Akili inaporuhusu kutazama ndio macho huona!

Akili inaporuhusu kutazama ndio macho huona!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,170
Reaction score
866,416
Na hayo macho hayawezi kuona hivi hivi ni mpaka yaangalie.... Ni kama mafiga matatu.. Kazi yake hutimia yakiwa yote pamoja bila upungufu... Kutazama, kuangalia na kuona
Unaweza kutazama usione
Unaweza kuangalia bila kuona

Lakini je unaweza kuona bila kutazama!? Unaweza kuona bila kuangalia. Unapofundishwa kuwa mwerevu kama nyoka haimaanishi uwe na IQ kama ya mende. Ni lazima kuna codes ziruhusu mwanga wa taa ya mawasiliano ndio macho yanaweza kutazama na kuona. Kinyume chake macho yataangalia bila kuona

Kinyume chake utaangalia tu lakini mwanga wa kuruhusu kuona ukiwa umezimwa ama mionzi yake ikiwa imeelekezwa kwingine kabisa na hii sio hiari yako. Ni sawa na security camera. Unapoitazama ni kama inakuangalia lakini si wakati wote inakuona kwakuwa kinachokuona kuna wakati hukioni na kimeangalia kwingine kabisa.

Tumetoka kwenye mapumziko ya sikukuu ya kuhitimisha mfungo wa Kwaresma. Pasaka! Kwakuwa hili ni jambo la kiimani basi tusilipe nafasi kubwa hapa bali tuangalie wakati tulio nao. Wakati huu wa mwezi wa nne ambao siku yake ya kwanza, yaani tarehe mosi inajulikana kama siku ya wajinga duniani. Na hakuna mwaka imekosa wateja.

Tuiangalie April hii kwa jicho la kipekee mno. Pengine huko mbeleni tutakuja kuangalia mahusiano na tafsiri yake kiroho 42018 kwa kutumia magazijuto ya kiroho.

Kuna kitu hakiko sawa sana. Tai ni ndege mahiri kwa uwindaji.. Hukaa juu sana angani akiangalia na kuona vizuri sana mlo wake ulipo. Hupiga hesabu zake kwa makini toka alipo, kasi atakayotumia mpaka kuufikia mlo wake hata kama utajaribu kusogea kwa kasi yoyote ile. Akikosea Tai basi jua ni bahati mbaya sana

Tofauti na tai kuna wawindaji wengine wa mwituni wenye ubabe mwingi simba chui fisi nk.. Hawa hawana akili ya tai japo wanajaribu kumuiga. Hawa kwao maguvu mengi akili kidogo ndio hulka yao. Kwenye Kutafuta mawindo yao.

Huanza na kasi ya ajabu bila kujua kwa hakika atamkamata nani. Na mwindwaji akiwa mwerevu akaweza kupiga chenga kadhaa. Wababe hawa wa mwituni huishia kukosa mlo walioumezea mate

April yetu imekaa kama pori kubwa linalowakutanisha wababe na wapole, wenye nguvu na wasio na nguvu.. Werevu na maboya.. Wenye kutumia nguvu nyingi na akili kidogo na wenye kutumia akili nyingi na nguvu kidogo......
Nyumbu na upimbi wake wote na uoga wake wote hufika mahali akamvimbia mbabe na mbabe akakaa chini.... Nyumbu akiamua kufanya hivi kila siku mbabe atageuka mawindo ya wengine.....

Kuna tai mbali juu kabisa angani anapaa kwa pozi zote hana haraka lakini anapaa kwa step. Jicho lake linatazama na kuona mbali... Anajua ni muda gani atashuka kwa kasi na kunyakua kilicho chake. Ndugu zangu na mimi kutwa kuchwa kuhangaika na pori. Liwe jua iwe mvua. Kuwe na tufani ama la ni kulivuruga pori tuu. Sasa si swalapala, ndezi nyumbu, pundamilia wameshaanza kuona udhaifu uliko. Wamejipanga kwa kuligawa pori lote kwa makundi ya umoja

Muda wa njaa ukifika wale carnivore wote wapenda nyama mbichi iliyo na damu watahangaishwa pori zima na ndezi hawa. Na kima hawa... Na nyumbu hawa. Watapigwa chenga za mwili mpaka waombe pooo. Kishapo kwa upole kabisa ila kwa kasi ya ajabu tai atamshukia mmoja na kumnyakua juu angani..

Iko hivi, Akili isiporuhusu kutazama basi macho hayataona.. Lakini kwanza ni lazima yaangalie

IMG_20180331_092005_353.jpg
 
Back
Top Bottom