Mitandao ya kijamii imejengwa kwa mfumo wa attention economy ambao unachochea hamu ya kupata likes na comments kila wakati. Hii inaharibu sana uwezo wa kijana kujistiri kwa sababu anajiona thamani yake inategemea jinsi anavyokubaliwa na watu asiowajua.
Tunahitaji kurudisha thamani ya tangible achievements, furaha anayopata kijana inapaswa kutokana na michezo, sanaa, au miradi ya ujasiriamali, badala ya kutafuta virtual validation.
Tunapaswa kurudisha physical hobbies ili kupunguza muda wa wao kukaa mtandaoni.