Akili yangu imetekwa na kamari

Nautico

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
341
780
Poleni na hekaheka za campaign wana JF.

Moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwathirika wa kamari, nacheza mchezo wa roulette kwa sana kuanzia cassino na popote napokutana na hilo dude.

Nimeajiriwa na kipato changu si haba maana nikichukua mshahara wangu pamoja na ganji nazopata kazini nina uhakika wa kutengeneza zaidi ya milion 5 kwa mwezi. Maana nina uwezo wa kupata kati ya 50,000 hadi laki 300,000 kwa siku hapa inategemea na hali ya siku yenyewe na hii ni pamoja na uchumi wa anko Magu kuwa hivi.

Pamoja na pesa zote hizo pesa pekee nayoweza kuiweka kwenye account ni kati ya laki 5 na m1 tu zingne zote naliwa kwenye ulaibu huu.

Hivyo nikikaaa bila kwenda kwenye kamari miezi 3 hua nafanya maendeleo makubwa.

Bahati mbaya pesa zote hizi zinaishia kwenye kucheza kamari.

Nimejitahidi kujaribu kuacha wapi,nimetembelea wataalamu wa psychology lakini sijaona mafanikio

Nashukuru nimejenga nyumba nzuri ya ndoto yangu pia usafiri wa haja ninao.

Nasikitika kwamba naweza kuwa na m1 asubuhi usiku sina hata pesa ya kuweka mafuta asubuhi.

Binafsi ninapambana kuacha hii kitu lakini sijui nianzie wapi kuacha.

Nishatangaza dau hata kwa mtu anaeweza nisaidia kuacha kamari lakini hakuna msaada.

Natamani nihamie mikoa ambayo hakuna haya madude bahati mbaya kazi yangu haina tawi kwa ofisi nayofanyia kazi.

Ukweli huwa naweza kushinda pesa kubwa tu kwenye hii kamari hata m10 kwa siku lakini inakuchukua hata siku 5 unapewa kipigo tena!

Mnaweza kunipa mawazo yenu wana jukwaa?

Nawasilisha.
 
Huwa nabet ila kwa wiki haizidi 10000/ isipozaa potelea mbali sina cha kulaumu. Kikubwa 1. limit kiwangi cha kutumia katika kamari, 2. Fungua fixed account ukipata pesa I.e 50000 kwa siku hamisha 30000 baki na 20000 hivyohivyo.. Utajikita siku zote unapesa kidogo mfukoni ila account yako inajaa.. By doing so pesa kidogo itakuwa inaenda kwenye kamari na hutajuta
 
Huwa nabet ila kwa wiki haizidi 10000/ isipozaa potelea mbali sina cha kulaumu.. Kikubwa 1. limit kiwangi cha kutumia katika kamari, 2. Fungua fixed account ukipata pesa I.e 50000 kwa siku hamisha 30000 baki na 20000 hivyohivyo.. Utajikita siku zote unapesa kidogo mfukoni ila account yako inajaa.. By doing so pesa kidogo itakuwa inaenda kwenye kamari na hutajuta
Wazo zuri sana,ndio maana panaitwa great thinker.
 
Unashindwa nini kuwekeza kwenye miradi midogo kila baada ya muda flani. Kila mwezi ukiwekeza kwenye mradi wa M moja na mwezi ufatao unaongeza mtaji au unafungua mradi mwingine utatunza hela, utarudisha hela, utapata faida na utakuwa na hela kwenye mzunguko.

Inaonekana huna uwezo wowote wa kuanzisha biashara kwa kuwa umezoea hela za ganji. Na wakati huo huna uwezo wa kusimamia. Wacheza kamari hawajawahi kujua kusimamia chochote, ona hata wewe hujui kutoka gambling.

Weka mtu kisha mpe mandate, yeye arejeshe kiasi kadhaa kwa muda flani. Wewe endelea na kulewa, wanawake na bata za ovyo. Najua haya hayakwepeki kwa gamblers. Mwisho nalenga kukwambia acha hizo mambo.
 
Wenzako wenye uraibu na hizo kamari huwa wanakabidhi funguo za gari zao mezani. Wanarudi nyumbani na kirikuu ya kubeba friji na sofa ili kuziuza kupata hela ya kuchezea kamari tena ili kurudisha gari. Nayo inapigwa tena, bhas nyumba ndio unafatia inauzwa kidogo kidogo..sasa wewe bado muoga kwenye kamari kabisa hujafikia uraibu.
 
Bila shaka kutakuwa pia na nguvu ya ziada kutoka kwa Ibilisi inayokusukuma kufanya jambo hilo. Nenda kaombewe kwa Jina la Yesu Kristo haraka sana kabla hali haijawa mbaya na ukajikuta unafilisika kabisa.
 
Ungejua ni jins gan wanaomiliki michezo hyo wanavyotupia majini kwenye hzo mashine na mchezo husika. ..usingeamini...unahis hyo adiction inatokana na nn...mkuu biashara hzi zina siri...kuna majin yanazunguka huko kama hayana akil nzur...waulize wanaobet....match zile zile ambazo alikua na wasiwas nazo ...na ndo hzo hzo mwisho wa siku anazicheza analiwa..hahah
 
Poleni na hekaheka za campaign wana JF.

Moja kwa moja kwenye mada.

Mimi ni mwathirika wa kamari, nacheza mchezo wa roulette kwa sana kuanzia cassino na popote napokutana na hilo dude.

Nimeajiriwa na kipato changu si haba maana nikichukua mshahara wangu pamoja na ganji nazopata kazini nina uhakika wa kutengeneza zaidi ya milion 5 kwa mwezi.

Maana nina uwezo wa kupata kati ya 50,000 hadi laki 300,000 kwa siku hapa inategemea na hali ya siku yenyewe na hii ni pamoja na uchumi wa anko Magu kuwa hivi.

Pamoja na pesa zote hizo pesa pekee nayoweza kuiweka kwenye account ni kati ya laki 5 na m1 tu zingne zote naliwa kwenye ulaibu huu.

Hivyo nikikaaa bila kwenda kwenye kamari miezi 3 hua nafanya maendeleo makubwa.

Bahati mbaya pesa zote hizi zinaishia kwenye kucheza kamari.

Nimejitahidi kujaribu kuacha wapi,nimetembelea wataalamu wa psychology lakini sijaona mafanikio

Nashukuru nimejenga nyumba nzuri ya ndoto yangu pia usafiri wa haja ninao.

Nasikitika kwamba naweza kuwa na m1 asubuhi usiku sina hata pesa ya kuweka mafuta asubuhi.

Binafsi ninapambana kuacha hii kitu lakini sijui nianzie wapi kuacha.

Nishatangaza dau hata kwa mtu anaeweza nisaidia kuacha kamari lakini hakuna msaada.

Natamani nihamie mikoa ambayo hakuna haya madude bahati mbaya kazi yangu haina tawi kwa ofisi nayofanyia kazi.

Ukweli huwa naweza kushinda pesa kubwa tu kwenye hii kamari hata m10 kwa siku lakini inakuchukua hata siku 5 unapewa kipigo tena!

Mnaweza kunipa mawazo yenu wana jukwaa?

Nawasilisha.
Mkuu fanya forex lazima utakua milionea yani hyo m5 ni kama $ 2,200 ukitia zako lot size ya moja unambamiza broker vibaya sana.
 
Mkuu fanya forex lazima utakua milionea yani hyo m5 ni kama $ 2,200 ukitia zako lot size ya moja unambamiza broker vibaya sana.
Aaaah! Forex gani inayotoa hela kirahisi namna hiyo. Mtu ambaye hawezi kujizuia kucheza kamari ukimwambia afanye forex trading ni sawa na kumwambia mtu ili asiwe mlevi aache Konyagi anywe K-Vant wakati vyote vilevi.

Sheria ya kwanza kutrade lazima usiwe na tamaa. Yeye anazo maradufu.
 
Back
Top Bottom