Akili za wanawake bwana!

Unampa siri zako mwanamke shambenga unategemea akutunzie siri?
Hata wanamme mashambenga mbona wapo?

Nna siri nzito zake za ofisini na sijawahi hata mwambia ndugu yangu.

Shambenga duuu? Umenikumbusha mbali hii term micharuko wa zamani waliitwa jina hili.
 
ebana inabidi nihoji kwani kugegeda ka binti mtaani kunaathiri vipi kazi yake mapaka afukuzwe haujaonesha connection hivyo huwez fukuzwa kazi kwa kitu ambacho hakiathiri utendaji wako wa kazi..nashawishika kuona hii ni moja ya stori za kijiweni....
 

Sikubaliani na wewe japo sina uhakika kama hili unalosema ni kweli au vipi?! Na hata kama ni kweli linaapply kwa wangapi?!

Nangoja wataalamu waje watueleze.
 
Hizo ni akili za matope za mwanaume!!!
 
kwa mwanamke kumpa siri za ofisini mumewe ni sawa au?
 
Unampa siri zako mwanamke shambenga unategemea akutunzie siri?
Hata wanamme mashambenga mbona wapo?

Nna siri nzito zake za ofisini na sijawahi hata mwambia ndugu yangu.

Hivi Kongosho siri na umbea kuna tofauti.
 
Kwa kweli hata mimi nashindwa kuwaelewa baadhi ya wanawake, si wavumilivu hata kidogo na sijajua ni kwa nini japo wapo walio wavumilivu si tu katika kutunza siri za nyumbani kwake bali hata katika kutatua baadhi ya migogoro inayowakabili pamoja na wenzi wao. Mfano, utakuta kabinti kakikosana na boy friend wake kanakuja JF kutafuta wanaume eti wa kubadilishana nao mawazo kuhusu mahusiano, lini mwanamke au mdada akabadilishana mawazo na mkaka au mwanaume zaidi ya kutafuta kugegedwa tu?? Wapo pia vijana hatari kwa ajili yao na wakisha kamatwa na hao vijana wanakuja tena JF ooo sikuelewa, oooh Mungu wangu nakadhalika nakadharika.
 

Kuna jamaa alimfuamnia mkewe, akachanganyikiwa. Mwanamke naye kuona hivyo akamtafuta bosi wa mumewe, akatiana nae ana kumpa siri zote za wizi anaofanya mumewe kwenye hiyo kampuni. Jamaa akafukuzwa kazi, ndoa ikafa. Wote wamebaki ma hohe hahe tu. Mwanamke karudi kwako Babati!

Usimmwambie kila kitu mkeo. Wazee wetu wa zamani walihakikisha kuna mipaka katika hili
 
kesi za namna hii ni nyingi ambazo wanawake wanawasemea waume zao makazini hasa wakisikia wana mahusiano ya nje. Kuna mmoja namjua alibeba mpaka documents za ushahidi na kumpelekea boss wa mumewe.
lakini yote nasema ni udhaifu tu wa mtu, madili yako ya wizi unamhusisha mkeo ili iweje?
wapo pia wanaume wenye tabia za namna hii, lakini mara nyingi ni vi boy friend.
hapa ni uwe na akili tu madili yako ni wewe na uliyefanya nae, kwisha!!! hakuna cha mume/mke, ndugu, rafiki au sijui nani kujua.
 
Sikubaliani na wewe japo sina uhakika kama hili unalosema ni kweli au vipi?! Na hata kama ni kweli linaapply kwa wangapi?!

Nangoja wataalamu waje watueleze.

huo ni mtazamo wako wewe lakini wapo wanawake ambao wanataka waume zao wakitoka kazini tu warudi nyumbani muda huo huo. halafu ku-hang out na friends kunawapa watu shule ya maisha...jinsi ya kutafuta au masula ya post za ajira, nk.
 
huo ni mtazamo wako wewe lakini wapo wanawake ambao wanataka waume zao wakitoka kazini tu warudi nyumbani muda huo huo. halafu ku-hang out na friends kunawapa watu shule ya maisha...jinsi ya kutafuta au masula ya post za ajira, nk.

Pekundu hapo ndipo penye mashaka!
Tujaribu kuwa honest tuseme mara ngapi hilo linatokea!? Kampani nyingi baada ya kazi ni pombe na story, bora mume akiwa mfanyabiashara kwa sababu huko baa walau anaweza kupata nafasi ya kutangaza biashara hiyo ni kama anakutana na watu tofauti tofauti ila wengi tunahang na wale wale. Binafsi naona wengi wetu huwa ni pombe tu na stori mbili tatu kuepuka kadhia za hom na wengine wachache madem kiasi!
 
mambo ya hom na ofisin yatenganishwe!ugomv ule ni wakijamii na sio kikaz hivyo hakpaswa kusema.
 

Nadhani haujataka kuwa fair just because mwenye kosa la kusababisha mume kufutwa kazi ni huyo mwanamke. Suala la makosa yenu binafsi eti unapeleka ofisini sidhani kama ni busara kwa kweli no matter what! ! Ningekuwa mimi ndio ningeachana nae kabisa afurahi.
 
Last edited by a moderator:
kweli kabisa kama anaona vipi akaoe mume mwenzie ndie anatumvulia maovu yake.

Dah! Na siku ya wanawake duniani inakaribia ndio mawazo ya baadhi yao mawazo yao yapo hivi sijui tunajenga au tunabomoa.
 
Nakumbuka jamaa anagu alifunguliwa kesi ya kubaka na mke wake! Jamaa aliwekwa ndani kwa wiki 2 hivi. Kamwachia mwanamke kila kitu ameenda kuishi hoteli tu sasa na kunywa kwa sana.
 
Kuna bwana mmoja alikuwa anahusika kutunza nyaraka za ushahidi wa mahakama. Kwa kuhofia kuibiwa kazini, akazibeba akaenda nazo nyumbani pamoja na baadhi ya picha za ushahidi. Akabwaga briefcase nyumbani akaenda kwenye kijiwe cha kahawa. Kurudi anakuta briefcase imepekuliwa na baadhi ya nyaraka hakuna(mkewe hakwenda shule) kabla hajauliza mkewe akaanza kuwaka anamwambia picha za mahawara zako na barua zao zote nimezichoma moto. Mzee alinyong'onyea, akaitisha mkutano wa familia kuwaeleza. Kesho yake anaulizwa kuhusu document hana,unajua tena enzi za mchonga, kibarua kikaota nyasi.
 

Duuu hii kali. hebu tuambie hatima ya huyu mama na mmewe ikawaje?
 
Duuu hii kali. hebu tuambie hatima ya huyu mama na mmewe ikawaje?

Hakumpa talaka wala hakumpa adhabu yoyote kwa sababu mama alijisikia vibaya mno baada ya kufahamu ukweli, na hasa baada ya mzee kuachishwa kazi. Bahati nzuri mzee alikuwa na biashara fulani ambayo alikuwa anafanya part time akaanza kuifanya full time na alifanikiwa mno, akaweza kujenga nyumba nyingine enzi hizo kwa hiyo biashara na mambo yakawa mazuri zaidi. Baada ya hapo akawa anajutia kupoteza muda kwenye kuajiriwa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…