Akikuchomekea mtoto dawa ni moja tu!

maishapopote

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
3,506
Reaction score
6,450
Wanawake sasa hivi wana roho ngumu kuliko Lilith (usiniulize ni nani), kukuchanganyia mtoto kwenye ndoa, kwake haombi hata ushauri.

Wewe cha kufanya kausha halafu jifanye hujui kabisa, then mpende huyo mtoto kweli kweli, hakikisha anasoma mpaka mwisho. Mpende kwa matendo na maneno.

Halafu akiwa mtu mzima mwambie mtoto ukweli bila kumwambia mama yake kitu, mwambie nilijua ila niliamua kukaa kimya, wakati huo akiwa na kazi yake, halafu kaa kimya.

Muziki utakaofuata hapo we kaa pembeni!
 
Hawa hakuwa anaitwa Lilith mkuu,it is a lie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…