Akilia sana, karibu kutunguliwa...!

Hahahaaa!! MMM bana, safi sana

Tatizo ni pale

  • Mtego wako unaposhindwa kunasa
  • manati yako inaposhindwa tungua
  • kipasulio chako kinaposhindwa pasua
  • Kikamulio kinapozeheka na kushindwa kukamua
  • Nguvu zinapokuishia na kushindwa kunyanyua
Sipati picha nina kinatokea....bila shaka dege LITAPAA na kupotelea angani
 
Mwanakijiji asante kwa vina,,,umeniwezesha pia kutambua waliokuwa hawavumi lkn wamo Asprin na Teamo!

Nashukuru mjukuu, tunu kunitunikia,
Wala hauna makuu, babuyo kumsifia,
Na hii nainukuu, badae ntaipitia,
Uzuri ulionao, kama ndege aimbaye.
 
Nashukuru mjukuu, tunu kunitunikia,
Wala hauna makuu, babuyo kumsifia,
Na hii nainukuu, badae ntaipitia,
Uzuri ulionao, kama ndege aimbaye.

BABU NAOMBA CHANGIA,kwenye hili umenigusa
KWENYE HII TASINIA,hakika umebobea
KWAKO SIFA NAZIMWAGA,hakika umebobea

ANGALIZO WAZI NAWEKA,wiselady uniachie
KAMA LOVE NI KUSAFA,walau sasa nitulie
BABU HUYO MTU ACHA,tena usichakachue
ANGALIZO NAWEKA WAZI,wiselady uniachie
 
BABU NAOMBA CHANGIA,kwenye hili umenigusa
KWENYE HII TASINIA,hakika umebobea
KWAKO SIFA NAZIMWAGA,hakika umebobea

ANGALIZO WAZI NAWEKA,wiselady uniachie
KAMA LOVE NI KUSAFA,walau sasa nitulie
BABU HUYO MTU ACHA,tena usichakachue
ANGALIZO NAWEKA WAZI,wiselady uniachie

Sasa huyo ndo Teamo sasaa,
Sasa huyo ndo mzee wa amani sasaaaa
sasa huyo ndo the king vile anapendaga kukaba sasaaa,
Sasa huyo ndo baba G mshirikisha familia misosi sasaaa!

Vile anatakaga kukaba Babu vile,
Vile anatakaga kunyang'anya babu vile,
Vile Natakaga kupora Wise lady vile..................
 
maneno unayotumia, si fumbo ninakwambia
neno kama kamua,tumbua na neno pasua
akili inaniambia, ni binti waongelea
Je akijilengesha kicheche, si itabidi nimwache


Funzadume (mwana wa Washawasha)
 
Sijawahi kusikia, ndege kuwa akilia,
Ndege zake kuimbia, hakuna kulialia,
Mtini akitulia, sauti nzuri atoa,
Mandege yanayolia, hayo mandege haramu.

Kikaa zake mtini, ndege kwa raha huimba,
Sauti toka kooni, na machoye kayafumba,
Miguu shika tawini, hakika Mungu kaumba,
Vindege vinavyoimba, hakika ndivyo vya kula.

Skulimeti,

Kumbe yule mwalimu wa Kiswahili (Mrs. Malisa?) ulikuwa unampata vizuri? Duh sikujua kama kwenye mashairi nako upo!!!
 
Skulimeti,

Kumbe yule mwalimu wa Kiswahili (Mrs. Malisa?) ulikuwa unampata vizuri? Duh sikujua kama kwenye mashairi nako upo!!!

Hii comment sijaona sehemu yoyote ulipoandika BIA. Inamaana kwenye ushairi hakuna kupongezana kwa biya?
 
Wakiiji zangu salamu,nikushukuru kwa hili
Nami nishike yangu kalamu, niseme moja mawili
Umesema yalo adimu, yenye mwanga kandili
Milio mingine feki, usivutike sauti

Kuna videge vizushi,kama kunguru mwangapwani
Vyashika wako utashi, Kwa milio vikighani
Sauti zao chekeshi,weza hisi umewini
Mioyo yao beleshi,utachotwa masikini.

Kuna vingine vidogo, vyafanana na shomoro
Vyapatikana ugogo, sauti zao si kero
Ila vipe tu kisogo, vyatunguliwa kwa jero
Hivi angalau kidogo, Anajua kaka Melo


Na kuna makorobindo, ya zamani sio leo
Sauti zao kishindo, yamekwepa makombeo
Manati kwao msondo, labda uje na komeo
Niliyaona Kibondo, kwa kaka Batolomeo


Duh! Kuna vichokoriko,Hivi kula kwangu mwiko
Vinalia dikodiko, Lakini,mmh! mevipiga kiwiko
Tatizo lao chereko,shebedua na vicheko
Hawa kwangu mwiko!

Kuna ndege sisubiri, alie wala acheke
Mhozo-habeshi nikiri, huyu hana makeke
Kazidi makhirikhiri,machejo na pozi zake.
Huyu mtini simtungui, Nampandia namchukua!!
 
Wakiiji zangu salamu,nikushukuru kwa hili
Nami nishike yangu kalamu, niseme moja mawili
Umesema yalo adimu, yenye mwanga kandili
Milio mingine feki, usivutike sauti

Kuna videge vizushi,kama kunguru mwangapwani
Vyashika wako utashi, Kwa milio vikighani
Sauti zao chekeshi,weza hisi umewini
Mioyo yao beleshi,utachotwa masikini.

Kuna vingine vidogo, vyafanana na shomoro
Vyapatikana ugogo, sauti zao si kero
Ila vipe tu kisogo, vyatunguliwa kwa jero
Hivi angalau kidogo, Anajua kaka Melo


Na kuna makorobindo, ya zamani sio leo
Sauti zao kishindo, yamekwepa makombeo
Manati kwao msondo, labda uje na komeo
Niliyaona Kibondo, kwa kaka Batolomeo


Duh! Kuna vichokoriko,Hivi kula kwangu mwiko
Vinalia dikodiko, Lakini,mmh! mevipiga kiwiko
Tatizo lao chereko,shebedua na vicheko
Hawa kwangu mwiko!

Kuna ndege sisubiri, alie wala acheke
Mhozo-habeshi nikiri, huyu hana makeke
Kazidi makhirikhiri,machejo na pozi zake.
Huyu mtini simtungui, Nampandia namchukua!!

JF kuna kila fani aisee dahhh nimechoka
 
Kikaa zake mtini, ndege kwa raha huimba,
Sauti toka kooni, na machoye kayafumba,
Miguu shika tawini, hakika Mungu kaumba,
Vindege vinavyoimba, hakika ndivyo vya kula.
Hahahaaaaaa, Nicheke mie!!!!
Vindege vinavyoimba, ujue vimeachishwa,
vipo pia viliavyo, havijaota mabawa
Kulia sio kwa Bundi, Na wao pia huimba
Bali kwa ndege Wachanga, Kulia kwao ni jadi
Kidege kinachoimba, Jua kimeshakomaa.
 
Da simchezo ,kama vina unajua.
Hata ndege huyo,juwezi kumkosa
Kwa stahili hiyo,male wote tukajifunze ushairi
Ili ndege akijilengesha,tuweze kumtungua,na nyimbo zote atuimbie
 
Hahahaaaaaa, Nicheke mie!!!!
Vindege vinavyoimba, ujue vimeachishwa,
vipo pia viliavyo, havijaota mabawa
Kulia sio kwa Bundi, Na wao pia huimba
Bali kwa ndege Wachanga, Kulia kwao ni jadi
Kidege kinachoimba, Jua kimeshakomaa.

Huyo ndege analia, machozi yake liona?
Ndege hajui kulia, mimi sijapata ona,
Ukimuona kilia, hiyo yako laana,
Ndege huyo ndege gani, anayelia mtini?
 
Huyo ndege analia, machozi yake liona?
Ndege hajui kulia, mimi sijapata ona,
Ukimuona kilia, hiyo yako laana,
Ndege huyo ndege gani, anayelia mtini?

Ndege aliye mtini, hawezi kamwe kulia,
Labda aliye shimoni, hewa imempelea.
Hivi ni sababu gani, machozi hawezi toa?
Ndege aliye mtini, kamwe hawezi kulia.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom