni, ndege asije kulia,
Ahsante kwa shukurani, sisi ni ndugu sawia,
Ila usije sahau, zuri kula na nduguyo.

Ndege huyo maridadi, kama ulivomsifu,
Asipigwe na baridi, wala kung'atwa siafu,
Kumtuna huna budi, Asije kupata ufu,
Msiba wake mkubwa, kufiwa na ndege wako.

Kaa naye kwa makini, haja kumtimizia,
Asijeshinda bandani, njaa kumuumizia,
Chakula alie ndani, siyo chini kumwekea,
Ndege akinona nona, ndo utamu utapata.

Hii ndo JF bwana!
 
Malenga merudi tena, nimeshindwa vumilia
Magulu amenibana,kwa bata kumsifia
Mefikiri toka jana, machache nitatupia
Bata ndege mtamu,sitochoka msifia

Shingo ndefu ya bukini, sitochoka msifia
Mwendo ka wenda harusini, bata anavyotembea
Kamzidi Jasimini, kwa anayoshebedua
Bata ndege mtamu,sitochoka msifia

Kama kunya anye kuku,Kinya bata kaharisha
Nani hanyi? Kasuku!,au kwele lisha lisha
Kimtokacho sishuku,nyama yake hutobisha
Bata ndege mtamu,sitochoka msifia

Magalumangu sikia, Kaizeri hajajua
Bata mlie kwa bia, Meno lazima tachokoa
Mle tena kwa hisia, hakika tafurahia
Bata,jamani bata mtamu,Kamwe sitomuachia

Washangaa mpakata?, wenzako wamdandia
Pembeni wana kashata,dizeti kumalizia
Bata afaa limbwata, sitojuta kujilia
Bata jamani bata, Khaa!nipeni tena na kesho

Napendaa anavyonyata,Nyumaye namfatia
Ananifanya nadata, Natamani mrukia
Ukinipa Dotinata,Bata nitamchagua
Bata laini bata,Sinikumbushe nitalia


Kadi tamati wa tama, hapa mwisho nafikia
Kwa huba namkumbata, bata wangu si kibua
Kaizer we cheza karata, Tamu ya bata hutojua
Bata uwii bata! Siwezi mkadiria
 
Babu uko vizuri aseee.....

Sante sana Jeneresho, kunipa kubwa nishani,
Ntahifadhi makumbusho, haya ya kwangu moyoni,
Sijazoea mipasho, yangu fani ni kughani,
Ya kumjadili ndege, Hii sababu nyingine.

Ndege tukimjadili, Eliza awe pembeni,
Zingatia maadili, Bia kwa wingi mezani,
Hakuna wa kubadili, mnyama awe mezani,
Sababu tumeipata, kukutana wikiendi.
 
Ndugu yangu klorokwini, ndege ulojipatia,
Usimtupe shimoni, ndege asije kulia,
Ahsante kwa shukurani, sisi ni ndugu sawia,
Ila usije sahau, zuri kula na nduguyo.

Ndege huyo maridadi, kama ulivomsifu,
Asipigwe na baridi, wala kung'atwa siafu,
Kumtuna huna budi, Asije kupata ufu,
Msiba wake mkubwa, kufiwa na ndege wako.

Kaa naye kwa makini, haja kumtimizia,
Asijeshinda bandani, njaa kumuumizia,
Chakula alie ndani, siyo chini kumwekea,
Ndege akinona nona, ndo utamu utapata.

yote nimeyakubali, mistari imetulia
lakini kuna mahali, naomba kukubishia
naomba niwe katili, udugu ulogusia
ndege si wa wawili, hilo wazi nakwambia

kizuri ule na nduguyo, msemo hauko sawia
kheri niitwe mchoyo, kuliko ndege kushea
ndege huyu si kimeo, kila mti kurukia
ana kijumba cha mbao, fensi nimemtilia.

tena natangaza wazi, msije mkaribia
nitatia mtu kitanzi , ndege kimsogelea
hatari ya ovadozi ,klorokwini mwaijua
ndege wangu si ulanzi, kila mtu kujinywea.

hehehe hapa hamna kizuri kula na nduguyo wala babuyo. tutashare sredi za JF tu lakini haka kandege hamna kabisa yaani. tafteni bata la magulumangu mkashee.
 
Nilikuwa ninawaza, kalamu nisiishike,
Nikae kwenye baraza, moja mbili nisishike,
Maguluma kanikwaza, ngoja mic niishike
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Ndio hapa mnambie, kwa nini wampakata?
Tena nidadavulie, ni raha gani wapata?
Ili nami nikimbie, nimsake huyo bata,
Nawauliza malenga, bata anapakatwaje?

Hommie wangu 'Sipirini, hata nawe Klorokwini,
Mwanakijiji Amani, Magulumangu mwiteni,
Aje hapa barazani, aujibu mtihani,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

'Mesikia nimeona, bata yake kuharisha,
Wala sio kunong'ona, hilo usije kubisha
Kumpakata mi naona, hilo jambo la kutisha,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Domo lake lachokoa, vinyesi na konokono,
Alacho ndio atoa, kwani nimpe mkono?
Usije kunizodoa, haya yangu ni maono,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Na Kaizer K. Kaizer (Sauti ya watu)

kuna zawadi yako hapa.
 
Klorokwini, AmaniGK, Magulumangu, Asprin......et al....I will BE BACK....U r hilarious

Halafu Mwanakijiji ako wapi?
 
yote nimeyakubali, mistari imetulia
lakini kuna mahali, naomba kukubishia
naomba niwe katili, udugu ulogusia
ndege si wa wawili, hilo wazi nakwambia

kizuri ule na nduguyo, msemo hauko sawia
kheri niitwe mchoyo, kuliko ndege kushea
ndege huyu si kimeo, kila mti kurukia
ana kijumba cha mbao, fensi nimemtilia.

tena natangaza wazi, msije mkaribia
nitatia mtu kitanzi , ndege kimsogelea
hatari ya ovadozi ,klorokwini mwaijua
ndege wangu si ulanzi, kila mtu kujinywea.

hehehe hapa hamna kizuri kula na nduguyo wala babuyo. tutashare sredi za JF tu lakini haka kandege hamna kabisa yaani. tafteni bata la magulumangu mkashee.

hahahahahahaaaaaa

Kizuri wakatalia
Tena wanipotezea,
Hutaki tena kushea,
Hata kama namezea.

Ndege hutaki kushea,
Manati nilikupea,
Ndege ukamuwindia,
Kisha ukamchukua.

Nduguyo wanikimbia,
Kisa ndege kanogea,
Yani wanipotezea,
Kisa ndege kakolea?

Hebu badili nia,
Undugu vema kushea,
Mapatano kolezea
Kisha sote twalea.
 
Klorokwini, AmaniGK, Magulumangu, Asprin......et al....I will BE BACK....U r hilarious

Halafu Mwanakijiji ako wapi?

Wa kijiji kakimbia,
Na ndege anayelia,
Tumbo limemvimbia
Kibudu amejilia.

Kurudi aogopea,
watu watamchekea,
bundi alijipatia,
Ndege alimdhania.
 
hahahahahahaaaaaa

Kizuri wakatalia
Tena wanipotezea,
Hutaki tena kushea,
Hata kama namezea.

Ndege hutaki kushea,
Manati nilikupea,
Ndege ukamuwindia,
Kisha ukamchukua.

Nduguyo wanikimbia,
Kisa ndege kanogea,
Yani wanipotezea,
Kisa ndege kakolea?

Hebu badili nia,
Undugu vema kushea,
Mapatano kolezea
Kisha sote twalea.

kuna vingi vya kushea
visokuwa na hatia
ndege wapo mia mia
aspirin bana tulia

ndege wangu kimchukua
aweza akakimbia
akajenga mazowea
na kwako akahamia

ndege si wa muamana
hawana hawa dhamana
tam tam akiona
atatoroka mchana

mjadala hapa hapana
lete vyengine vina
kwa ndege kuazimana
suala hili hakuna

ndege wangu sio bundi
kuruka ruka hapendi
ndege huyu si wa lindi
na kwengineko haendi.
 
kuna vingi vya kushea
visokuwa na hatia
ndege wapo mia mia
aspirin bana tulia

ndege wangu kimchukua
aweza akakimbia
akajenga mazowea
na kwako akahamia

ndege si wa muamana
hawana hawa dhamana
tam tam akiona
atatoroka mchana

mjadala hapa hapana
lete vyengine vina
kwa ndege kuazimana
suala hili hakuna

ndege wangu sio bundi
kuruka ruka hapendi
ndege huyu si wa lindi
na kwengineko haendi.

Haikuwa yangu nia,
Ndege kumng'ang'ania,
Nakutaka kuridhia,
Kamwe sitambugia.

Hakika nitamtunza,
hataliwa na mafunza,
Na mengi atajifunza
Hatayapata mauza.

Kwako akisharejea,
Uzoefu kapatia,
Wewe unajimegea,
Kwa raha pia madaha

Ndugu yangu klorokwini
Mimi nduguyo asprini,
Tuko pamoja kundini,
Undugu mpaka damuni.
 
Shairi lanikumbusha wimbo wa Fundi konde:

Nina dume langu, kila siku makeleLle
Likitaka kunipiga lazima linishike manywele
Nami nalibembeleza kwa kulipikia mchele

Dume hili dume gani??
 
Haikuwa yangu nia,
Ndege kumng'ang'ania,
Nakutaka kuridhia,
Kamwe sitambugia.

Hakika nitamtunza,
hataliwa na mafunza,
Na mengi atajifunza
Hatayapata mauza.

Kwako akisharejea,
Uzoefu kapatia,
Wewe unajimegea,
Kwa raha pia madaha

Ndugu yangu klorokwini
Mimi nduguyo asprini,
Tuko pamoja kundini,
Undugu mpaka damuni.

bango umemshikia, ndege wataka kushea
jibaba hebu tulia ,punguza kung'angania
tena ukiendelea, ban nitakupatia
huyu ndege najilia, hakuna cha kugawia

bundi la mwanakijiji, mwenyewe kalikimbia
wekeza hapo mtaji, nadhani ataridhia
mzee kahama mji , bundi lishamzingua
huyu wangu sihitaji, na yeyote kushea

kama lazima kushea, mlete kwanza wa kwako
kama atanikolea , nitafikiri ombi lako
kama akinichengua, kumpata wangu mwiko
ndege huyu kaniuwa, sijui lini maziko

undugu hapa hakuna, wa masika wala vuli
kijana hebu tulizana, siwe kama pilipili
DNA tutaongozana, ikibidi tukasaili
sirejee hili tena , mimi nafunga kauli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom