Akili za Manara zimeishia hapa

Simba Mkali

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
620
239
PRINCE JOKES
SIJUI nani alimdanganya akaibuka na kumzodoa Rais wa TFF, Wallace Karia mara baada ya kufungiwa miaka miwili na faini ya Sh 20 milioni.

Najua ulimsikia Haji Sunday Manara alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kufungiwa miaka miwili na faini ya Sh 20 milioni.

Kama ulimsikia utagundua baadhi ya vitu vya msingi, kwamba hakutarajia kama angefungiwa au kupewa adhabu yoyote ile. Manara alikuwa akizungumza akiwa amepaniki au kwa nia ya kumwaga mboga badala ya wenzake kumwaga ugali.

Kumbuka siku chache baada ya kutoka Arusha, Manara na Rais wa Yanga, Engineer Hersi Said walienda kumuona Rais Karia nyumbani kwake. Nini kiliendelea kwenye mazungumzo yao? Baada ya hapo akajua kila kitu kitakuwa kimemalizika.

Kesho yake Manara alizungumza na vyombo vya habari na kumuomba radhi Karia. Hapa alionekana kuwa na busara sana. Hebu tujiulize alimwomba radhi kwa kosa gani?

Katika kumuomba radhi, Rais wa TFF Manara alimwita kaka, alimwita Rais na alimwita majina yote mazuri na kujishusha kwa kukiri kuwa amekosea kubishana hadharani na Rais wa TFF.

Lakini baada ya kufungiwa tu heshima zote alizompa Rais Karia zikatoweka. Unafki wake ukatamalaki mbele ya hadhara.

Baada ya kufungiwa Manara alizungumza mambo mengi ambayo ukiyachunguza kwa makini utagundua hakukua na sababu ya yeye kuyazungumza.

Kumgombanisha Karia na Yanga
Manara alikuwa akitafuta huruma ya mashabiki wa Yanga. Alijua watamwamini kwa kuwa anawajua akili zao zilipoishia. Unakumbuka aliwahi kuwatukana pale aliposema wangapi wenye akili na wangapi hawana.
Na kwa kufanya hivyo alilazimika kumgombanisha Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia na mashabiki wa timu yake ya Yanga.

Manara anasema Julai 2 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid pale Arusha, Karia alimwambia kuwa Yanga wote walikuwa wakitembea na vinyesi makalioni mwao.

Pale jukwaani siku ile kulikuwa na wageni wa heshima wenye hadhi kubwa sana na wenye mapenzi yasiyo na shaka juu ya Klabu ya Yanga kuliko hata Manara.

Alikuwepo Waziri wa Fedha, Mwigulu Mchemba, huyu humwambii kitu kwa Yanga. Anashiriki hata kuwasajili wachezaji. Mfano Fei Toto ni yeye ndiye aliyempeleka Yanga. Alikuwepo Waziri wa Nchi Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Huruma Mkukuchika. Hawa wote wanajulikana kwa mapenzi yao kwa Yanga yasiyokuwa na chembe ya shaka. Karia angeweza kutamka maneno kama hayo mbele yao?

Kumbuka wakati Manara akiwa anatoka Simba na kujiunga na Yanga kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuwaaminisha mashabiki wa timu hiyo kuwa TFF haikuwa na baya kwa Yanga.

Wakati huo mashabiki hao walikuwa hawana na imani na uongozi wa Karia katika shirikisho hilo wakiamini Rais huyo ndiye aliyekuwa akiwapa mafanikio watani wao wa jadi.

Sasa Manara anakula matapishi yake kwa maslahi yake! Imekuwa ni lazima atumie mbinu ya kumgombanisha tena na Karia hili kutafuta huruma ya mashabiki wa Yanga.

Amchonganisha Karia na Serikali
Kama haitoshi, bado Manara amendeleza propaganda zake dhidi ya Karia na kumchonganisha na serikali akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani.

Manara alisema Rais Karia alikuwa akijigamba kwamba baada ya Rais Samia anayefuata ni yeye.
Yaani hapa kati hakuna kiongozi mwingine mwenye nguvu zaidi yake kwa sababu tu anaongoza soka la Tanzania.

Tumia akiri yako kukubali au kukataa jambo hili. Lakini ni vigumu sana kwa Rais Karia kutozitambua mamlaka nyingine baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Manara ni mtu anayeweza kujipendekeza kwa yeyote ilimradi lake litimie. Ameendeleza tabia yake hiyo kwa kujipa unasaba wa Rufiji ili tu kutaka kujiona yeye ni mtu wa karibu na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa.

Akamtaka Mchengerwa asikubaliane na uonevu anaofanyiwa! Manara anadhani anaweza kufanya chochote na kumwamuru yeyote afanye anavyotaka yeye. Anajiona ni mtu special sana hapa Tanzania kuliko mwingine.
Anataka kuonyesha serikali kwamba Karia anazuia mipango yake ya kutaka kuitangaza siku ya Sensa kwa kulitumia Tamasha la Yanga.

“Eti safari hii nilikuwa nimepanga kuja na ujumbe wa Sensa kwenye Tamasha la Yanga. So what?
Nani kamdanganya huyu? Hivi kati yake yeye na yule anayetuma ujumbe wa sensa kwenye simu zetu nani anatangaza vizuri ujumbe huo?

Kuna mambo ambayo, Manara anayazungumza halafu kuna watu wanayaona ni ya maana sana na kumuona ni kama vile anaonewa. Katika mkutano wake alisema tatizo si yeye, bali ni Yanga.

Akaongeza anazuiwa ili asishiriki tamasha la Wiki ya Yanga. Kwa saabu mashabiki wasifike kwa wingi uwanjani na tamasha lidode ili lile la Simba lifanye vizuri. Kweli? Ili tamasha la wiki ya Yanga lisifanye vizuri! Halafu Karia apate nini? TFF ipate nini? Ajabu kwelikweli.

Pamoja na Simba kufanikiwa kujaza watu uwanjani baada ya Manara kuondoka, bado anaamini yeye ndiye aliyeipa mafanikio timu hiyo na kujaza mashabiki uwanjani!

Unakumbuka Yanga bila ya Manara iliwahi kufanya vizuri tamasha lake kuliko lile la Simba na kujaza umati wa kutosha bila ya uwepo wake?

Unakumbuka Manara pamoja na hamasa zake Msimbazi alishindwa kujaza viwanja viwili vya Benjamini Mkapa na Uhuru kwa wakati mmoja wakati wa Simba Day?

Nataka niwaambie kitu kimoja, Manara ndiye anayepata umaarufu kupitia Simba na Yanga wala timu hizo hazinufaiki na yeye.

Ajisafisha kuvuta sigara
Manara alichukizwa na kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, alipozungumzia kuhusu yeye kwenda kwenye kamati hiyo akiwa na pakti la sigara na kibiriti cha gesi.

Nani asiyejua kama Manara anavuta sigara? Tena Embassy au anataka tutaje na kilevi chake kingine? Mbona ameona kama amedharirishwa kwa kuambiwa kuwa alikuwa na vitu hivyo?

Mbona yeye ameendeleza tabia yake ya kuwadhalilisha wenzake? Kwa kudai Karia amesema Yanga wanatembea na kinyesi makalioni.

Mbona amesema Katibu Mkuu wa TFF, Wlifred Kidau alimuomba radhi kwa niaba ya Rais wa TFF? (Kidau amekanusha kufanya hivyo). Lengo lake ni nini kama sio kuwagombanisha viongozi hao?

Ishu la hospitali
Hakuna siri kwamba Manara alitengeneza cheti cha hospitali. Lakini tusiingie kwa undani. Tuachane na hicho kitu. Kitu cha ajabu, alipoambiwa kuhusu kuvuta sigara, alisema anadhalilishwa lakini alipoambiwa hana hadhi ya kwenda kutibiwa Hopsitali ya ndogo kama ye Temeke alisema yeye ni nani asitibiwe kwenye hospitali hiyo.

Manara anapenda sifa na ameshakiri hili hadharani. Lakini hapendi kusifiwa kwa kumkandamiza bali kwa kumsikia kwelikweli. Anaweza kujishusha ukadhani anajishusha kweli. Tunaomjua tunaamini umaarufu wake alioupata tangu utotoni unamlevya vibaya sana.

Manara anaamini anaweza kufanya chochote na kumchafua yeyote lakini yeye hataki kuguswa, hataki kuambiwa ukweli. NI SHIDA.

Wadau walimpigania
Manara hakutakiwa kusema chochote baada ya kufungiwa. Alitakiwa anyamaze kimya na kuacha wadau wampiganie.

Mtu kama Zitto Kabwe alijitokeza hadharani na kumtetea Manara kwa kusema adhabu yake ilikuwa kubwa mno.

Nani asiyejua kama Zitto ni mnyama wa kulialia? Kwanini alimtetea?

Je, kwa upuuzi huu alioufanya baada ya kufungiwa nani anaweza kumtetea tena? Labda mtu mwenye akili kama zake.
 
Ukimya wa TFF sio wa kiboya na Manara kastukia

Wanamsubiria ajichanganye kwenye tamasha la mwananchi ajitokeze kama msemaji waje na kubwa kuliko
 
Manara, Mwijaku, yule sijuj nani lokole, kuna yule sijui nani alisema atamzalia diamond ni watu aina moja, wanawakilisha watanzania weengi.

Hata wanasiasa wetu wengi wapo hivyo, mcheki kigwangalah, wacheki wale waliokuwa wanamuabud anko magu, kisha baada ya umauti wake wamepia u turn moja hatari, kama sio wao vile 😂🤣
 
Manara na yanga ndio contents kwenye soka la bongo.

Kama hauwawezi kuwaandika basi utawasoma tu.
 
Msela mavi kama huyu anataka Rais wa nchi aache kazi zake ajadili wenda wazimu wake !!!!!
JamiiForums-157563313.jpg
Screenshot_20220725-162904.jpg
Screenshot_20220726-102835.jpg


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mada ndeeeefu ya kumponda mtu aliehamasisha sana Simba kupata mashabiki wengi! Kisa kahamia Yanga na upepo wake wa makombe imekuwa shida kubwa huko Kolokoloni FC!
Manara kiukweli ana jina kubwa kwenye mpira wa bongo na Afrika kuliko hata Rais Kolo Karai!
 
Atukane watu sababu aliwapa simba mashabiki. Kwani karia anacheza namba ngapi simba useme amkomoe manara.
 
Mswahili sana yule jamaa..but umeandika vzuri kongole...umeonyesha unaweza kusoma akili za watu
 
Back
Top Bottom