Akili yangu imetekwa na kamari

Akili yangu imetekwa na kamari

Ushauri wangu Uza nyumba , Uza Gari , Acha kazi kama hujaoa Oa au km una mke mmoja Ongeza wapili , ishi miezi sita bila kaz ya maana (Fanya vibarua usiingize zaidi ya 20000 per day) .. Ukiishindwa hapo basi
 
Aaaah! Forex gani inayotoa hela kirahisi namna hiyo. Mtu ambaye hawezi kujizuia kucheza kamari ukimwambia afanye forex trading ni sawa na kumwambia mtu ili asiwe mlevi aache Konyagi anywe K-Vant wakati vyote vilevi.

Sheria ya kwanza kutrade lazima usiwe na tamaa. Yeye anazo maradufu.
Mkuu akifanya forex trading kumbuka lazima atajifunza mbinu ambazo ndio pamoja na kuzuia greed yake yaan sijui unaipata point yangu ni kwamba ukiwa unatrade kuna namna flani trading ina shape maisha yako in a good way ili utengeneze pesa huko lazima kufuata hizo rules ambazo automatically zitambadilisha.
 
Poleni na hekaheka za campaign wana JF.

Moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwathirika wa kamari, nacheza mchezo wa roulette kwa sana kuanzia cassino na popote napokutana na hilo dude.

Nimeajiriwa na kipato changu si haba maana nikichukua mshahara wangu pamoja na ganji nazopata kazini nina uhakika wa kutengeneza zaidi ya milion 5 kwa mwezi. Maana nina uwezo wa kupata kati ya 50,000 hadi laki 300,000 kwa siku hapa inategemea na hali ya siku yenyewe na hii ni pamoja na uchumi wa anko Magu kuwa hivi.

Pamoja na pesa zote hizo pesa pekee nayoweza kuiweka kwenye account ni kati ya laki 5 na m1 tu zingne zote naliwa kwenye ulaibu huu.

Hivyo nikikaaa bila kwenda kwenye kamari miezi 3 hua nafanya maendeleo makubwa.

Bahati mbaya pesa zote hizi zinaishia kwenye kucheza kamari.

Nimejitahidi kujaribu kuacha wapi,nimetembelea wataalamu wa psychology lakini sijaona mafanikio

Nashukuru nimejenga nyumba nzuri ya ndoto yangu pia usafiri wa haja ninao.

Nasikitika kwamba naweza kuwa na m1 asubuhi usiku sina hata pesa ya kuweka mafuta asubuhi.

Binafsi ninapambana kuacha hii kitu lakini sijui nianzie wapi kuacha.

Nishatangaza dau hata kwa mtu anaeweza nisaidia kuacha kamari lakini hakuna msaada.

Natamani nihamie mikoa ambayo hakuna haya madude bahati mbaya kazi yangu haina tawi kwa ofisi nayofanyia kazi.

Ukweli huwa naweza kushinda pesa kubwa tu kwenye hii kamari hata m10 kwa siku lakini inakuchukua hata siku 5 unapewa kipigo tena!

Mnaweza kunipa mawazo yenu wana jukwaa?

Nawasilisha.
njoo inbox
 
Unashindwa nini kuwekeza kwenye miradi midogo kila baada ya muda flani. Kila mwezi ukiwekeza kwenye mradi wa M moja na mwezi ufatao unaongeza mtaji au unafungua mradi mwingine utatunza hela, utarudisha hela, utapata faida na utakuwa na hela kwenye mzunguko.

Inaonekana huna uwezo wowote wa kuanzisha biashara kwa kuwa umezoea hela za ganji. Na wakati huo huna uwezo wa kusimamia. Wacheza kamari hawajawahi kujua kusimamia chochote, ona hata wewe hujui kutoka gambling.

Weka mtu kisha mpe mandate, yeye arejeshe kiasi kadhaa kwa muda flani. Wewe endelea na kulewa, wanawake na bata za ovyo. Najua haya hayakwepeki kwa gamblers. Mwisho nalenga kukwambia acha hizo mambo.
Sio kama sina uwezo wa kuwekeza,nina biashara pia zaidi ya 1 tena zinatengeneza pesa pia...

Hoja yangu kubwa ni kwamba kamari inaniendesha,nikiwa na gape hata la nusu saa naendq kucheza..

Mpaka natoroka job
 
Wenzako wenye uraibu na hizo kamari huwa wanakabidhi funguo za gari zao mezani. Wanarudi nyumbani na kirikuu ya kubeba friji na sofa ili kuziuza kupata hela ya kuchezea kamari tena ili kurudisha gari. Nayo inapigwa tena, bhas nyumba ndio unafatia inauzwa kidogo kidogo..sasa wewe bado muoga kwenye kamari kabisa hujafikia uraibu.
Sijafikia huko kwa sasa,Mungu anisaidie
 
Bila shaka kutakuwa pia na nguvu ya ziada kutoka kwa Ibilisi inayokusukuma kufanya jambo hilo. Nenda kaombewe kwa Jina la Yesu Kristo haraka sana kabla hali haijawa mbaya na ukajikuta unafilisika kabisa.
Amina.
 
Poleni na hekaheka za campaign wana JF.

Moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwathirika wa kamari, nacheza mchezo wa roulette kwa sana kuanzia cassino na popote napokutana na hilo dude.

Nimeajiriwa na kipato changu si haba maana nikichukua mshahara wangu pamoja na ganji nazopata kazini nina uhakika wa kutengeneza zaidi ya milion 5 kwa mwezi. Maana nina uwezo wa kupata kati ya 50,000 hadi laki 300,000 kwa siku hapa inategemea na hali ya siku yenyewe na hii ni pamoja na uchumi wa anko Magu kuwa hivi.

Pamoja na pesa zote hizo pesa pekee nayoweza kuiweka kwenye account ni kati ya laki 5 na m1 tu zingne zote naliwa kwenye ulaibu huu.

Hivyo nikikaaa bila kwenda kwenye kamari miezi 3 hua nafanya maendeleo makubwa.

Bahati mbaya pesa zote hizi zinaishia kwenye kucheza kamari.

Nimejitahidi kujaribu kuacha wapi,nimetembelea wataalamu wa psychology lakini sijaona mafanikio

Nashukuru nimejenga nyumba nzuri ya ndoto yangu pia usafiri wa haja ninao.

Nasikitika kwamba naweza kuwa na m1 asubuhi usiku sina hata pesa ya kuweka mafuta asubuhi.

Binafsi ninapambana kuacha hii kitu lakini sijui nianzie wapi kuacha.

Nishatangaza dau hata kwa mtu anaeweza nisaidia kuacha kamari lakini hakuna msaada.

Natamani nihamie mikoa ambayo hakuna haya madude bahati mbaya kazi yangu haina tawi kwa ofisi nayofanyia kazi.

Ukweli huwa naweza kushinda pesa kubwa tu kwenye hii kamari hata m10 kwa siku lakini inakuchukua hata siku 5 unapewa kipigo tena!

Mnaweza kunipa mawazo yenu wana jukwaa?

Nawasilisha.

Dawa ya moto ni moto, wewe endelea kucheza tu kamari usiache.
 
Ushauri wangu Uza nyumba , Uza Gari , Acha kazi kama hujaoa Oa au km una mke mmoja Ongeza wapili , ishi miezi sita bila kaz ya maana (Fanya vibarua usiingize zaidi ya 20000 per day) .. Ukiishindwa hapo basi
Sijafikia huko
 
mkuuuu pole sana beti mpira,kila siku najitolea bule kukutengenezea od ya 1.10 ili ushinde laki kila siku
Dakika 90 zote nasubiri tu

Wakati roulette sec 33 tu dakika 2 naingizq pesa au nasafishwa
 
Minashauri ufunge na kusali...ukimuomba Mungu wako akunyofoe katika hu uraibu. Addiction Ni mbaya Sana na inaendelea kukua JINSI unavyoendelea kucheza.

Kama una Dini na unamuamini Mungu jaribu kumshirikisha na Kumuomba kwa kumaanisha.

POLE SANA MKUU
 
Mkuu nadhani hela unazokulaa na unazoliwa zinataka kufanana..!! Ukiliwaa pesa tu bila kulaa hata miaa mfululizoo nadhanii utaacha tu mwenyewe.. Me mshahara wangu huwa natoa 20k tu ikiliwaa naacha jumla
 
Back
Top Bottom